Mizengo Pinda aomba kujiuzuru

na akicheza cheza kusubiri mpaka june tuna mchinjia baharini na zamu ya dada/akina mama
 
... Endapo prof lipumba atakubali kujiunga na hili li baraza la mawaziri uozo la ccm hakika nitamdharau milele na kutilia wasiwasi utashi wake na kazi ya usomi wake pia!!!!!!!!

Acheni ccm kimalizie uchafu wake wote kama walivyouanza mara baada ya mwalimu nyerere kufa ili hukumu ya walalahoi kwa chama hiki hivi karibuni isije ikasambaa hata kwa vyama ambavyo havihusiki na uhandisi wa ufisadi wote wanaolifanyia taifa hili.

hapa apewe kazi mrema tu
 
Kabla ya sakata hili,lakini siyo kuhusiana na sakata hili,Rais Kikwete alisema kwamba hataki Waziri Mkuu Pinda ajiuzulu. Kwa hiyo Pinda akijiuzulu sasa itakuwa Rais amebadili mawazo yake.
Zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM.

 
Mzee apumzike tuu ameshachoka .Baba riz amemzunguka sana na wenzake bila yeye kujua
 
Mliosoma gazeti la RAIA MWEMA la leo kuna article ya ndefu pg. 08 yenye headline isemayo BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.

Ukihesabu utaona kuwa article ina paragraph 31. Siwezi kukopi paraghraph zote bali nakopi ya 20 na 21 kama ifuatavyo:

20:
..Kuna uvumi umeenezwa kuwa Waziri Mkuu ameomba kupumzika asiwemo katika Baraza jipya (linalosukwa upya). Inadaiwa kuwa Mzee Pinda amesisitiza kuwa asifikiriwe kuendelea kuwa Waziri Mkuu kwa sababu anadai amechoka na kuwa yupo tayari kusaidia kwa njia nyingine..

21:
..Inasemekana wametumwa watu kadhaa kumwomba Mzee abadili uamuzi wake huo na kwamba atapewa timu bora zaidi ambayo haitampa kazi kuiongoza....

Nasisitiza, thread haina matatizo yoyote kwani nimekopi wanachokisoma mtaani kupita gazeti hili, RAIA MWEMA wana mtindo ikipita siku moja wanaweka kwenye website yao na tukijifanya tunaiogopa kwa kui-move au kuifuta basi hatutawazuia forum zingine wawe wa kwanza kuishadidia mjadala bila uoga.

SOURCE: RAIA MWEMA
DATE: MAY 02, 2012
PAGE: 08

Mizengo amedhalilishwa vya kutosha ni bora akapumzika,kwanza ilikuwa kazi kubwa kumshawishi kukubali nafasi ya uwaziri mkuu baada ya uchaguizi mkuu 2010 na alikubali kwa shinikizo kwa hiyo nadhani niwakati muafaka kwake kupumzika atakuwa majijengea heshima kubwa.

Ila ieleweke kuwa hata Raisi akivunja baraza na kuunda jipya waziri mkuu nafasi yake iko palepale maana hachaguliwi na raisi,raisi anapendekeza jina then wabunge ndio wanaompitisha kwa hiyo mabadiliko ya mawaziri hayamuhusu wala hayagusi nafasi ya Pinda,ila kikatiba ikitokea Waziri mkuu akajiuzuru hapo baraza huwa lazima livunjwe.Nawasilisha
 
Mtoto wa mkulima keshasoma upepo wa kisiasa ndani ya nchi. So kubakia na heshima individually kabla meli ya CCM haijazama 2015 kupumzika ndio uamuzi mkuu. Hongera mzee Pinda
 
Mliosoma gazeti la RAIA MWEMA la leo kuna article ya ndefu pg. 08 yenye headline isemayo BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI.

Ukihesabu utaona kuwa article ina paragraph 31. Siwezi kukopi paraghraph zote bali nakopi ya 20 na 21 kama ifuatavyo:

20:
..Kuna uvumi umeenezwa kuwa Waziri Mkuu ameomba kupumzika asiwemo katika Baraza jipya (linalosukwa upya). Inadaiwa kuwa Mzee Pinda amesisitiza kuwa asifikiriwe kuendelea kuwa Waziri Mkuu kwa sababu anadai amechoka na kuwa yupo tayari kusaidia kwa njia nyingine..

21:
..Inasemekana wametumwa watu kadhaa kumwomba Mzee abadili uamuzi wake huo na kwamba atapewa timu bora zaidi ambayo haitampa kazi kuiongoza....

Nasisitiza, thread haina matatizo yoyote kwani nimekopi wanachokisoma mtaani kupita gazeti hili, RAIA MWEMA wana mtindo ikipita siku moja wanaweka kwenye website yao na tukijifanya tunaiogopa kwa kui-move au kuifuta basi hatutawazuia forum zingine wawe wa kwanza kuishadidia mjadala bila uoga.

SOURCE: RAIA MWEMA
DATE: MAY 02, 2012
PAGE: 08

Kama kweli PM Pinda anataka kujiuzulu, ingawa amechelewa lakini bado ana nafasi.. sababu ni nyingi lakini, mosi ni kulinda heshima yake na pili kwenye hii regime ya JK na chama chake (CCM) yeye amewekwa kuwa kama rubber stamp tu... how come Prime Minister hawezi kumwajibisha Katibu Mkuu wa Wizara au Mkurugenzi hata pale inapoonekana wazi kuwa ameshindwa kuwajibika!? It's shame kwa kweli.. personally naunga mkono kujiuzulu kwake kwani ndo itakuwa heshima kwake na kwa future ya familia yake.. hawatasodolewa kama "EL" aliyeshinikizwa kujiuzulu na kubakia kusema TATIZO NI UWAZIRI MKUU...
 
21:
..Inasemekana wametumwa watu kadhaa kumwomba Mzee abadili uamuzi wake huo na kwamba atapewa timu bora zaidi ambayo
haitampa kazi kuiongoza....


SOURCE: RAIA MWEMA
DATE: MAY 02, 2012
PAGE: 08

am i missin somethin here....kwani hili baraza limekua ka watoto wa shule ya msingi kua ni watukutu kiasi ambacho kiranja anamwomba mwalimu asimpe tena ukiranja maana wanafunzi ni sugu mno
 
kumbe ndiye anaayecheleweshwa kutangwaza kwa Baraza Jipya. So wanasubiri mpaka akubali ombi?

Jamaa lazima ajiuzulu. Nikikumbuka ile ya Madaktari namuonea Huruma.

Mwacheni apumzike kwani ukiangalia tangu alivyoteuliwa hajafanya lolote la maana, heri ya Lowasa alihimiza shule za kata. Wazirii mkuu lazima uwe wa vitendo, lakini Pinda kwenye ile issue ya Jairo alishindwa kushauriana na Makamu wa rais kutoa mahamuzi lakini alichoweza kusema ni " Hili liko nje ya uwezo wangu, lakini rais atakaporudi kutoka pretoria nitamshauri" Kwani rais hajarudi hadi leo? Rais alisafiri na Makamu? Nchini alibakia nani? Waziri mkuu analilia tuuuu!!!!!!! Utafikiri anaomboleza.... Let him resign

 
Hivi kumbe watu bado kabisa hamjui katiba. Kwani mmesahau kuwa waziri lazima atoke miongoni mwa wabunge? Sasa Lipumba ni mbunge wa wapi? Hili haliwezekani msitupotezee muda.

Mimi si mbunge lakini naweza kuwa waziri pale tu Rais atakapotumia nafasi zake kumi za kuteua wabunge akaniteua na kunipa Uwaziri. Wewe ndio hujui mkuu.
 
Nimetoka kuisoma makala ya MSOMAJI RAIA KTK RAIA MWEMA ....Kuna maneno kayaandika naomba kuwashirikisha wadau mnaonaje kuhusu pinda kujiweka pembeni kama kweli itatokea...


Baraza jipya la mawaziri


Pinda alifanya kosa, asirudie kosa

Msomaji Raia

Toleo la 237
2 May 2012













WAKATI makala hii inasomwa, huenda tukawa tayari na baraza jipya la mawaziri. Laweza kuwa jipya, au lenye viraka, lililosukwa upya au vyovyote vile, lakini cha msingi ni kuwa tutakuwa na kitu kinachoashiria kuwa ni kipya.
Hatua hii inafuatia mjadala ulioibuka bungeni kuwa mawaziri wanane wameshindwa kufanya kazi zao vizuri na kusababisha ubadhilifu wa fedha za umma katika wizara zao.
Kamati Kuu ya chama tawala cha mapinduzi (CCM), ama ikaunga mkono au ikashinikiza yafanyike mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri.
Makala hii haina lengo la kuwatetea walioshinikizwa kujiuzulu au kuwahukumu, inalenga kuwatahadharisha baadhi ya watu ninaowaheshimu.
Baba wa Taifa aliwahi kusema kuwa “inahitaji mtu uwe na moyo wa mwenda wazimu kutetea Azimio la Arusha”. Wakati ule aliona mwendokasi wa kupuuza maadili ya uongozi wa kisiasa na katika utumishi wa umma kuwa ulikuwa unatisha.
Kwa mantiki ile ile, mtu anahitaji kuwa jasiri sana kutetea yanayoelezwa kufanywa na viongozi wetu wa kisiasa kama tulivyoshuhidia bungeni majuzi.
Kwa kuwa sasa tuhuma hizi zinasemwa na wenye chama wenyewe na kwamba wameridhia kuwa Serikali isukwe upya kwa sababu ya ufisadi wa mawaziri hiyo ni hatua moja kubwa imefikiwa.
Hapa nina maana kuwa mawaziri wanaoitwa wezi na mafisadi hawakuanza tabia hiyo walipoteuliwa kuwa mawaziri.
Tabia hii waliianza mapema kabla hawajajitupa uwanjani kugombea ubunge. Kama walihonga ili kununua kura, au kama waliiba kura ili kushinda, hawakufanya hivyo kwa ajili yao wenyewe.
Walifuata sera ya mafiga matatu (diwani, mbunge na rais). Jinai hiyo ya kuhonga na kuiba haitakwisha katika fikra za watu hivi karibuni.
Kimsingi, anayeteua mawaziri ni yule yule aliyeteua hawa walioshindwa na kuachwa katika baraza jipya. Ukiwauliza walioachwa katika baraza hili na waliowahi kuachwa katika mabaraza yaliyopita ya Rais huyu huyu, wanakueleza kuwa tatizo ni la aliyewateua na si tatizo lao.
Kwamba, Rais akishawateua anaacha kuwaamini na kuwasikiliza au akiwasikiliza hafuati ushauri wanaompa.
Kwamba, wakati wote wa kutekeleza majukumu yao ya uwaziri, hawakuwa na uhakika kuwa watalindwa na kuheshimiwa na yule aliyewateua.
Ni hali hii hii ambayo watu wengi wamekuwa wakiichambua kuwa pale wanapopata matatizo, wateule wengi hutoswa pale wanapoingia katika matatizo ya kiutendaji.
Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda amepata misukosuko mingi ya kisiasa tangu ateuliwe kuwa Waziri Mkuu. Yawezekana sana hakujua nini kitamtokea alipokubali kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Alishindwa kujiuliza ni kwa nini Rais alishindwa kumlinda swahiba wake wa siku nyingi. Kosa la kushindwa kujiuliza swali hilo, hivi sasa linamgharimu sana. Mara nyingi ama amelazimika kushughulikia madhara ya maamuzi mabovu au maamuzi yaliyochelewa sana. Na wakati wote huo, Pinda huwa hana uhakika kama bosi wake atasimama naye hadi mwisho wa safari.
Tumeyaona ya sakata la David Jairo, misamaha ya kodi kwa mashirika ya dini, Mahakama ya Kadhi, mgogoro wa madaktari na sasa mgogoro wa shinikizo la kujiuzulu kwa mawaziri.
Wakati wa misukosuko hiyo, tumeona kwa hakika kuwa Rais anawasikiliza na kuwaamini baadhi ya mawaziri kuliko anavyomuamini Waziri Mkuu Pinda.
Hata katika sakata nyinginezo, Pinda amejikuta anasikilizwa akiwa mtu wa pili. Hii ingetosha kumfanya Pinda aombe kupumzika kuliko kusubiri siku moja kupumzishwa bila kujiandaa.
Kosa la kukubali kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu linasameheka, lakini la kukubali kuendelea hata baada ya Serikali hii kupata likizo ya wiki moja na zaidi, nina mashaka kama litasameheka.
Kuna uvumi umeenezwa kuwa Waziri Mkuu ameomba kupumzika asiwemo katika baraza jipya (lililosukwa upya). Inadaiwa ya kuwa Mzee Pinda amesisitiza kuwa asifikiriwe kuendelea kuwa Waziri Mkuu kwa sababu anadai amechoka na kuwa yupo tayari kusaidia kwa njia nyingine.

Inasemekana wametumwa watu kadhaa kumwomba Mzee abadili uamuzi wake huo na kwamba atapewa timu bora zaidi ambayo haitampa kazi kuiongoza. Natamani hizi ziwe ni tetesi za kweli kama zilivyo nyingine ambazo hukanushwa lakini zikabakia kuwa za kweli.
Kama Mzee Pinda ameamua hivyo amefanya vema. Pinda ni mtu muungwana na uungwana wake ndio kitanzi chake cha hatari.
Kupitia uungwana wake, amedhalilika mbele ya umma na kuishia kuuguza vidonda vya tumbo.
Kazi ya punda anayoifanya ili kufunika aibu ya Serikali hii, haijampatia heshima mbele ya waliomteua. Kwa kuwa sasa imetokea fursa kuwa baraza linaundwa upya, ni ruksa na busara kwake yeye kumwomba Rais apumzike hata kama kwa kufanya hivyo atatafsiriwa kuwa ameogopa na ni mdhaifu.
Uamuzi wa Mzee Pinda kuomba kupumzika kama ni wa kweli, unapaswa kuigwa na wabunge wote waliobakiza chembechembe za maadili katika maisha yao ya uongozi wa umma.
Kukosekana kwa uadilifu miongoni mwa baadhi ya mawaziri kunawatesa wale wachache walio waadilifu. Imefikia hatua sasa kuaminika kuwa hakuna mtu mwadilifu ndani ya Serikali ya CCM na hakuna hatua zinazochukuliwa.
Kutowachukulia hatua viongozi wasio waadilifu kunawaumiza na kuwakatisha tamaa wale walio waadilifu katika utumishi wa umma.
Pinda huyu akatangaza kuwa ni mwiko kuagiza magari ya kifahari, bado yakaagizwa. Pinda akapiga marufuku misafara mirefu ya magari katika ziara za viongozi, badala ya kupungua ikaongezeka. Pinda akapiga marufuku semina maofisini; zikaachwa au kupunguzwa lakini malipo yakabaki pale pale. Pinda akaagiza watendaji watoke maofisini waende kutembelea miradi na kusikiliza kero za wananchi; matokeo yake hata waliokuwa field wakarudi maofisini na kuacha kabisa kwenda.

Pinda akatoa waraka wa kuhakiki watumishi hewa, badala ya kupungua wakaongezeka. Pinda anatoa amri kwa watendaji, kabla hawajatekeleza, wanamuuliza Rais au Waziri Mkuu aliyepita ikiwa watekeleze au waache.
Pinda anapokea maagizo kutoka kwa wasaidizi wa Rais hata yale yaliyo kinyume cha yale aliyoagizwa yeye mwenyewe binafsi na Rais. Jambo moja Mzee Pinda amebakiza, nalo ni heshima na huruma ya Watanzania wanaomwona akilialia kila anapokumbana na dhoruba za kisiasa.
Kama atafanya kosa la kukubali wajibu wa uwaziri mkuu, ajue kuwa huruma hiyo hataipata tena maana muda uliobaki kabla ya siasa za uchaguzi ni mfupi. Si ajabu katika baraza hili jipya ndimo alimo Rais ajaye na huyo hawezi kukubali kumtii Pinda wakati anataka kuweka mikakati ya ushindi. Kwa kuwa Pinda hapendi urais wala ubunge mwaka 2015, apishe kwa wema ili wenye meno waendelee kula nchi.
 
Unaendelea kuonyesha kutokujua kwako sheria za nchi!

Nilipokuita kilaza nilikuwa nina maana hujui unachokisema na sasa umethibitisha.

HAKUNA KIFUNGU KATIKA KATIBA KINACHOMBANA RAIS KUTEUA MBUNGE WA CHAMA CHOCHOTE KUWA WAZIRI! ISIPOKUWA KWA PM NDIO UTARATIBU UMEELEZEWA NI ATOKE CHAMA CHENYE WAJUMBE WENGI. FULL STOP

Case ya znz ni completely different, wamebadilisha muundo wa serikali kutoka waziri kiongozi, kwenye two VP na

mengineyo ilikuwa ni lazima KATIBA ichakachuliwe.

Nimekwambia kaakimya kama hujui

kweli katiba haizuii hilo unalosema, lakini na wewe yawezekana ni kilaza pia maana umekomaa kutetea kuwa Lipumba anaweza kuwa waziri kwenye serikali hii-hihii? hii-hii? ya JK?. Kwa ubishi wako nakufananisha na rafiki yangu mmoja kutoka kabila moja kule Kigoma, wabishi haoooooooooooooo mpaka kero.
 
Wakuu walitia sahihi zao kuwa atoke yeye kakomaa tu hivi hajisikii aibu.
 
Back
Top Bottom