Miwasho baada ya kuoga inatibika vipi?

Miwasho baada ya kuoga inatibika vipi?

Do this

Usitumie dodoki kujisugua..tumia tu mikono..then ulete mrejesho hapa.

Pia tumia maji ya uvuguvugu kuogea.
Hiyo ndiyo dawa mimi nilikuwa na tatizo hilo nilishauriwa hivyo, sijisigui na dodoki tatizo limeisha.
 
Hilo tatizo haliishi ila unaweza kulicontrol na kuishi nalo, Mimi toka nijifahamu nimekua nalo, now nimekua mkubwa najua cha kufanya.

Kwanza lazima ufahamu kuwa unaasili ya ngozi kavu ndio maana unawashwa ikikutana na vitu kama 1.Maji ya baridi sana, 2. Maji ya moto sana. 3. Baridi au upepo mkali baada ya kuoga, 4. Sabuni yenye manukato na kemikali kali, 5.kujifuta mwili na nguo au taulo lenye unyevu, au chafu 6.kujisugua mwili na dodoki gumu au kujisugua sana 7.Kusugua mwili kwa scrub.

Sasa kazi kwako kuavoid hizo situations, Usioge maji ya moto sana au ya baridi sana pendelea ya uvuguvugu, Epuka sabuni za manukato kama alivyosema mdau hapo juu, sugua mwili kwa mikono tu au kitambaa laini, ukimaliza kuoga usikae na maji, jikaushe kwa taulo/nguo safi then paka mafuta mazito yenye moisture then stay hydrated. Halafu tuletee mrejesho.

Mimi hizo measures zimenisaidia siku hizi siwashwi kabisa siku zingine nawashwa kwa mbaali nikikosea step. Waliokwambia juu ya kwenda hospitali, unaweza kujaribu lakini kwangu mimi dawa nilizopewa hazikufanya kazi, Ohh its bad, nilikua sipendi wala sifurahii kuoga.
hapana hilo sio jambo la kuzoeleka ... kuwashwa baada ya kuoga kunaweza sababishwa na mambo ma3
1.Fangasi
2.Kutumia taulo chafu lililovunda kwa maji (ambalo halikuanikwa juani baada ya kutumika ambalo huzaa bacteria wanaoathiri ngozi na kupelekea miwasho)
3.Kuchezea manyasi (vijijini)

kwa hiyo jambo hilo sio la kawaida ni either una moja ya haya mambo ma3 kamuone daktari aljekaribu nawe pia kwa ushauri zaidi usikubali kuteseka na miwasho
 
kuna wale ambao wanatumia sabubi za magadi kisha wanaogea maji chumvi hili pia ni tatizo ambalo linaweza kusababisha miwasho ktk ngozi pindi inapogusa maji ,,, kuna madini katika sababu za magadi ambayo yakichanganyika na maji chumvi basi huleta shida ,, pia sabuni zenye harufu ya kunukia huwa baadhi huwa madini hayo.
 
Habari zenu wana Jamii Forum. Poleni kwa changamoto na mchaka mchaka wa utafutaji pesa na kadhalika.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Mimi mwenzenu katika hili jukwaa la Urembo, mitindo na Utanashati nahisi nnashida ambayo inanitesa sana saivi ni takriban miaka minne. Yani iko hivi, shida ninayoipitia ni kwamba kila nikitoka kuoga nahisi kuwashwa washwa kwenye ngozi kila mahali ya mwili wangu hata sometimes nikitaka kuoga naanza kua na mawazo. Yani kila nikimaliza kuoga nawashwa karbia dakika 15 au 20, kila sehemu ya mwili inawasha lakini hauvimbi wala nini. Na baada ya hizo dakika 15 au 20 za kuwashwa kuisha naendelea na maisha freshi tu kama hakukua na tatizo lolote.

Nimesha badilisha kila aina ya sabuni na madodoki nikihisi pengine labda chanzo ndo hiko lakini hii hali bado inanisumbua vibaya mno.

Sasa wadau wangu wa Jamii Forum hasa katika hili jukwaa kwa wale ambao wameshapitia hii hali na ambao hawajapitia lwa ujumla. Naombeni ushauri nifanyeje ili niondokane na hii hali maana inanitesa sana.
Duuh, pole sana mkuu.
Nami nimeishi na hili tatizo mwaka wa 10 sasa, sijawahi kupata ufumbuzi. Nimefikia hatua ya hata nikitokwa na jasho nawashwa ila sivimbi.
Ninachofanya siku hizi huwa nikioga sijisugui kwa wavu wala kitu chochote kigumu lakini pia baada ya kuoga najifuta na kitambaa chepesi sana au kanga, imenisaidia kupunguza tatizo japo bado lipo.
 
Habari zenu wana Jamii Forum. Poleni kwa changamoto na mchaka mchaka wa utafutaji pesa na kadhalika.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Mimi mwenzenu katika hili jukwaa la Urembo, mitindo na Utanashati nahisi nnashida ambayo inanitesa sana saivi ni takriban miaka minne. Yani iko hivi, shida ninayoipitia ni kwamba kila nikitoka kuoga nahisi kuwashwa washwa kwenye ngozi kila mahali ya mwili wangu hata sometimes nikitaka kuoga naanza kua na mawazo. Yani kila nikimaliza kuoga nawashwa karbia dakika 15 au 20, kila sehemu ya mwili inawasha lakini hauvimbi wala nini. Na baada ya hizo dakika 15 au 20 za kuwashwa kuisha naendelea na maisha freshi tu kama hakukua na tatizo lolote.

Nimesha badilisha kila aina ya sabuni na madodoki nikihisi pengine labda chanzo ndo hiko lakini hii hali bado inanisumbua vibaya mno.

Sasa wadau wangu wa Jamii Forum hasa katika hili jukwaa kwa wale ambao wameshapitia hii hali na ambao hawajapitia lwa ujumla. Naombeni ushauri nifanyeje ili niondokane na hii hali maana inanitesa sana.
Unaweza ukadondoshea kwenye maji PP solution kifuniko japo kimoja....
 
Ni minyoo wa kwenye ngozi mi nilisumbuliwa sana nikanywa dawa ya kienyeji ya wamasai nikapona mwanzoni nilihisi sabuni hola nikahisi maji hola nikahisi dodoki hola baadae jikamweleza dokta mmoja wa ngozi akaniambia kuna dawa ya sindano kuchoma au vidonge,au nikiamua nitafute ya kienyeji ndio nikapata kwa mmasai huyo alienda nichimbia nikainywea kwenye kahawa ila ilikuwa chungu balaa nimepona mpaka leo tatizo limeisha
Yawezekana kweli ikawa minyoo ya kwenye ngozi
 
hapana hilo sio jambo la kuzoeleka ... kuwashwa baada ya kuoga kunaweza sababishwa na mambo ma3
1.Fangasi
2.Kutumia taulo chafu lililovunda kwa maji (ambalo halikuanikwa juani baada ya kutumika ambalo huzaa bacteria wanaoathiri ngozi na kupelekea miwasho)
3.Kuchezea manyasi (vijijini)

kwa hiyo jambo hilo sio la kawaida ni either una moja ya haya mambo ma3 kamuone daktari aljekaribu nawe pia kwa ushauri zaidi usikubali kuteseka na miwasho
1. Fangasi... ya wapi? ngozi yote?
2.Mimi situmii taulo kabisa, natumia kanga nyepesi/kikoi chepesi atleast kimoja kwa siku moja, asubuhi na jioni. Unaniambiaje kuhusu hilo?
3. Nimekua kwa madaktari since i was 15.

I'm afraid hili tatizo umeli-underestimate. Hii ni aina fulani ya mzio ambao kuutibu sio rahisi, mara nyingi unahusishwa na ukavu wa ngozi na pumu ya ngozi.... Pitia upya makabrasha.
 
Nilimeza cetrizen mpaka nilikoma sijui hata ule muwasho ulipoteleaga wapi.
Mi mwenyewe umefika muda siwashwi kabisa au nawashwa kiasi kidogo sana. Ila zamani ilikua balaa kubwa sana 😅 my mam used to feel sorry for me kwa ninavyojikuna.
 
Nina hili tatizo pia toka 2003. Nikioga mwili unawasha sana hadi muda mwingine nikiwaza hii hali nakosa mood ya kuoga. Nina allergy pia ya nyama nyekundu na maziwa fresh toka 2001
 
Back
Top Bottom