Miwasho baada ya kuoga inatibika vipi?

Miwasho baada ya kuoga inatibika vipi?

Habari zenu wana Jamii Forum. Poleni kwa changamoto na mchaka mchaka wa utafutaji pesa na kadhalika.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Mimi mwenzenu katika hili jukwaa la Urembo, mitindo na Utanashati nahisi nnashida ambayo inanitesa sana saivi ni takriban miaka minne. Yani iko hivi, shida ninayoipitia ni kwamba kila nikitoka kuoga nahisi kuwashwa washwa kwenye ngozi kila mahali ya mwili wangu hata sometimes nikitaka kuoga naanza kua na mawazo. Yani kila nikimaliza kuoga nawashwa karbia dakika 15 au 20, kila sehemu ya mwili inawasha lakini hauvimbi wala nini. Na baada ya hizo dakika 15 au 20 za kuwashwa kuisha naendelea na maisha freshi tu kama hakukua na tatizo lolote.

Nimesha badilisha kila aina ya sabuni na madodoki nikihisi pengine labda chanzo ndo hiko lakini hii hali bado inanisumbua vibaya mno.

Sasa wadau wangu wa Jamii Forum hasa katika hili jukwaa kwa wale ambao wameshapitia hii hali na ambao hawajapitia lwa ujumla. Naombeni ushauri nifanyeje ili niondokane na hii hali maana inanitesa sana.
Tafuta Acrason cream changanya na kwenye kopo la mafuta ya Vaseline Mil. 100. Unapaka kila unapotoka kuoga unajipaka mwili mzima kama unavyojipaka kawaida.
 
Kama umebadili sabuni bila mafaniko basi inaweza kuwa maji
Fanya hivi
Uwe unaweka dettol ya maji kidogo kwenye maji yako ya kuoga,

Pia jaribu kutumia showergel

100%
 
Nimesha badilisha kila aina ya sabuni na madodoki nikihisi pengine labda chanzo ndo hiko lakini hii hali bado inanisumbua vibaya mno.
Usibadilishe dodoki, achana na dodoki kila mara.

Litumie siku ukilikumbuka mara moja moja. Dawa ya aleji ni kuikimbia hali inayopelekea itokee
 
Wengine huwa ni damu kuzidi mwilini. Huwa wanawashwa wakioga, hasa wakioga maji ya moto.
 
Ni minyoo wa kwenye ngozi mi nilisumbuliwa sana nikanywa dawa ya kienyeji ya wamasai nikapona mwanzoni nilihisi sabuni hola nikahisi maji hola nikahisi dodoki hola baadae jikamweleza dokta mmoja wa ngozi akaniambia kuna dawa ya sindano kuchoma au vidonge,au nikiamua nitafute ya kienyeji ndio nikapata kwa mmasai huyo alienda nichimbia nikainywea kwenye kahawa ila ilikuwa chungu balaa nimepona mpaka leo tatizo limeisha
Naweza kupata hiyo dawa nina mtu wangu wa karibu pia anasumbuliwa na hiyo kadhia
 
Ni minyoo wa kwenye ngozi mi nilisumbuliwa sana nikanywa dawa ya kienyeji ya wamasai nikapona mwanzoni nilihisi sabuni hola nikahisi maji hola nikahisi dodoki hola baadae jikamweleza dokta mmoja wa ngozi akaniambia kuna dawa ya sindano kuchoma au vidonge,au nikiamua nitafute ya kienyeji ndio nikapata kwa mmasai huyo alienda nichimbia nikainywea kwenye kahawa ila ilikuwa chungu balaa nimepona mpaka leo tatizo limeisha
Aisee umenifungua hii. Tunafanyaje hii kupata dawa?
 
Back
Top Bottom