Miujiza 40 ya mtume Muhammad (S.A.W)

Ungeendelea na 51 pia.
 
Hizo ni fix wanazopigana misikitini kuionyesha kuwa Quran kuwa ni bora wakati si kweli, Quran haijashushwa wala nini wala Muhammad hakupata wahyi wowote kutoka kwa Mungu ni ubunifu wa watu tu kama ambavyo kuna uongo mwingi kuhusu utume wake
 
WAO WALIULIZA KAMA BAAZI YA WATU WALIVYO ULIZA....MIUJIZA WALIFANYIWA KAMA IYO NA WAKAISHIA KUSEMA "SIJAPATA KUONA UCHAWI KAMA HUU"....KAFIRI KAFIRI TU
unadanganya watu unataka allah aonekane muongo? muhamadi hakupewa mujiza tafta msafu mzima yy ni muonyaji na mbashiri tu achana na hadith za kijinga hizo zinazo pingana na kweli ya quran sio kila nabii lazima awe na mujiza shekhe
 
unadanganya watu unataka allah aonekane muongo? muhamadi hakupewa mujiza tafta msafu mzima yy ni muonyaji na mbashiri tu achana na hadith za kijinga hizo zinazo pingana na kweli ya quran sio kila nabii lazima awe na mujiza shekhe
Quran tu yenyewe ni muujiza tosha...
 
sawa lakini hajaufanya yy bali kashushiwa tuu unafahamu mana ya kufanya muujiza?
13:38. Na hakika Sisi tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na tukajaalia wawe na wake na dhuriya. Na haiwi kwa Mtume kuleta miujiza isipo kuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila kipindi kina hukumu yake.
 
13:38. Na hakika Sisi tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na tukajaalia wawe na wake na dhuriya. Na haiwi kwa Mtume kuleta miujiza isipo kuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila kipindi kina hukumu yake.
leta haya sasa mtume kafanya mujiza kwa idhini ya allah?
 
Hizo ni fix wanazopigana misikitini kuionyesha kuwa Quran kuwa ni bora wakati si kweli, Quran haijashushwa wala nini wala Muhammad hakupata wahyi wowote kutoka kwa Mungu ni ubunifu wa watu tu kama ambavyo kuna uongo mwingi kuhusu utume wake

Unaelewa nini unapoambiwa "Qur'aan" imeshushwa ?

Kama Qur'aan haijashushwa ni upi ukweli kuhusu hilo ?

Naomba unipe mambo ya uongo matatu tu kuhusu utume wa Muhammad ?

Kadhalika,naomba uniambie huo ubunifu ulisukumwa na nini na kwanini na lini ?
 
Sijamaliza uzi. Lakini waislamu kwanini baadhi yenu huwa mna mawazo mgando ? Kuna sheikh nilimsikia anadai quran ilishushwa ila biblia imeandikwa na mtu .sasa najiuliza mbinguni kuna printer ?

Sasa hapo unafikiri tatizo ni la Sheikh au Tatizo ni lako ? Jibu sahihi ni kuwa, tatizo ni lako,kwa kuona unachokifikiri na kukariri kuwa ni sahihi,hapa ndipo unapo onekana umuhimu wa watu kusoma.

Mathalani tamko "Kitabu" humaanisha zaidi ya kitabu chenye "Cover" na kurasa. Mathalani Injili ni kitabu lakini hutakuta kitabu kama kitabu kwa asili yake chenye kurasa kikaitwa Injili na ndio aliyokuja nayi Yesu,bali kimeitwa kitabu kwa kurejewa kilicho andikwa katika "Ubao uliohifadhiwa". Hapa kuna maelezo mapana kidogo na ya kielimu,tosheka na huo mfano tu. Hapa nakusudia lugha iliyotumika si lugha uliyo izoea,mbinguni hakuna "Printer" ila Qur'aan imeshuka kwa kuwa mtume alikuwa anapewa wahyi kutoka kwa Allah aliye juu kupitia malaika muheshimiwa Jibril,hii ndio maana ya Qur'aan imeshushwa sio katika mtindo wa karatasi bali maneno.
 
leta haya sasa mtume kafanya mujiza kwa idhini ya allah?

21:5. Lakini wao walisema: Hizo ni ndoto za ovyo ovyo, bali amezizua tu, bali huyo ni mtunga mashairi. Basi atuletee miujiza kama walivyo tumwa wale wa mwanzo.6. Hawakuamini kabla yao watu wa mji tulio uangamiza. Basi, je, wataamini hawa?7. Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui.

Sio kila jambo limeelezwa ndani ya quran bali wanasimulia walioona na kusikia nazo ni hadidhi za mtume zinazosimuliwa na maswahaba waliokuwa pamoja nae zama za uhai wake

Kwaizo aya wale walikuwa wanadai muujiza walijibiwa na aya iyo n a zingine kwamba muujiza hata ukafanywa bado hawataamini kama wale watu wamiji....Ndugu Kiufupi ni kwamba sio kila jambo lazima zitoke kwenye Quran bali pia Suna(matendo/maneno na yaliyoshuhudiwa na mtume kisha akawa kimya) za mtume....Na usinifundishe dini yangu ila mimi nitakufundisha yangu sio eti nisiamini hadithi bali quran tu hahahahaaaa....Iko hivi nitakalolikosa ndani ya kuran nitalitafuta katika sunna za mtume(hadithi) na nikakosa basi maswahaba na wema waliotangulia....zaidi sana nitafuata aya ......Basi waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui.
 
leta haya sasa mtume kafanya mujiza kwa idhini ya allah?
17:1. SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.
Iyo misikiti miwili ni Al-Masjid Al-Haraam (saudia) mpaka Al-Masjid Al-Aqswaa (Jerusalem).
Haya ningekosa usingizi kama ningekosa kukujibu kwa ushahidi japo sio lazima kila kitu kiandikwe/kipatikane ndani ya quran.......Haya ndani ya usiku mmoja mtume katoka saudia hadi jerusalem.....tena kisa kinaendelea alipotoka yerusalem alienda mbinguni na huko akakutana na mengiiiiiiiii.....asubuhi kaamkia saudia alipolalia......Nashukuru kwa kunielewa zaidi juu ya muujiza huu soma hapa.......Usiku mwema
 
Good
 
ww hauelewi yan ukisoma andiko mfano mungu akampleka musa kushuhudia mti ukiwaka motoo na usiteketee utasema huo mujiza musa kaufanya yy? yan mujiza kufanywa na mtume au nabii inabidi yy ndio atekeleze huo mujiza mungu aidhinishe sasa mtume muhamad s.w ktk msaf mzima hajawai kutekeleza mujiza wowote na wapo wengi waliodhan kuwa mtume amekuja na mujiza lakini mungu aka fafanua ktk msafu kwamba mtume ni kwa ajili ya kuonya na kubashili tu nenda kasome shekhe
 
Hizo ni fix wanazopigana misikitini kuionyesha kuwa Quran kuwa ni bora wakati si kweli, Quran haijashushwa wala nini wala Muhammad hakupata wahyi wowote kutoka kwa Mungu ni ubunifu wa watu tu kama ambavyo kuna uongo mwingi kuhusu utume wake
17:88. Sema: Wangeli kusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur'ani basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao.
2:23. Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli.

Haya chalenge iyo mliyopewa na mwenyezi mungu hadi leo hamjaishinda na hamtaishinda kamwe......Ikiwa unahisi au unauhakika kwamba quran imetungwa na mwanadamu basi na wewe itunge,,,huenda ikakuwia vigumu basi waite ndugu na jamaa zako,pia ikawa ngumu basi waiteni na viumbe wengine msaidiane walau mpate kutunga aya inayofanana na quran.
 
labda na mimi nikuulize hao mitume wengine ushahidi yakwamba wao walifanya muujiza umeipata wapi
 
na nyongeza Quran ilishuka wakati mtume yupo sasa sijui ulitaka ilisimulije wakati watu wanaona wenyewe....yan eti aya ishuke jamani huo ni muujizaaaaaaaaaaaa...wakati watu waliona na kusimua.Ndugu naomba uelewe kwamba Quran haijakanusha kwamba mtume hajafanya muuja....Bali ilishangaa walioleta kisingizio cha kwamba sisi hatuamini hadi tuone muuja wakati mwenyez mungu anawajua watu tangu zama za adamu....Unataka majibu toka kwenye Quran basi haya ni majibu
2:37. Na wamesema: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuteremsha muujiza. Lakini wengi wao hawajui.
Ufafanuzi
Na makafiri washupavu wamesema: Tunataka ateremshiwe Muhammad dalili ya kuonekana kutoka kwa Mola wake Mlezi, itayo shuhudia ukweli wa huu wito wake! Waambie, ewe Nabii: Hakika Mwenyezi Mungu anaweza kuteremsha hiyo dalili muitakayo. Lakini wengi wao hawajui nini hikima ya Mwenyezi Mungu katika kuziteremsha Ishara. Na hayo hayafuati matamanio yao. Na lau kuwa Yeye akiwakubalia hilo walitakalo, na kisha wakakanusha baada yake, basi atawateketeza tu. Lakini wengi wao hawajui nini matokeo ya vitendo vyao!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…