Ndo shida ya viongozi kutoijua nchi yao vizuri. Nchi hii ina watu maskini ambao yebo yebo inakatika anaishona hadi inatoboka bado mtu anaivaa.Shibe ugonjwa mbaya sana. Kuna watu wakiambia Tanzania, akili zao zinaingiwa na picha ya kuanzia Mbagala, inaambaaambaa Posta Mpya, Kivukoni kutokea Kinondoni hadi Bunju, Madale hadi Msakuzi...yaani kwa kifupi hufikiri nje kidooogo ya upeo wa macho plus mji mkuu wa mkoa aliotoka. Mbaya zaidi hadi watunga sera na wasimamizi wanaamini hivyo hivyo.
Hivi, kuna mtu anauziwa nguo mbovu kwa lazima? Kinachoamua soko ni upatikanaji peke yake? Hivi wote ambao hatuvuti bangi tunakuwa hatuvuti kwa kuwa tu tumeshindwa kuipata?
Hivi viwanda vya nguo hapa Tanzania ni vipi? Ni hivi vinavyotengeneza vitenge na khanga?
Nafahamu uwepo wa Mtibwa Suger, Kilombero Sugar, Kagera Suger, TTC Moshi na bado kurupu ya sukari inatuumiza kiasi mamlaka zinajitoa fahamu kubadili bei elekezi angani. Leo hii tunakurupuka na nguo, tutavaa madera kwenda kazini?
Ndo shida ya viongozi kutoijua nchi yao vizuri. Nchi hii ina watu maskini ambao yebo yebo inakatika anaishona hadi inatoboka bado mtu anaivaa.
Mtu ananunua nguo ya elfu nne miezi sita inapita hajanunua nguo nyingine na ikichanika anatia kiraka.
Watu wa vijijini wanaishi kwa msimu. Msimu ukipita si ajabu mtu kupita wiki nzima haijui mia tano inafananaje. Duh! watu watatembea uchi.
hivi wewe tanzania kuna kiwanda cha nguo bwana acha kutujazia server kwa urojo wakoMleta uzi hayo maduka yote uliyotaja yanafanya kuzungusha mtumba wa ndani yani mtu anatoa nguo yake au kiatu ambacho hana matumizi nacho tena anapeleka goodwill. Huwezi agiza mtumba Indonesia ukapeleka kuuza USA.
Serikali inataka kuinua soko la bidhaa za ndani hasa nguo na viatu kama ilivyokuwa hapo awali.
Kila nchi Lazima ilinde soko lake la ndani ili kukuza uchumi wake.
Mleta uzi hayo maduka yote uliyotaja yanafanya kuzungusha mtumba wa ndani yani mtu anatoa nguo yake au kiatu ambacho hana matumizi nacho tena anapeleka goodwill. Huwezi agiza mtumba Indonesia ukapeleka kuuza USA.
Serikali inataka kuinua soko la bidhaa za ndani hasa nguo na viatu kama ilivyokuwa hapo awali.
Kila nchi Lazima ilinde soko lake la ndani ili kukuza uchumi wake.
Tofauti iko wapi? Si zote za ndani na za nje zimeshavaliwa? Huku hatuna za ndani kwa kuwa tunavaa hadi tunatia virakaKwa hiyo mitumba unayoongelea inaingia nchi hizo kutoka nchi za nje au ni wananchi wanazungusha humo humo nchini kwao?
Viwanda vipi? Matokeo yake tutakosa hata za kuvaa.Mpango Ni kufungia uagizwaji/uingizwaji wa mitumba nchini sio kwa wamachinga tu ili kuinua uvaaji wa nguo na viatu vya ndani.
Incredible hebu niweke bayana: na huko majuu kuna mitumba ya chupi, sidiria, soksi na taulo?