Mitumba ipo hata nchi zilizoendelea

Incredible

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,031
1,603
Katika nchi za Northern America yaani United States of America na Canada, kuna maduka makubwa ya kuuza mitumba.

Mfano

Value Villages
Goodwill
Salvation Army
Na mengineyo.

Katika maduka haya wazungu na watu wengine ununua nguo , viatu, furniture, vyombo kama sahani, vikombe, vijiko n.k

Value village kwa mfano, supplier wao mkubwa ni kampuni iitwayo Servers ambayo upata vitu kutoka Canada au Marekani.

Viwanda vipo lakini na mitumba ipo. Mitumba siyo Nguo tu, ni pamoja na vitu kama spare za magari, magari, vitabu, mafriji, n.k.

Miaka ya nyuma, Dr. Salim Ahmed Salim alitumia uzoefu wake wa kukaa nje kuwaelimisha viongozi wenzake serikalini kipindi akiwa waziri mkuu, kwamba mitumba ipo hats nchi zilizo endelea. Ilisaidia sana.

Kwasasa sijui utumuelimisha Nani? Maana ni vurugu.
 
Kwa hiyo mitumba unayoongelea inaingia nchi hizo kutoka nchi za nje au ni wananchi wanazungusha humo humo nchini kwao?
 
Kwa hiyo mitumba unayoongelea inaingia nchi hizo kutoka nchi za nje au ni wananchi wanazungusha humo humo nchini kwao?
ccm wamechanganyikiwa kwa hiyo hata zile mitumba za misaada kanisani au je ni mitumba kwa wauzaji au machinga na je kama ni hivyo kwanini serikali ya CCM hisizuie uwagizaji bali wanafunga kwa watembeza barabarani.huozo huo.

swissme
 
Mie sijawaelewa, labda watajieleza baadae.

Hao watembeza barabarani nao si wananunua mitumba hiyo kutoka kwa walioigiza...ila kuna siku nilikuta duka linamaburungutu ya mitumba wanauza nilishangaaa kuwa kumbe hii imekuwa biashara lazima waletaji watakuwa wengine wanaleta ambazo hazifai kuvaaa kwa sanabu moja au ingine... ila ndio hivyo.
 
ccm wamechanganyikiwa kwa hiyo hata zile mitumba za misaada kanisani au je ni mitumba kwa wauzaji au machinga na je kama ni hivyo kwanini serikali ya CCM hisizuie uwagizaji bali wanafunga kwa watembeza barabarani.huozo huo.

swissme
Mpango Ni kufungia uagizwaji/uingizwaji wa mitumba nchini sio kwa wamachinga tu ili kuinua uvaaji wa nguo na viatu vya ndani.
 
Mpango Ni kufungia uagizwaji/uingizwaji wa mitumba nchini sio kwa wamachinga tu ili kuinua uvaaji wa nguo na viatu vya ndani.

Swali je wamejipanga kuhakikisha viwanda vya ndani vina uwezo wa kuzalisha nguo za kutosha na bei ambazo watamudu watu???au ndo yaleyale ya sukari mwisho wa siku watu waanze kutembea uchi???
 
Mleta uzi hayo maduka yote uliyotaja yanafanya kuzungusha mtumba wa ndani yani mtu anatoa nguo yake au kiatu ambacho hana matumizi nacho tena anapeleka goodwill. Huwezi agiza mtumba Indonesia ukapeleka kuuza USA.

Serikali inataka kuinua soko la bidhaa za ndani hasa nguo na viatu kama ilivyokuwa hapo awali.

Kila nchi Lazima ilinde soko lake la ndani ili kukuza uchumi wake.
 
Natoa tahadhari tu..tusifanye vitu i.e serial I isifanye naamuzi kwa kuangalia nchi za Ulaya au life style ya viongozi ambapo hawavai mavazi ya Mitumbo kama asilimia 80 ya Watanzania waliobakia. Sidhani kama tumejiandaa kukabiliana na mahitaji ya mavazi ya wananchi wetu wote ambao ni masikini wenye uwezo Mdogo kununua dukani..lazima tutafakari hilo.
 
South Africa wana brand za viatu au nguo zaidi ya laki kadhaa na mall zipo za kutosha ni mwezi tuu wamefungua mall kubwa kuriko zoote SA hapa johannesburg lakini mitumba ipo wanderas street pale...wanatoa maamuzi kwa kuangalia Dar es salam tuu vijijini kama mtera huko nguo tuu za mtumba tuu ni hatari...
 
Inavyoonekana Waziri wetu ameshajisahau kabisa na hajui kwa nini mitumba iliruhusiwa kuingia na kunza nchini. Ukianza kuangalia viwanda vyenyewe vya nguo vinasusua na hata wakizalisha hizo nguo hiyo bei yake itakuchosha kabisa. Hivi anafikiri hatupendi kuvaa nguo spesho? Hivi anafikiri watu wanapenda kuvaa mitumba? Ugumu wa maisha na kipato kigogo ndivyo vinawafanya watz wavae mitumba.
 
Kwa hiyo mitumba unayoongelea inaingia nchi hizo kutoka nchi za nje au ni wananchi wanazungusha humo humo nchini kwao?
China ni watengenezaji wa nguo/vifaa kutokana na unafuu, ila ni nguo au vifaa vyenye majina ya kampuni ya Canada/Marekani. Na zinaishia katika maduka hayo(kama mitumba) mtu anapopata vifaa vipya, wenzetu wanabadilisha vifaa/nguo katika muda mfupi kutokana na maendeleo ya teknolojia, na pia kama njia ya kusaidia wenye mahitaji hayo na ila hawamudu bei za asili.
 
Mitumba ipo ya grade ya juu mpaka chini kabisa. Serikali ingezuia ile ya grade ya chini kabisa ili nchi yetu isiwe dampo la huo uchafu
 
Yale yale ya sukari, wanazuia mitumba wakti hawana kiwanda cha nguo za kututosha wote tukashaini.
Ni watz wangapi wanaweza kumudu pamba za duka?
 
Mitumba niliiona Copenhagen Denmark'free market pia Kuala lumpur malaysia,Uae huko kote mitumba kawaida...Haya yanayotokea hapa yatamuumiza sana mtu wa chini,sasa hivi sukari na mafuta ya taa ni adimu sasa tunaenda kwenye nguo!
 
China ni watengenezaji wa nguo/vifaa kutokana na unafuu, ila ni nguo au vifaa vyenye majina ya kampuni ya Canada/Marekani. Na zinaishia katika maduka hayo(kama mitumba) mtu anapopata vifaa vipya, wenzetu wanabadilisha vifaa/nguo katika muda mfupi kutokana na maendeleo ya teknolojia, na pia kama njia ya kusaidia wenye mahitaji hayo na ila hawamudu bei za asili.

Samahani sijakuelewa kizaidi ujumbe wako...nijuze
 
Back
Top Bottom