Mitsubish Pajero GDI IO 1.8 5 Doors

Mitsubish Pajero GDI IO 1.8 5 Doors

wanaoifahamu vyema hii gari nipeni mawazo na usahuri pia uzoefu wenu hasa kwa matumizi ya hapa Dar na kusafiri nayo mikoani je inafaa na matunzo yake ni vipi ili idumu? Naombeni ushauri na mawazo yenu kwani niko mbioni kuinunua Transmission ni Manual cc 1800 5Doors.

karibuni

Nakushauri usinunue kabisaaaaaaaaaaaaaa! Ni mtumiaji wa hii gari tangu 2007 but from this point nakujuza tu tafuta gari ingine kama rav 4 au nunua Suzuki grand vitara hizi!!! na nimeona sasa hivi zinauzwa bei rahisi but i am warning kama hujalipa hela badili mawazo! kutembea na ulaji wa mafuta hata safari ndefu zote ipo sawa wala haina shida ila kwa ushauri usiipende hii gari hata nukta
 
kwanza elewa kuwa
1. HAKUNA GARI ISIYOHARIBIKA DUNIANI KOTE, SPARE ZINAUZWA KILA KONA KARIBU MIJI YOTE!
2. NEW TECHNOLOGIES HAZIEPUKWI KWA KUOGOPA ETI UNASIKILIZA MAWAZO YA MTAANI
3. UKIWA MWEREVU LAZIMA UTUMIE MAFUNDI WANAOLEWA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA NA LAZIMA WATUMIE MANUALS
4.HUNA UWEZO WA KUWASHAWISHI MANUFACTURERS WAKUTENGENEZEE OLD TECHNOLOGIES KWASABABU YA UJINGA NA UMASKINI WAKO!!!!!!!!!!!!!!
5. D4, GDI NA ZINGINE ZIPO NA ZINATUMIKA KWENYE NEW CARS.....PAJERO, HILUX, PRADO AND SO ON
 
Mkuu, my honest opinion would be........dont buy that car.
hiyo gari inahitaji kuwa handled kama mtoto. proper service, mafuta masafi (kitu ambacho huku kwetu ni ndoto) na fundi anayeijua sawasawa.

ikianza kuleta issues za low compression na slow accellaration unaweza ukachanganyikiwa. then white smoke na miss....balaa.
lakini kwa fundi anayeifahamu anajua problem ilipo.

If you want a low maintenance 4WD vehicle, go for Rav4 old model....perfect. sio hizi zenye engine za D-4...vimeo hivyo.

Mkuu Bigirita hiyo niisemayo engine yake ni 4G93 is it the same with the one you said to be D-4? naomba kueleweshwa hapo tafadhali
 
Last edited by a moderator:

Mkuu, hizi engine za Mitsubishi 4g93 sio sawa na D-4 engines.

Tatizo la 4g93 ni throttle sensor, ikibuma hiyo au ikichokonolewa vibaya na mafundi njaa itakusumbua balaa. nafikiri bei yake ni kama 400 USD kwa original Mitsubishi parts, as far as i know hiyo ndio headache kubwa especially ikianza kusumbua.

Lakini mambo mengine yanayosumbua ni idle control valve na plugs/plug wire. lazima uweke original parts mwanangu. ukiweka janja janja utakuwa rafiki wa mafundi kila siku.

Otherwise, ulaji wa mafuta ni gari nzuri sana..........unfortunately a car is more than fuel consumption, if it was then kila mtu angenunua baiskelit.
 
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi wako nimekuelewa vema. Ubarikiwe
 
Nakushauri usinunue kabisaaaaaaaaaaaaaa! Ni mtumiaji wa hii gari tangu 2007 but from this point nakujuza tu tafuta gari ingine kama rav 4 au nunua Suzuki grand vitara hizi!!! na nimeona sasa hivi zinauzwa bei rahisi but i am warning kama hujalipa hela badili mawazo! kutembea na ulaji wa mafuta hata safari ndefu zote ipo sawa wala haina shida ila kwa ushauri usiipende hii gari hata nukta

come on the table mkuu kwa nini unasema hivyo?
 
Mkuu, hizi engine za Mitsubishi 4g93 sio sawa na D-4 engines.

Tatizo la 4g93 ni throttle sensor, ikibuma hiyo au ikichokonolewa vibaya na mafundi njaa itakusumbua balaa. nafikiri bei yake ni kama 400 USD kwa original Mitsubishi parts, as far as i know hiyo ndio headache kubwa especially ikianza kusumbua.

Lakini mambo mengine yanayosumbua ni idle control valve na plugs/plug wire. lazima uweke original parts mwanangu. ukiweka janja janja utakuwa rafiki wa mafundi kila siku.

Otherwise, ulaji wa mafuta ni gari nzuri sana..........unfortunately a car is more than fuel consumption, if it was then kila mtu angenunua baiskelit.

mkuu Bigirita samahani tena kwa swali langu vp kuhusu 4G94 Engines? je zina unafuu compared to 4G93 engines? nina option ya kuchagua between the two of them
 
Last edited by a moderator:
Tafadhali usipate shida gdi zinatengenezeka vizuri sana na spare zake zipo bila matatizo.tuko tabata round about kuelekea st marry mwanzoni round about kulia gate la jekundu.tunatumia scan tool kwa diagnosis.mawasiliano yangu .0755399613,0715399613.tunaweka spare sahihi za gari.pia angalizo gari hizo zinatakiwa kiwango cha mafuta kwenye tank ni nusu tank.sumu kubwa gari hizo ni kutembelea taa ya mafuta inawaka kosa sana.natumaini mtaipenda ushauri wangu.gharish john.dar es salaam
 
Habari za sikuu nyingi wanajamii ,nimekuwa kimya muda mrefu sana,napenda kutoa shukrani zangu zote ziwafikie wanajamii kwa kupokea ushauri wangu pale walipo uliza kuhusu matatizo ya gari aina ya mitsubishi pajero io or GDI,
Tunaendelea kutengeneza gari hizo bila tatizo,na gari aina zingine kwa ufasaha mkubwa,gaurage automotive star services,
 
Magari yanayoogopwa ndio mazuri kuwa nayo.
Mi ninayo sasa miaka 2 hakuna shida yoyote zaidi ya service tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom