Wamiliki wa Mitsubish Pajero IO, GDI Tukutane Hapa

Natania

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
262
217
Wakuu heshima kwenu.

Mimi ni mmoja kati ya wamiliki wa Pajero IO, GDI. Kwa ujumla ni gari zuri ila linachangamoto zake ambazo nyingi nadhani zinatokana na mafundi wetu mtaani kutokuijua vizuri gari na wanaishia kusema hayafai (nimewasikia wengi). Sasa ebu tupeane maujuzi hapa, kuanzia kwenye mafundi ambao wanaiwezea vizuri GDI, maduka ya spare na uzoefu mwingine (nasikia kuna wengine wanabadilisha injini na kuweka ya Noah). Lengo la uzi ni kujua matatizo ya GDI na Namna ya kuyatatua.

Toa uzoefu wako (bila kujali upo mkoani ama jijini Dar.

cp5723813158781326804.jpg
 
Injini used ya GDI naiweza kuipata wapi na kwa kiasi gani?
 
Hazina matatizo yoyote ziko vizuri sana,labda ungetuwekea hapa hizo changamoto
 
Nenda Shaurimoyo Ilala kwenye maduka wanayouza spare za magari utapata,ila sijui bei itakuwa kiasi gani.
Asante sana mkuu kwa kunishtua, nipo mkoani kwa sasa ila nikishuka jijini nitawatembelea
 
Kwa sasa zitakuwa $3000 mpaka 3500 CIF from japan na inaletwa mpka dar.
Hbb
Spea za GDI zipo nyingi nenda mtaa wa songea ILALA tembea humo ulizia mpaka ukutane mtaa wa iringa. Pia shauri moyo wanauza spea.
 
Mkuu, hiyo ILALA uliyoitaja ndiyo hiyohiyo iliyo karibu na Gerezani (Kituo cha Mwendokasi)? Shauri Moyo ni wapi huko mkuu?
 
Yes baada ya gerezani na kituo cha mwendo kasi barabara inayofuata ni shaurimoyo na hapo ulizia spea za gdi kuna maduka ya mitsubishi. Pia kama una smartfone ingia googlemap utafute Songea mosque dar es salaam itakuonesha
 
Asante mkuu, hata sikujua kama Dar ipo vema namna hii kwenye google maps. Thank you a million.

Screen Shot 2017-02-10 at 14.37.57.png
 
Engine za GDI zinatengeneza uchafu sana aina ya carbon kwenye engine. Na hii ikizidi engine inakosa power, gari kuwa na miss na kuzima zima na baadae inaweza engine inaweza kuharibika kabisa.

Chukua tahadhari: mwenye GDI iliyofika mileage 100000km au zaidi, nunua dawa "complete fuel system cleaner" na umwagilie kwenye tenki lako la petroli halafu jaza mafuta (FUATA MAELEKEZO YALIYOKO KWENYE CHUPA YA DAWA HIYO".
Ukirudia kufanya hivi kama marambili kwa kila kabla ya oil service (yaani 5000km) sio mbaya.
Dawa utazipata kwenye maduka ya oil za gari kama lumumba na livingstone.

Angalizo:natoa ujuzi tu na siko kwa ajili ya matangazo ya kibiashara
 
Asante kwa shule mkuu! Sikujua kinachosumbua kwenye engine ni carbon ila kwa habari ya gari kukosa nguvu hiyo ipo sana. Vipi ushauri wa wengine wanaosema ni heri kuitoa engine ya GDI na kuweka engine ya Toyota? Ama kwa kutumia hiyo "complete fuel system cleaner'' engine ya DGI inaweza kutengamaa vizuri?
 
Tanzania kuna kasumba ya kuogopesha watu kuhusu magari zaidi ya toyota. Gari yoyote ile inahitaji mkono wa mtu mmoja na service kama manual za gari zinavyoeleza. Fuel system cleaner ni mojawapo ya service ya gari. Sishauri kubadilisha engine ikiwa gari bado ipo vizuri. Na kesho naenda nayo dodoma na kugeuza.
 
Gari ndogo za kutembelea toka kwa kampuni ya Mitsubishi ni chache hivyo kunachangamoto ya spea na mafundi tofauti na Toyota
 
Tanzania kuna kasumba ya kuogopesha watu kuhusu magari zaidi ya toyota. Gari yoyote ile inahitaji mkono wa mtu mmoja na service kama manual za gari zinavyoeleza. Fuel system cleaner ni mojawapo ya service ya gari. Sishauri kubadilisha engine ikiwa gari bado ipo vizuri. Na kesho naenda nayo dodoma na kugeuza.

Kila la kheri mkuu na safari. Kama huta-mind naomba utupie kapicha ka hiyo -complete fuel system cleaner ambayo umeshaitumia na kufanya kazi, lakini ukitaja duka ambako inapatikana kwa Dar utakuwa umetusaidia sana.
 
Back
Top Bottom