kunatetesi zimezagaa mitaani,juu ya upunguzwaji wa mb za [internet] katika mitandao ya simu, inasemekana mamlaka ya mawasiliano tanzania [tcra] imeyaagiza makampuni ya simu nchini,kupunguza megabite za vifurushi,vya internet ili kudhibiti utumiaji mbaya wa mitandao,
wanadai watanzania wanatumia mitandao vibaya,sasa mimi najiuliza kwamba zile sera za kupandisha bei ya mafuta ya taa ili kudhibiti uchakachuaji wa petrol ndio sera hizo hizo zimeletwa huku?
lakini mimi nafikiria kwa jicho la mbali kidogo haya yanakuja sio kwa baati mbaya ni kutokana na mambo ya nalo likabili taifa kwa sasa na ili kuwafanya watanzania wasiweze kujua mambo yafuatayo.
1: uandikishwaji wa daftari la mpiga kura
2: upingwaji wa kura ya ndio au hapana katiba pendekezwa
3: uchaguzi mkuu mwezi octoba
kutokana na vyombo vya habari hapa nchini kutokuwa huru na hawa jamaa wanaona kwamba kupitia mitandao ya internet watu wataelimishana njia ni kupunguza mb ili kuwanyima watu wengi fursa ya kujua mambo.
nakumbuka kule misri wakati wa vuguvugu la kuungoa utawala wa hosni mubarrakha serikali ili zima kabisa mawasiliano ya internet ili kuzuia taarifa kuzagaa.hizi zote ni kujilisha upepo,serikali iache kama ni kweli uhu mchezo.
huku ni kuwanjima uhuru wananchi kutoa maoni yao,serikali ishugulike na matatizo ya wananchi nasio kufanya hila badala ya kutibu itazidisha hasira kwa wananchi maana taarifa hizi zimezagaa sana mitaani:
kama ni kweli [tcra] imetumika ni vyema ikajua wajibu wake kuliko kutumiwa na kikundi cha watu wa chache kwa maslahi yao,