Mitandao ya simu: Kuna nini nyuma ya pazia?

Mitandao ya simu: Kuna nini nyuma ya pazia?

Wakuu hii ni zaidi ya wizi. Mimi nina laini mbili za simu, Zantel na tigo.

Kiufupi mimi laini ya Zantel huwa ndio natumia kwa internet, whatsapp na kadhalika kutokana na vifurushi vyake kuwa bomba, na laini ya tigo ni smartphone lakini zile za kizamani zenye qwerty keyboard, ambayo mm hujiunga kifurushi cha Tsh.649 kwa ajili ya kupiga tu na sifungui kabisa internet.

Cha ajabu huwa natumiwa msg na tigo mara unaambiwa umebakiwa na MB 5, mara MB 2 na mimi sifungui kabisa internet. Sasa huwa najiuliza nani katumia hizo MB? ina maana wenzangu mnaotumia INTERNET mnaibiwa jamani amkeni!!!!
 
Wakuu hii ni zaidi ya wizi. Mimi nina laini mbili za simu, Zantel na tigo.

Kiufupi mimi laini ya Zantel huwa ndio natumia kwa internet, whatsapp na kadhalika kutokana na vifurushi vyake kuwa bomba, na laini ya tigo ni smartphone lakini zile za kizamani zenye qwerty keyboard, ambayo mm hujiunga kifurushi cha Tsh.649 kwa ajili ya kupiga tu na sifungui kabisa internet.

Cha ajabu huwa natumiwa msg na tigo mara unaambiwa umebakiwa na MB 5, mara MB 2 na mimi sifungui kabisa internet. Sasa huwa najiuliza nani katumia hizo MB? ina maana wenzangu mnaotumia INTERNET mnaibiwa jamani amkeni!!!!

Si afadhali wewe? Mie nilijiunga kwa bundle ya shilingi 999 jana leo nimeambiwa zimeisha sawa silalamiki kwa vile nilipiga simu je sms nazo zimefia ndani? Wizi mwingine mbaya jamani!
 
Unanunua muda wa hewani, halafu ukitaka kujiunga na cheka inashindikana. Wakati huohuo ukiwa na tsh 500 na hujajiunga na cheka unatuma sms 3 au 4 tu au unaongea dakika moja na sekunde kadhaa salio kwisha. Mbona mnatugeuza watz watumwa/mishikaki ndani ya ardhi yetu. Kufurushi cha tsh 500 ukijiunga cheka unapata MB 8 tu. Jamani MB 8 zinasaidia nini? Bei za vifurushi zinabadilika badilika kama kinyonga kila baadaya muda fulani. kifafa sana.
 
Katika hali isiyo ya kawaida Kampuni ya mtandao wa simu ya Vodacom-Tanzania imebadilisha ghafla gharama za vifurushi kwa wateja wake huku wengi wakiwa ni watu wa hali ya chini,kwa kupunguza muda wa maongezi(dakika) pamoja na MB kwa ajili ya internet kiasi cha kuanza kuwakatisha watumiaji tamaa kuendelea kutumia mtandao huo na kupanga kuamia mitandao mingine kama TIGO na AIRTEL ambayo huduma zake ni nafuu ukilinganisha na Vodacom.
 
Huu mtandao ni bure kabisa! Customer service is poor, wanafanya daylight robbery, yet wameshrink MBs na mida ya maongezi, stupidly wanatuongezea texts! Nimeshahamia Airtel thaaaank you!!
 
Imekula kwao wengi tumeshahama. Wangechagiza mahesabu ili waongeze gharama kwa awamu. Na hata hivyo faida wanayopata ni kubwa sana sijui hayo matumizi au kodi ya ghafla imetoka wapi. Labda hawataki tupashane habari maana ndio nji iliyopo ya kuelimishana hasa wakati huu wa uchaguzi!
 
Mimi mwenyewe nshahama. Unajiunga mfano university promotion unaambiwa upo nje ya eneo la chuo.
Sasa sijui hadi uingie ifisi ya VC ndo eneo la chuo. MB 8 na wanakujibu kwa nyodo.
Ila walishasema kazi ni kwako
So nimeamia tigoooooo. 350 una MB 300!
Vodacom kaxi sasa ni kwenu
 
Vodacom ni kifafa kwa wateja wao hasa wenye kipato duni. Dawa ni moja tu KUACHANA NAO
 
hahaha mb 8 za nini sasa....alafu tulishasema mitandao ni mingi kwa nini uing'ang'anie mitandao inayokuibia?
Kasya,
Poa mkuu. Mie nilikuwa natumia Airtel toka enzi za Celtel lakini wakanizuia kupokea miito na ujumbe tokea 2011 japo nililalamika TCRA lakini hakuna kitu. Nilichofanya ni kutumia TTCL tu basi.
 
wanataka kufanya kama Tanesco walivyo tubambika bei kubwa ya umeme na makampuni ya simu yanapita njia ilele sisi watanganyika tukoje mbona tumekaa kimya bila kuchukua hatua.
 
Yana jiandaa kutoa sadaka kusaidia chama fulani kwenye kampeni za uchaguzi mkuu na kura ya maoni kuhusu katiba.
Because otherwise there is no justification on it.
Tigo said expansion...i dont about voda.
Sasa kama sisi tunalipia moja kwamoja expansionzao kwa nini wasitupataie share??
 
Sijui inakuwaje serikali ipo kimya na wizi huu wa mitandao mb zinawahi kwisha nahisi kuna mchezo mchafu unafanyika mana mwanzo mb 500 nilikuwa siwez kuzimaliza kwa kuperuzi habari tu bila kudownload vitu saiv hali imekuwa mbaya hata kuperuzi zinaliwa kwa kas ya ajabu jamani tuhurumiane hasa tigo nnaotumia.
 
Yani hao airtel dakika mbili tu Mb 300 chaliii...Duh
 
Aisee kunasiku nimejiunga kama kawa nikawa natumia dakika tu za maongezi ile zimekwisha niangalie zimebaki ngapi nakuta Mb zimekwisha pasipo kuzitumia yaani Hii mitandao inatuumiza kweli
 
Back
Top Bottom