Mitandao ya simu: Kuna nini nyuma ya pazia?

Mitandao ya simu: Kuna nini nyuma ya pazia?

Tunakoelekea sasa ni zaidi ya ubeberu! Mtandao niliokuwa nautegemea sasa na wao wameamua kupunguza vifurushi vyao.

Awali, kifurushi;

- Tshs 399 dk 5+ 50sms na mb 15
- Tsh 499 unapata dk 10 sms 300 na mb 75
- Tsh 599 dk 15+ 350sms mb 100
- Tsh 649 dk 17+ 450sms na mb 125
- Tsh 999 dk 25 +1000sms na mb 150

Sasa hivi;

- Kifurushi cha 399 hakipo,
- Tsh 499 unapata dk 9 sms 300 mb 10
- Tsh 699 dk 24 +1000sms na mb 10
- Tsh 999 dk 24+1000sms na mb 10

Tunakoelekea hii nchi sio sasa!
 
mkuu hapo umenena vyema, hapo kuna aina ya wizi huwa unafanyika! kwanini warundike dakika, sms na bundle pamoja!?

Na kwa nini wanipangie muda wa matumizi? na zikibaki zinaenda wapi?? Wizi nje nje
 
Mtandao pekee ambao una haki ya kuulalamikia ni TTCL Hiyo mingine Biashara Huria. Hata wakikushushia ni kwa sababu za kibiashara.
 
Yaani hiyo management ya voda na komitii ya marketing imeshindwa kazi,,,, mi nahama leo jana niliweka jero nikashindwa kujiunga cox mi napenda net sana nikaona nimebanwa sana, mb8 hata haifungui 3G Cm yangu, basi nikaishia kupiga bila cheka,
LEO NAHAMIA AIRTEL

VODA NI WEZI, kesho kutwa mtawaona wamebadili wakati washatuibia!

AIRTEL NASIKIA MTANDAO MZURI SANA HAWAYUMBI YUMBI WAKO MAKINI NA MAMBO YAO.
 
Angalau watu watapunguza kelele hapa JF.
Hii itaweka heshima mjini whatsapp itapungua kabisa.
 
mwanga lutila

•148*88#
chagua kifurushi unachotaka kwa sh 800 unapata 1.2 GB
ambayo ni nzuri saaaaaaaana kuliko
unayolalamikia
 
Last edited by a moderator:
Duh kwa mtindo huu,sasa itatubidi tuwe online work hours,mana kuna internet free. Hii ya kutegemea bundle za mitandao ya simu itatufirisi kwa kweli..
 
Naona wameamua kutenganisha ya gharama ya internet na muda WA maongezi, kwa tigo kifurushi cha internet 1000 unapata 900mb wakati muda WA maongezi unapata dakika 21 kwa 999
 
sawa lakin airtl kiujumla wako vema kuliko wengne. Voda ni wezi toka zaman tanzania hii na kama si ma mpesa washakosa watu mda
 
Msijali uchaguzi mkuu wa Octoba ukipita hali itarudi kama ilivyokuwa awali.
 
Wakati nikitafakari ni vipi nijinasue na wizi wa mtandao wa vodacom kwa kubadilisha vifurushi vyao vya cheka, nikasema ngoja nijaribu Tigo. Huko nako ni wizi uleule ambapo sh.499 unapata dk 15 sms 250 na mb 8 tu!

Ndugu zanguni hii mitandao sielewi kama inataka kuturudisha nyuma. Na sielewi kwa nini wanatubania sana vifurushi vya internet? Kweli mb 8 zinatosha nini jaman?

Mtujuzeni jaman mlioko huko airtel huduma zao zikoje huko?
 
tigo wameshusha mb vibaya mnoo. hata kifurushi cha mini kabang 999 unapewa mb 8...
internet megabox day sh.999 unapewa 700 mb badala ya 900mb..
nahamia zantel leo huu ufalasi sasa
 
Airtel nao wameshashusha wqo wamefanya 10mb hili ni pigo kwa watumiaji wa smartphone.
 
Back
Top Bottom