Labda kwa kuwa huyu mwanaasha kasoma hapa tanzania....khalfan, khalifa, Rashid(chodo) na ali..wako nje ya bongo wanapiga kitabu...Mkuu, Mhariri kampongeza eti anasomesha watoto hapa nchini...hapo tuna jiuliza umakini wa mhariri..
Tatizo ni baraza la mitihani na wizara ya elimu. Kama siyo wao hii mitandao ingepata wapi hayo matokeo. Huu ujinga wa kuanika majina ya watoto hadharani ukomeshwe. Matokeo ya mitihani ni private matter. Wanachofanya baraza/wizara ni kama vile upime afya halafu matokeo ya lab yatolewe hadharani. Sioni sababu ya Tz daima kulaumu mitandao
Kwa muda mrefu mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kumchafua Rais JAKAYA KIKWETE kwa mambo ambayo hayahusiani kabisa na majukumu yake ya kuongoza serikali.
Yapo mambo mengi ambayo watu kupitia mitandao wamekuwa wakimchafua Rais na hapa nitatoa michango michache tu:-
1) Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ya mtoto wake aitwaye MWANAASHA KIKWETE yametumika sana kumchafua JK.
2) Thread iliyoletwa hapa JF na kichwa cha habari "Maswali mia moja kwa Rais KIKWETE" yakiwemo yaliyohoji ana wake wangapi na mengine mengi yalioonekana ni ya kumchafua Rais zaidi na hayakuwa ya kiutendaji.
Yapo mengine mengi ambayo kiukweli hata kurudia kuyaandika hapa hayafai.
Katika gazeti la Tanzania Daima la leo tarehe 15/02/2012 katika ukurasa wake wa Tahariri (The Editorial page) mhariri ameandika kuhusu hili kwa kichwa cha habari "Mitandao isitumike kumchafua Rais". Amebainisha kwa uwazi na kuonya wanaomiliki mitandao hiyo wawe wanahariri na habari zinazotumwa kabla ya kuziandika katika mitandao yao.
Refference: Tanzania Daima la tarehe 15.02.2012
Kwa bahati mbaya sana, matokeo ya mtoto huyo hayakuwa mazuri licha ya shule yake kufanya vizuri kitaifa katika mitihani hiyo na kuwa moja ya shule kumi bora
wanamchafua au wanasema ukweli?
pole ila nafikiri magazeti au media inaripoti yale ambayo yameshatokea na hata kama hayataandikwa bado hayatafutika....yatajulikana tu...big figures ni target za media and somehow that is the prize they have to pay for being "big." It happens everywhere sio Tanzania tu......
Binafsi naona wao tanzania daima ndo wame mchafua kabisa
maana idadi ya watu wanao ingina mtandaoni ni chache kuliko wale wanao soma magazeti.
Kwa kuiweka habari hii gazetini ni sawa na ku-broadcast kwa ulimwengu kwamba
jamani kuna hili na hili,kama mnataka kujua kwa undani zaidi nendeni kwenye mitandao.
Tanzania daima wana tumia petroli kuzima moto,...wame kosea.
Ni kazi ya chama cha maandamano. Jk ni adui yao namba 1.
Huyu mtoto angepata div1 ya point saba nina uhakika kingeandaliwa kipindi maalumu kwa ajli yake ili awasihi wanafunzi wengine namna alivyokuwa anasoma ili na wao wafaulu.....lakini kwa kuwa amefeli na kupata four ya point 27 watu wakiuliza imekuwaje mtoto mwenye kila kitu nyumbani akapata daraja hilo wanaonekana ni wachochezi....tena ilifaa waandishi wamfate huyo mtoto na wamuulze imekuwaje akapata hivyo....nini kilipungua?
Lakini ukweli utabaki pale pale juu ya mwanaasha......huyu mtoto alikuwa mzito na wazazi wake hawakujua mapungufu yake toka alipotimuliwa kifungiro baada ya kushindwa kufikisha wastani na wakamuhamishia hapo Feza.... Wazazi walishindwa kujua kuwa binti ni mzito wa kuelewa na walikuwa hawafuatilii maendeleo yake ya shule...kama wote mjuavyo wazazi wa huyu binti wanashinda angani na kwenye bembea na wakirudi nyumbani badala ya kufatilia maendelea ya mtoto wao wao...wenyewe wazazi wanamchukua mtoto na kumpeleka kwenye shows kama inavyoonekana hapa chini...
Sasa hivi mama Salma na Kikwete waongeze nguvu na ufatiliaa kwa watoto wao wengine..kuna huyo mmoja anaitwa Ali nae ni mzito wa kuelewa tena sana.....kwa kuwa wako Botswana najua matokeo yao hayataonekana kama ya huyu Mwanaasha...ila ukweli utabaki kusemwa kuwa juu ya Mwanaasha, ni uzembe wake na uzembe wa wazazi wake...
Siku zote huwa nasema hivi:
Anayepata div one na anaepata div.iv wote msuli wao uko sawa ila in opposite direction.....wakati huyu anakomaa kupata div one huyu mwingine nae yuko bize na shows kama hizi :
Ni kweli kabisa hata mimi namwunga mkono Mhariri ingawa mimi si CCM na wala sifurahishwi na utendaji wa Rais wetu. Uhuru wa mmoja huishia uhuru wa mwezie unapoanzia, kwa kweli mimi nachukia "Personal attacks" ziwe kwa JK au yeyote. Lakini hapa ni lazima ieleweke kwamba kusema jambo fulani ni baya, linatuumiza, linakera, au linatuhujumu si dhambi hata kidogo, na kwa taasisi ya urais hilo ni sawa kabisa ila kuzungumzia juu ya mambo yake binafsi na familia (nje ya kujihusisha kwao na siasa za nchi) si ustaarabu hata kidogo.
mwandishi yuko sahihi wengi tulitumia tukio hilo kisiasa badala ya ukweli.
Kwa matokeo ya mwanao unaona wanamchafua sana.Je nahapa utasemaje mkuu??? https://www.facebook.com/photo.php?...66006044.14156.100002518337070&type=1&theater
FEZA ni shule ya Private; ningemuona ni mzalendo kweli kama angelimpeleka katika shule za KATA zilizotapakaa kila kata. na ambazo anazisimamia MKULU AU HATA SHULE YA MSINGI ALIFELI HIVYO HAKUCHAGULIWA HATA KWENDA SHULE YA KATA??
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Mimi nadhani watoto wake ndio wanamchafua JK, mfano hili la Ridhiwani kudaiwa HESLB ni kashfa kwa Rais, kweli ameshindwa Ridhiwani ameshindwa kulipa bodi ya mikopo!? au ndio mambo ya kimjini mjini!! Sasa jamaa wakimshtaki maana kwa sheria ya HESLB wana nguvu hiyo watasema Rais anadhalilishwa!? Riz kafanya kazi IMMA Advocates na salary ni nzuri kiasi angeamua wamkate hata laki moja tu kwa mwezi saa hizi angemaliza huo mkopo!!
hapakuepo na sababu ya kushupalia kiushabiki huo mjadala,mimi nadhani tujifunze kwa wenzetu wa nchi zilizoendelea kwamba maisha binafsi ya familia za viongozi wao na hasa watoto wanachukua tahadhari kubwa. kama huyo mtoto angekuwa amefanya mambo yasiyofaa ktk jamii angejadiliwa kwa kiwango kile lakini kufeli mtihani siyo dhambi ama kosa,hata watoto wetu na wadogo zetu wanafeli,na baadhi yetu humu kwa nyakati fulani tulifeli.