HORSE POWER
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 2,077
- 1,392
Safi! Serikali ichukue mitambo hiyo haraka tunusurike na huyo mumiani.
Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
lesseni ndo ime ishaaa na sio mkatabaMkataba umeisha, wanatupelekaje mahakamani??
MUNGU MKUBWA NA IZIMWE ILI TUWEZE KUWEKA MKATABA MPYA NA WENYE MITAMBO HIYO? NA WATUMIE GESI NA BEI ISHUKE TENA CHINI YA WENZAO MAANA UNUNUZI WA MITAMBO TULISHALIPIA TAYARI SASA WAKO KWENYE FAIDA TU.
mkuu, uki-google utapata details lakini nadhani ya kwanza inajihusisha na biashara ya umeme na hiyo ya pili mambo ya "gesi ya Mtwara".Nombeni kujilishwa kama hizi ni Kampuni Mbili tofauti.
1. PAN AFRICA POWER
2. PAN AFRICA ENERGY
Endapo hawatapewa leseni nini kitatokea??
Mkataba wao na Tanesco utakuwa mashakani kuvunjika.Endapo hawatapewa leseni nini kitatokea??
gesi si ipo?Kwa hiyo mgawo (wa umeme) unarudi au vipi?
Sent from my Kimulimuli
ndio maana nimekwambia yy alijitahidi kwenye kulipa wafanyakazi hayo makosa mengine ni yake mbona mafisadi wengine wanakimbiza pesa tu nje hata duka hafungui bongoNi hela zenu hivyo anajua anatoa 0.5 tu ya pato lake.!
Hata dhahabu ipo, ila wanakomba mpaka ukoko.gesi si ipo?
Mgawo mkali unakuwaje na usiokuwa mkali unakuwaje?Migao mikali ilikuwa inasababishwa na ukame na wapiga dili wenye plants binafsi za kuzaliwa Umeme(hawa wako wengi sana, japo iptl ndo maarufu). Kumekuwa na mvua za kutosha na kinyerezi imejengwa plant nyingine, hivyo hata kama kutakuwa na mgao basi utakuwa ule tuliouzoea.
Ikumbukwe iptl ilikuwa inatumika kunapokuwa na mahitaji makubwa, mfano jioni au wakati wa sikukuu.
waswshili wanasema ukimchunguza kuku utumbo huwezi kumla..mi nasema ukiichunguza iptl utumbo waweza zimia..Ni wingu zito. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya maombi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kukwama, huku wakilazimika kuzima rasmi mitambo yao ya uzalishaji umeme.
Hatua hiyo imekuja baada ya kukwama kwa maombi ya kuongezewa muda wa miezi 55 ya leseni yake ya uzalishaji umeme kutokana na kusubiri uamuzi wa Ikulu.
Hali hiyo inajitokeza wakati mmiliki wa Kampuni ya Pan Africa Power (PAP) Harbinder Singh Sethi na Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering, James Rugemalira wakiwa tayari wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uhujumu uchumi, kutakatisha fedha na kusababisha hasara Serikali.
Hali za uhakika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema mitambo hiyo kwa sasa haizalishi umeme.
MTANZANIA lilitembelea mitambo hiyo iliyoko Tegeta na kukuta wafanyakazi wachache ambao walikiri mitambo hiyo kutofanya kazi.
"Mitambo ilizimwa tangu siku ile walipomkamata Sethi", alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake gazetini.
Pamoja na hatua hiyo inaelezwa kuwa kuna hatari ya kuitaifishwa kwa mitambo hiyo hasa baada ya Serikali kuweka ngumu katika utoaji wa leseni mpya ya biashara ya kuzalisha umeme kwa kampuni hiyo.
Licha ya hali hiyo leseni ya kampuni hiyo ilimalizika muda wake Julai 15, mwaka huu ambapo hadi sasa uamuzi wa kuitaifisha mitambo hiyo kurudi kuwa mali ya TANESCO ama laa ukisubiri uamuzi wa Ikulu.
Kwa sababu hiyo, kama Serikali itaendelea na msimamo wake dhidi ya IPTL ndiyo utakuwa mwisho wa miaka 23 ya IPTL.
Kampuni hiyo au IPTL iliingia nchini tangu mwaka 1994 na kila mwezi imekuwa ikilipwa Sh. bilioni 5.943 na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ikiwa ni gharama za uwekezaji mbali na gharama za umeme inaoliuzia shirika hilo.
Novemba 2014, baada ya Bunge kujadili Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ilitoa maazimio manane ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuichukua mitambo ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO.
Siku chache baada ya Bunge kupitisha uamuzi huo ambao ulifanyiwa kazi kwa haraka kwa Profesa Sospeter Muhongo kujiuzulu nafasi yake.
As usual Mkuu Chige at your own best! Asante kwa darasa! Je haiwezekani kukubaliana viwango wa tofauti vya capacity charge kulingana na mahitaji yetu ya nishati?Ngoja niweke blah blah pembeni na kujifanya mzalendo linapokuja suala la Capacity Charge under normal condition. I am talking from business point of view na sio from (fake) nationalism point of view.
Hapa kuna mambo mawili... Power Purchase Agreement (PPA) na Leseni ya Uuzaji umeme!!!
PPA ni makubaliano kati ya serikali na IPTL kuuziana umeme pale kunapokuwa na hayo mahitaji! Mkataba huu ilikuwa ni IPTL kutuuzia umeme pale tu tunapokuwa na mahitaji ya ziada ya umeme... hususani pale tunapokuwa na upungufu wa uzalishaji umeme kutoka vyanzo vingine, hususan vyanzo vya maji!
Kwavile mkataba haukuwa kununua umeme wa IPTL wakati wote, hapo Capacity Charge haikwepeki hata kama ingekuwa ni wakati wa Nyerere! Hii ni kwa sababu, endapo mabwawa yetu yanakuwa na maji mwaka mzima, ina maana mitambo ya IPTL nayo ingezimwa mwaka mzima! Kama tusingekuwa na uhaba kwa miaka 5, ina maana mitambo ya IPTL nayo ingezimwa kwa miaka 5!!!!
Sasa sijui ni Mwekezaji gani angekubali aje kuwekeza mitambo kisha iwe inakaa hata mwaka mzima na zaidi bila kuingiza hata senti tano wakati kuna cost of wear and tear!!!
Hivyo kabla hatujaenda mbali, Capacity Charge haikuwa dhuluma bali tulipaswa kulipa kutokana na nature ya mkataba tulioingia!!!
Ki-Tanzania ukisema hivyo unaambiwa sio Mzalendo as if Uzalendo ni kuwa Mjinga na Mbumbumbu!!!
Je, kwa sasa bado tunapaswa kulipa Capacity Charge?!
REMEMBER... kuna Mkataba wa Kuuziana Umeme na Leseni ya Kuuza Umeme! Hivyo ni vitu viwili tofauti!!! Jambo la kuhoji, Capacity Charge inatokana na nini? Inatokana na Mkataba wa Kununua Umeme au Leseni ya Kuuza Umeme?
Kwa maoni yangu, kwavile sifahamu mkataba upo vipi, Capacity Charge inatokana na Mkataba wa Kuuziana Umeme na sio Leseni ya Kuuza Umeme!!!
Capacity Charge inatokana na Mkataba wa Kununua Umeme kwa sababu, kama mkataba ungekuwa ni kuuziana umeme bila conditional ya mahitaji, yaani kuuziana continuously, basi Capacity Charge kuna uwezekano isingekuwapo! As we speak, Mkataba wa Kununua Umeme unaisha mwaka 2022.
So, unless Mkataba wa Kununua Umeme unavunjwa mapema iwezekanavyo, kuna hatari tutaendelea kulipa Capacity Charge hata kama kupitia mahakamani!!! Au, tutaendelea kulipa CC hadi pale mkataba utaakapovunjwa rasmi kama kuna hiyo room ya kuvunja!!!!
Hapo juu tena, kwa mujibu wa Tanzania yangu, nina sifa ya kuitwa sio Mzalendo kwa sababu wanadhani Uzalendo ni kuwa Mjinga au kufumbia macho FACTS!
REMEMBER, Haki na Sheria ni mambo mawili tofauti!!!!
Kaaazi kweli kweli!For 23 years wamekua wakila monthly pension ya billion 6 bila kufanya kazi yeyote ile.., bure kabisa
Nombeni kujilishwa kama hizi ni Kampuni Mbili tofauti.
1. PAN AFRICA POWER
2. PAN AFRICA ENERGY
Risk ipi? Ile risk ya kula billion 6 kila mwezi kiulaini kabisa, ufanye kazi au usifanye kazi ni uamuzi wako, 6B yako iko pale pale, au risk ipi unazungumzia?Hakuna athari yeyote ila wana mkataba hai....hilo ni pigo sio kwao tu wakitaifisha wawekezaji hawatakuja inabidi watumie akili sanaa nini cha kufanya!! Mwekezaji akija anakuw haelewi kama akikosea lolote halindwi na mkataba!! Ni tishio kwa wawekezaji!! Tuone busara kama ipo au hakuna kabisa!! Yeye ataondoka next 8yrs unaachaje nchi umevuruga miaka 100 mingine?? Sera za uwekezaji Zipo ila zinavunjwa nani atajenga viwanda?? Labda wajenge serikali.......maana wengine wataogopa!!! Makampuni mengi ya exploration yameamua kuondoka!!! Nani atakuja kwa hali ilivyo?? Sio rahisi kuwekeza kwenye risk!!!!
Rejea hiyo barua ya mwaka 2004, hiyo barua inaonyesha kwamba endapo IPTL itashindwa kuzalisha umeme pale watakapohitajika, kwa sababu zozote zile, iwe ubovu wa mitambo au ukosefu wa vibali, basi Tanesco ina haki ya kimkataba kuvunja mkataba huo.Ngoja niweke blah blah pembeni na kujifanya mzalendo linapokuja suala la Capacity Charge under normal condition. I am talking from business point of view na sio from (fake) nationalism point of view.
Hapa kuna mambo mawili... Power Purchase Agreement (PPA) na Leseni ya Uuzaji umeme!!!
PPA ni makubaliano kati ya serikali na IPTL kuuziana umeme pale kunapokuwa na hayo mahitaji! Mkataba huu ilikuwa ni IPTL kutuuzia umeme pale tu tunapokuwa na mahitaji ya ziada ya umeme... hususani pale tunapokuwa na upungufu wa uzalishaji umeme kutoka vyanzo vingine, hususan vyanzo vya maji!
Kwavile mkataba haukuwa kununua umeme wa IPTL wakati wote, hapo Capacity Charge haikwepeki hata kama ingekuwa ni wakati wa Nyerere! Hii ni kwa sababu, endapo mabwawa yetu yanakuwa na maji mwaka mzima, ina maana mitambo ya IPTL nayo ingezimwa mwaka mzima! Kama tusingekuwa na uhaba kwa miaka 5, ina maana mitambo ya IPTL nayo ingezimwa kwa miaka 5!!!!
Sasa sijui ni Mwekezaji gani angekubali aje kuwekeza mitambo kisha iwe inakaa hata mwaka mzima na zaidi bila kuingiza hata senti tano wakati kuna cost of wear and tear!!!
Hivyo kabla hatujaenda mbali, Capacity Charge haikuwa dhuluma bali tulipaswa kulipa kutokana na nature ya mkataba tulioingia!!!
Ki-Tanzania ukisema hivyo unaambiwa sio Mzalendo as if Uzalendo ni kuwa Mjinga na Mbumbumbu!!!
Je, kwa sasa bado tunapaswa kulipa Capacity Charge?!
REMEMBER... kuna Mkataba wa Kuuziana Umeme na Leseni ya Kuuza Umeme! Hivyo ni vitu viwili tofauti!!! Jambo la kuhoji, Capacity Charge inatokana na nini? Inatokana na Mkataba wa Kununua Umeme au Leseni ya Kuuza Umeme?
Kwa maoni yangu, kwavile sifahamu mkataba upo vipi, Capacity Charge inatokana na Mkataba wa Kuuziana Umeme na sio Leseni ya Kuuza Umeme!!!
Capacity Charge inatokana na Mkataba wa Kununua Umeme kwa sababu, kama mkataba ungekuwa ni kuuziana umeme bila conditional ya mahitaji, yaani kuuziana continuously, basi Capacity Charge kuna uwezekano isingekuwapo! As we speak, Mkataba wa Kununua Umeme unaisha mwaka 2022.
So, unless Mkataba wa Kununua Umeme unavunjwa mapema iwezekanavyo, kuna hatari tutaendelea kulipa Capacity Charge hata kama kupitia mahakamani!!! Au, tutaendelea kulipa CC hadi pale mkataba utaakapovunjwa rasmi kama kuna hiyo room ya kuvunja!!!!
Hapo juu tena, kwa mujibu wa Tanzania yangu, nina sifa ya kuitwa sio Mzalendo kwa sababu wanadhani Uzalendo ni kuwa Mjinga au kufumbia macho FACTS!
REMEMBER, Haki na Sheria ni mambo mawili tofauti!!!!
Kipindi cha Mkwere kulikuwa na mgao wa masaa 12 kila siku kwa mwaka mzima, hasa ktk mkoa wa Arusha. Huo ndo mgao mkali kwangu mimi. Mgao wa masaa 1-3 naweza kusema tumeshauzoea, ni kawaida.Mgawo mkali unakuwaje na usiokuwa mkali unakuwaje?
Sasa hayo maelezo yana uhusiano gani na nilichoandika?!Rejea hiyo barua ya mwaka 2004, hiyo barua inaonyesha kwamba endapo IPTL itashindwa kuzalisha umeme pale watakapohitajika, kwa sababu zozote zile, iwe ubovu wa mitambo au ukosefu wa vibali, basi Tanesco ina haki ya kimkataba kuvunja mkataba huo.
naona hata likes tunazopeana JF awamu hii ya 5,kwenye jf app,zinaishia kusoma 5.Awamu ya 5 hii
Post sent using JamiiForums mobile app
Sasa kama mliwapa wa kumkataba wa kununua umeme pale tu mnapohitaji ulitarajia nini?! Ingekuwa wewe ungekubali uwekeze mitambo lakini kuuza umeme ni hadi watakapotaka wao?!For 23 years wamekua wakila monthly pension ya billion 6 bila kufanya kazi yeyote ile.., bure kabisa
Of course, negotiation ni LAZIMA kwa watu wanaoweka mbele maslahi mapana ya taifa! Kwa mfano, Investor ata-propose capacity charge lakini upande wa serikali nao watatakiwa kwenda mezani na maximum proposed capacity charge kwamba, above that, no business!!!!As usual Mkuu Chige at your own best! Asante kwa darasa! Je haiwezekani kukubaliana viwango wa tofauti vya capacity charge kulingana na mahitaji yetu ya nishati?
Sent using Jamii Forums mobile app