SoC02 Mitaala ya Elimu na Rasilimali za Taifa

Stories of Change - 2022 Competition

Michael nguma

New Member
Jul 26, 2022
4
2
Michael nguma
0693110405

Inakuaje taifa kubwa kuwa na wasomi wengi wasio na maarifa katika rasilimali za taifa hilo?
Inakuaje taifa lenye mifumo ya elimu kuanzia ngazi za chini mpaka chuo kikuu linakuwa na wasomi wasio na maarifa ya kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao na kwa manufaa ya taifa?

Mitaala ya elimu iliyopo nchini haiendani na rasilimali zilizopo nchini, hali hii inasababisha wasomi wengi kutokuwa na maarifa katika rasilimali za nchi. Taifa pamoja na kuwa na vyuo vikuu vinavyozalisha wasomi kila mwaka, bado halijafanikiwa kuwa na mitaala ya masomo inayotoa maarifa ya rasilimali zilizoko nchini. Hii inasababisha taifa kutafuta wataalamu nje ya nchi pale litakapo kutumia rasilimali lilizo nazo.

Gharama kubwa inayotumika katika kutafuta wataalamu wenye maarifa ya rasilimali taifa iliyo nazo inatakiwa itumike katika kurekebisha mitaala ya masomo, ili masomo yatolewe katika mfumo ambao utatoa maarifa ya rasilimali za taifa.

Kuna hasara nyingi kwa taifa kutafuta wataalamu wenye maarifa ya rasilimali za taifa hilo nje ya taifa hilo ila hasara kubwa ni usalama wa rasilimali hizo. Taifa linatakiwa mara tu pale linapogundua rasilimali yeyote ile ndani ya taifa hilo, litengeneze mfumo wa elimu unaotoa maarifa ya rasilimali hiyo kwa watu wake kabla halijaanza kuitumia rasilimali hiyo.

Taifa linaeza likawa linakosea sana pale lianzapo kutumia rasilimali liliyo nayo pasipo mzalendo/mtu wake mwenye maarifa katika rasilimali hiyo.

Mifumo ya elimu inayotumika haimpi mhusika maarifa ya kujitambua wala haimpi mhusika maarifa ya kutumia rasilimali zinazomzunguka. Mifumo ya elimu iliyopo inampa mhusika maarifa ya kumtambua mwanzilishi wa kanuni flani mfano wa kanuni ya second law of motion na nyinginezo. Mifumo iliyopo haimpi mhusika maarifa ya kubuni, bali inampa mhusika maarifa ya kumjua aliebuni na namna alivyobuni.

Ikiwa wasomi wengi wana maarifa juu ya ubunifu ambao tayari ushabuniwa, watawezaje kuwa na maarifa juu ya ubunifu ambao bado haujabuniwa. Mifumo ya elimu inahitaji mabadiliko makubwa.

Mitaala ya elimu iliyopo inachangia sana katika kuzinyima akili za mhusika uhuru, haiwezekani mwanafunzi afungwe akili zake kwa kanuni za mbunifu flani alafu mwanafunzi huyo huyo awe mbunifu!!. Inashangaza kuona wabunifu wengi kwa ubinafsi wao wameweka kanuni katika ubunifu wao, ili watu wafuate kanuni hizo wasije wakabuni kitu kikubwa kuliko hicho chao walichobuni.

Taifa linahitaji mitaala ya elimu inayotoa uhuru wa akili za mwanafunzi, miltaala inayotengeneza wanafunzi wasiofungwa akili zao kwa kanuni flani za mahesabu flani...na hapo ndipo taifa litakapoweza kupata wabunifu wengi.

Ikiwa taifa halitabadilisha mifumo ya elimu iliyopo, litaishia kuwa na wasomi wengi wasio na maarifa ya rasilimali zinazowazunguka, litakuwa na wasomi wengi wasioweza kuongeza thamani katika rasilimali zinazowazunguka.
 
Hata kama haijakuvutia naomba kura yako, maana kweli siku hizi ni nguma na uongo ni mlaini. Naomba kura yako nibadilishe maisha. ASANTE
 
Back
Top Bottom