Huo ndiyo ukweli halisi ambao CCM inakuwa vigumu kuumeza.
Hilo ndilo lilikuwa goli la mwisho la mkono ambalo lilikuwa limebaki kwa maccm.
Hata hivyo hebu tuangalie kwa kutumia common sense tu, ikiwa NEC wamesema mara tu baada ya kuhesabu kura matokeo yote ya udiwani, ubunge na Urais yatabandikwa vituoni, sasa matokeo hayo yatasomwa na nani iwapo wapiga kura wote watakuwa 'wamelazimishwa' kwenda kulala majumbani kwao?
Swali la pili ambalo ndilo la muhimu zaidi, kwa kuwa vituo vingi vya kupigia kura vipo kwenye makazi ya watu, sasa iwapo agizo la JK kutaka watu wasiwepo ndani ya mita 200 toka kituo cha upigaji kura, ina maana wakazi wote hao walio ndani ya mita 200 watatakiwa kuwa 'wakimbizi' kwa lazima kuyakimbia makazi yao?!