Misukosuko Izalishayo Kauli Tata .

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,780
Members ,
Ni matumaini yangu tumeamka salama J'3 ya leo.
Wiki kadhaa nyuma nikiwa katika mishemishe zangu za kusaka daily Bread , dira zangu siku hiyo zikahitaji niende pembezoni mwa Jiji ninapoishi .
Ni safari iliyonilazimu nipande kwanza Daladala nishuke, kisha nipande Ferry linifikishe huko nilipokua nakwenda .
Wakati tukiwa kwenye Ferry na tumekaribia kufika upande wa pili , mara kwa ghafla tukasikia makelele ya mtu (Me) aliyekua akipiga mayowe ya kuomba msaada wa kuokolewa kuzama majini .
Mabaharia waliokua kwenye Ferry tuliopanda nikawaona wamekurupuka na wakaanza jitihada za kumuokoa mtu yule .
Ilichukua kitu takriban dakika 15 hivi , mabaharia wale kufanikiwa kumuopoa toka katika msukosuko ule uliokua ukiendea kuyagharimu maisha yake .
Mtu yule baada ya kuopolewa akawa yumo kwenye Ferry tulilokuwemo .
Mabaharia na baadhi ya abiria wenzangu wakawa wanamuhoji maswali .
Maswali kama :-
"Wewe ni mvuvi ?"
" Ulikua unafanya nini kwenye maji?" "Unajua kuogelea? " n .k
Yule mtu aliongea neno moja tu ! Kisha hakuongea tena hadi tukashuka kwenye Ferry .
Aliongea hivi :
"Sitorudi tena kwenye maji , hadi niwe nimejua kuogelea ! Nasema sirudi Ng'oo ! "
Mimi maneno hayo, ya huyo mtu yameniachia changamoto, hadi hivi sasa bado najiuliza huyo mtu kwa kudai hatorudi kwenye maji hadi ajue kuogelea !
Atajifunzia wapi kuogelea pasipokua na maji?.
Baadae nikapata jibu kwamba binadamu anapokua kwenye taharuki ama msukosuko huweza sana kutamka kauli zenye utata kama hiyo.
Nawe member mwenzangu mpendwa, napenda unichangie katika baadhi ya matukio uliyoyaona na ukasikia kauli tata zilizotoka kwa waliokua wamepatwa na misukosuko ,
Karibu .
 
Dah mi hiyo kauli yake nimeipenda sana kwani imenichekesha sana ingawa labda sikupaswa kucheka.
 
Unaweza kujifunza kuogelea inchi kavu halafu ukaenda kuogelea baada ya kuelewa. Theory and Practal.
 
atarudi tu majini ngoja akili yake itulie uone kama hajarudi huko baharini.
 
"KULA SIRI KULALA SILALI, USIKU KUCHA NAKUOTA WEWE!", hii ndo inayonichanganyaga mimi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom