Mistari ya JK: hivi hii mmeishaiona? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mistari ya JK: hivi hii mmeishaiona?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ms Judith, Mar 4, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Swali: Mheshimiwa Rais je unawajua wamiliki wa kampuni ya Dowans?


  Jibu:
  Nasema mimi sijui, ni kina nani sijui,
  Wanatoka wapi sijui, walifikaje sijui,
  Kama nawafahamu sijui, kama wananijua sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Mheshimiwa Rais, lakini waliingia nchini na kupata Mkataba wa Richmond na kuleta majenereta katika kutekeleza mpango wako wa kupunguza tatizo la umeme nchini kweli huwajui?


  Jibu:
  Nasema mimi sijui!, kwanini walikuja sijui,
  Uhusiano wao siujui, Kama nao Richmond sijui,
  Waliingia kwa lipi sijui, na walirithishana vipi sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Lakini ulisema kuwa Richmond ni kampuni Hewa kama Kamati ya Mwakyembe ilivyoonesha na kudai, na ukatoa pongezi! Unawaeleza vipi Watanzania kuwa Taifa liko tayari kuheshimu mkataba wa kampuni ya kitapeli?


  Jibu:
  Nasema tena sijui!Kama kampuni hewa sijui,
  Kama ni matapeli sijui, Kama walibebwa sijui,
  Wahusika kina nani sijui, Mwakyembe alijuaje sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!
  Tulikoanzia sijui, tumefika vipi sijui,
  Nahusika vipi sijui, nimuulize nani sijui,
  Niwaridhishe vipi sijui, nianzie wapi sijui!
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Lakini Rostam Aziz ametajwa kuhusika kuanzia mwanzo wa sakata hili na yeye mwenye amekiri kuhusika na hili kwanini usimuulize ili ujue?


  Jibu:


  Nitamuanza vipi sijui, Rostam huyu sijui,
  Kama mwingine sijui, anahusika vipi sijui
  Nimuamini nani sijui, kama ni kweli sijui!
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Lakini, inawezekana vipi usijue wakati una vyombo vingi vya usalama ambavyo vingeweza kukupata taarifa mbalimbali za kiinteligensia kama walivyoweza kuzipata kule Arusha na kuvunja maandamano ya Chadema? Kwanini hujapatiwa taarifa za kiinteligensia kuhusu Dowans?


  Jibu:


  Intelligensia mimi sijui, nani anipe sijui,
  Kwanini wanipe sijui, nifanye nayo nini sijui,
  Wasiponipa sijui, kama nadaganywa sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Nani awaagize sijui, kama nini mimi sijui,
  Au makamu sijui, Waziri Mkuu sijui,
  Wajitolee tu sijui, au ni Bunge mimi sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Sasa msimamo wako wewe binafsi kama Rais ni upi, Dowans walipwe au wasilipwe?


  Jibu:


  Msimamo gani sijui! Kama ninao sijui,
  Nilikuwa nao sijui, nitakuwa nao sijui,
  Kama walipwe sijui, na wasilipwe sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Wizara ilipe sijui, Au Tanesco sijui,
  Au huko hazina sijui, au hapa Ikulu sijui,
  Bunge litenge fedha sijui, au Mahakama sijui,
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Sasa mheshimiwa inaonekana hujui mambo mengi tu; kuna mambo mengine yoyote unayoyajua?


  Jibu:
  Kwanini masikini sijui, Kagoda ni nani sijui,
  Meremeta nani sijui, Dipu Grini nani sijui,
  Mbona elimu duni sijui, wanagomea nini sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Sijui mimi sijui, mengine mengi sijui,
  Ya kilimo siyajui, ya Sayansi siyajui,
  Mambo ya maji sijui, umeme ndiyo sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!
  Kama napendwa sijui, kama nachukiwa sijui,
  Nafurahiwa sijui, au nakejeliwa sijui,
  Kama ninachekewa sijui, au nakebehiwa sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Swali: Mheshimiwa swali la mwisho; asante sana kwa kutupa nafasi hii na kwa hakika umetuelewesha na tumeelewa kuwa hujui mambo mengi sana. Labda uwaambie Watanzania, je wewe ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?


  Jibu:


  Sijui mimi sijui, ninarudia sijui,
  Kama miye sijijui, mtajuaje sijui
  Kama najua sijui, kama sijui sijui
  Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji -BGM)
   
 2. stwita

  stwita JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 1,184
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  ikienda studio inaweza kuwa rap safi sana
   
 3. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mimi najua kuweka chorus. afu malipo studio juu yangu!
   
 4. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  MM alisahau hii, KWANINI SISI NCHI MASKINI SIJUI, INGAWA TUNA MADINI SIJUI,NA MBUGA ZA WANYAMA SIJUI,MLIMA KILIMANJARO SIJUI,NASEMA TENA SIJUI...LOL,
   
 5. T

  Tewe JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2011
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 744
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  nilikuwa nimekasirika lakini kwa hii siku imekwisha vizuri kwa kicheko, asanteni wana jf
   
 6. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HApa Mwanangu Museveni haoni ndani, mistari anashuka, Hii singo inatoka lini kama mmefuatilia kwa karibu?
   
 7. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,555
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Jioni yangu imekuwa njema kwa hizi rylics.Na huo ndio upeo wake kweli wala sio utani.
   
 8. c

  chidide Member

  #8
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  For sure you are veru creative, maana nilikuwa kama vile naona jinsi Asiyeheshimiwa JK anavyojibu!!!
   
 9. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Napia alisahau kuuliza kwa nini anasafari nyingi zisizoisha nchi za nje

  Kama nasafiri sijui, naenda wapi sijui
  Naenda kubembea jamaika sijui, mimi ni mtalii sijui
  Marekani mimi sikujui, Obama simjui
  Safari zina tija sijui, natangaza njaa sijui
   
 10. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Maisha bora kwa mtz,sijui. Kama nlihadi sijui,kama nlihaidi mgao wa umeme sijui. Kama majenereta ya Ali alidaiwi yamezimwa sijui,kama yamewashwa sijui. Na cdm wanikera sijui,kama nahandaa hotuba ya kuikimbia ikulu sijui,na lini sijui. Wananchi hawanitaki sijui,kama ntamwachia kiti makamba Jr. Sijui au Riz1 sijui. Mh. Mtangazaji anayenihoji,nawe sikujui. Kusema kwa heri sijui. Mh mtangazaji mimi sijui,nasema yote sijui. Sijui kwa kuwa sijui. Sijui mimi sijui.
   
 11. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  dah,sijui kama sijui,....hahahaha na watanzania wengi hawajui kama wana raisi ambaye hajui
   
 12. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Aaah aaah am happy now I was furious on the way our prime minister is doing things but these lyrics have made my day ...-lol
   
 13. 2015ready

  2015ready JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mwanakijiji.
  Ingia studio bwana. Mistari imetulia sana hiyo na uhakika utauza hiyo singo kwa mamilioni ya pesa.
  Tehetehete !!!
   
 14. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Chorus-sitaki nijue kama mimi "sijui" unauliza "sijui" kitugani "sijui" mwandishi "sijui" karibu tena"siiijuuuiiiiii"
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ngojeni tu... naona hii ni mara ya tatu hii mistari inazungushwa tena.. the first time mojawapo ya hizi kazi imeonekana kuvutiwa na watu. Shukrani!!
   
 16. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Chorus-sitaki nijue kama mimi "sijui" unauliza "sijui" kitugani "sijui" mwandishi "sijui" karibu tena"siiijuuuiiiiii"
   
 17. Abigree

  Abigree Member

  #17
  Mar 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hlo song jina gan?
   
 18. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,222
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Chorus-sitaki nijue kama mimi "sijui" unauliza "sijui" kitugani "sijui" mwandishi "sijui" karibu tena"siiijuuuiiiiii"
   
 19. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Ndugu, Usisahau mchango wangu hapo juu,uingize kwenye vina vyako....
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,374
  Likes Received: 414,694
  Trophy Points: 280
  PHP:
  My body belongs to GodI am just holding it in TRUST
  I JESUS CHRIST we trust...............................................
   
Loading...