Mistari ya JK: hivi hii mmeishaiona?

Mistari ya JK: hivi hii mmeishaiona?

It baffles me how JK is really our president...............................we must be a bunch of lunatics to accept a mediocre running our nation.................
 
Swali: Mheshimiwa Rais je unawajua wamiliki wa kampuni ya Dowans?


Jibu:
Nasema mimi sijui, ni kina nani sijui,
Wanatoka wapi sijui, walifikaje sijui,
Kama nawafahamu sijui, kama wananijua sijui,
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Mheshimiwa Rais, lakini waliingia nchini na kupata Mkataba wa Richmond na kuleta majenereta katika kutekeleza mpango wako wa kupunguza tatizo la umeme nchini kweli huwajui?


Jibu:
Nasema mimi sijui!, kwanini walikuja sijui,
Uhusiano wao siujui, Kama nao Richmond sijui,
Waliingia kwa lipi sijui, na walirithishana vipi sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Lakini ulisema kuwa Richmond ni kampuni Hewa kama Kamati ya Mwakyembe ilivyoonesha na kudai, na ukatoa pongezi! Unawaeleza vipi Watanzania kuwa Taifa liko tayari kuheshimu mkataba wa kampuni ya kitapeli?


Jibu:
Nasema tena sijui!Kama kampuni hewa sijui,
Kama ni matapeli sijui, Kama walibebwa sijui,
Wahusika kina nani sijui, Mwakyembe alijuaje sijui,
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!




Tulikoanzia sijui, tumefika vipi sijui,
Nahusika vipi sijui, nimuulize nani sijui,
Niwaridhishe vipi sijui, nianzie wapi sijui!
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Lakini Rostam Aziz ametajwa kuhusika kuanzia mwanzo wa sakata hili na yeye mwenye amekiri kuhusika na hili kwanini usimuulize ili ujue?


Jibu:


Nitamuanza vipi sijui, Rostam huyu sijui,
Kama mwingine sijui, anahusika vipi sijui
Nimuamini nani sijui, kama ni kweli sijui!
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Lakini, inawezekana vipi usijue wakati una vyombo vingi vya usalama ambavyo vingeweza kukupata taarifa mbalimbali za kiinteligensia kama walivyoweza kuzipata kule Arusha na kuvunja maandamano ya Chadema? Kwanini hujapatiwa taarifa za kiinteligensia kuhusu Dowans?


Jibu:


Intelligensia mimi sijui, nani anipe sijui,
Kwanini wanipe sijui, nifanye nayo nini sijui,
Wasiponipa sijui, kama nadaganywa sijui,
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Nani awaagize sijui, kama nini mimi sijui,
Au makamu sijui, Waziri Mkuu sijui,
Wajitolee tu sijui, au ni Bunge mimi sijui,
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Sasa msimamo wako wewe binafsi kama Rais ni upi, Dowans walipwe au wasilipwe?


Jibu:


Msimamo gani sijui! Kama ninao sijui,
Nilikuwa nao sijui, nitakuwa nao sijui,
Kama walipwe sijui, na wasilipwe sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Wizara ilipe sijui, Au Tanesco sijui,
Au huko hazina sijui, au hapa Ikulu sijui,
Bunge litenge fedha sijui, au Mahakama sijui,
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Sasa mheshimiwa inaonekana hujui mambo mengi tu; kuna mambo mengine yoyote unayoyajua?


Jibu:
Kwanini masikini sijui, Kagoda ni nani sijui,
Meremeta nani sijui, Dipu Grini nani sijui,
Mbona elimu duni sijui, wanagomea nini sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Sijui mimi sijui, mengine mengi sijui,
Ya kilimo siyajui, ya Sayansi siyajui,
Mambo ya maji sijui, umeme ndiyo sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!




Kama napendwa sijui, kama nachukiwa sijui,
Nafurahiwa sijui, au nakejeliwa sijui,
Kama ninachekewa sijui, au nakebehiwa sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Swali: Mheshimiwa swali la mwisho; asante sana kwa kutupa nafasi hii na kwa hakika umetuelewesha na tumeelewa kuwa hujui mambo mengi sana. Labda uwaambie Watanzania, je wewe ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?


Jibu:


Sijui mimi sijui, ninarudia sijui,
Kama miye sijijui, mtajuaje sijui
Kama najua sijui, kama sijui sijui
Nasema mimi sijui, tena nasema sijui!


Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji -BGM)
Bro. U r so great in so many of your writings you but with this one, naomba niseme I couldn't stop laughing. U know, umeelezea vitu serious na vya kweli katika mtindo ambao si tu, mtu atajua kinachoendelea katika utawala huu bali ataburudika na kucheka wakati anasoma. Kaka, you are the Greatest!
 
Ni kweli kabisa,
Nakumbuka watoto wanapojaribu kukwepa responsibility kwa makosa waliyofanya kutokana na michezo yao ya kitoto kama kuvunja vifaa vya udongo nk. Nani kavunja chemli..... Thijui! (Wakati wao ndo walikuwa home), Nani alikuwa nyumbani wakati inavunjika?....... Thijui! Haya niambieni wapi mlienda leo?.......... Mie thijaenda popote leo. .... Sasa kwa nini hukuona ilipovungika? ... Thijui yenyewe! Haya ndo mambo ya kiongozi wetu huyu.
Hajui chochote muhimu katika matatizo yetu.
 
View attachment 24374
kama hundi waliiandika kwa maneno ilikuwa ni tofauti na walivyoandika kwa tarakimu mimi sijui,
sijui ile pesa ingesaidiaje taifa hili sijui, nasema mimi sijui,
sijui chochote mimi sijui, nasema mimi sijui.
 
I love this, no better way to describe JK aka Jamb.zi K.u than this! Ushauri, uza songi hili kwa Sugu, au shirikiana naye. Then juu ya kasha, hiyo picha ya hundi iwe kwenye cover. Mtafikisha ujumbe kwa milions of Tanzanians!
 
Back
Top Bottom