Mbona wamasai huku mjini wanazunguka na masime, mafimbo, virungu lakini wala hatuwashangai, tunadhani ni utamaduni, jaribu kumchokoza uone atakavyokushughulikia na hizo silaha zake ni balaa!!!!!
Hii picha ilishaonyeshwa humu JF, sijui kwa nini niarudiwa rudiwa, ilipoonyweshwa mara ya mwisho walisema ilipigwa kilimanjaro na baadhi ya wachangiaji walisema labda alitokea shambani. Lakini pamoja na hayo yote tujiuulize katika nafsi zetu je tunawaheshimu wazee wetu katika jamii?? Huyu bibi is a private citizen, siyo mwanasiasa, siyo fisadi wa ccm na sheria za tanzania hazikatazi mtu kubeba panga au jambia au kisu. Kosa lake ni nini hadi akashifiwe kiasi hiki na great thinkers wa JF?? Kumdhalilisha huyu bibi kwa hizi comments zenu na kuweka picha yake kwenye public media bila idhini yake ni ukosefu wa adabu uliopitiliza na ni uvunjaji wa haki yake kama binadamu kuwa huru kutenda apendalo ili mradi havunji sheria. Suppose huyu ni mama yako mzazi au bibi yako aliyetokea shambani na zana zake za shambani na akakuta mtoto au mjukuu amezimia kwa homa kali, bila kuchelewa akamkimbiza dispensary ya kijijini!!! Je utafurahia hizi dhihaka na kashifa???? Jamani tuacheni ukafiri!! Waheshimuni baba na mama zenu ili siku zenu ziwe nyingi katika nchi mpewayo na bwana Mungu wenu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.