Serikali toa tamko kuhusu ugonjwa uliokikumba Kijiji cha Magoma Tarime

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
479
1,253
Ni siku ya nne heka heka katika kituo cha afya Magoma kilichopo Kijiji cha Magoma Wilaya ya Tarime

Gari la wagonjwa likiwa bize kuhamisha wagonjwa wanaozidiwa na kupekekwa hospitali ya mji wa Tarime huku vifo vikitokea

Ni ugonjwa usiojulikana ambao umevamia kijijini hapo ambapo wagonjwa ni kuharisha na kutapika mfululizo na kuishiwa nguvu

Baadhi ya tetesi ambazo hazijadhibitishwa na mganga mkuu wanasema ni kipindupindu lakini mwenyekiti wa Kijiji hicho akiwa kwenye msiba wa mgonjwa aliyefariki kutokana na ugonjwa huo amesema madaktari wamechukua sample na kuituma maabara ya Taifa Dar es salaam na bado majibu hajatolewa licha ya siku kadhaa kupita na kuwasihi wananchi wachukue tahadhari

Serikali wambie wanajamii ni ugonjwa gani umevamia Kijiji hicho
 
Back
Top Bottom