""miss Tanzania Arudisha Taji Na Pesa "" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

""miss Tanzania Arudisha Taji Na Pesa ""

Discussion in 'Entertainment' started by Pdidy, Aug 10, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Balozi wa Redds arudisha taji

  MSHIRIKI WA MISS TANZANIA
  Angela Luballa

  Angela Luballa leo aliwashangaza watu alipoamua kurejesha taji hilo wiki moja tangu avalishwe.
  Luballa ambaye pia alishika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema kuwa imani yake haimruhusu kuwa Balozi wa REDDS.
  “Imani yangu kwa Yesu ni kubwa mno na hainiruhusu mimi kuwakilisha REDDS, hivyo nimeamua kurejesha taji na zawadi za fedha nilizopewa,” alisema Luballa.
  “ Nimerudisha taji hili si kwa shinikizo la mtu yeyote bali ni imani yangu, siwezi kuwa balozi wa REDDS.”
  Luballa ambaye inaaminika ni mtoto wa mchungaji ana imani ya kanisa lao ambalo haliruhusu kujihusisha na kitu chochote kinachohusu pombe.
  Luballa anasali katika Kanisa la World Alive International Outreach lililopo Sinza.
  Mrembo huyo alisema kuwa tayari ameshaiarifu Kamati ya Miss Tanzania na kurudisha taji na fedha Sh milioni 2.5 alizopewa kwa kutwaa taji hilo.
  Tangu mwaka 2006, REDDS imekuwa na utaratibu wa kumtangaza balozi wa bidhaa hiyo ambaye anapewa majukumu ya kufanya shunguli za kijamii kupitia kinywaji hicho.
  Kwa ushindi huo, Luballa alitakiwa kupewa Sh milioni 2.5 na posho ya Sh 250,000 kwa mwezi kazi ambayo angeifanya kwa mwaka mzima.
  Taji la Miss REDDS mwaka jana alikuwa ni Victoria Martin.
  Alipoulizwa Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema kuwa tayari ameshapata taarifa za kurejeshwa kwa taji hilo.
  “ Mimi niko nje ya mji, ila nimeshapewa taarifa kuwa mrembo huyo amerudisha zawadi, nitalizungumza kwa kina pindi nitakaporejea,” alisema
   
 2. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mbona ziko 2 on the same topic,zingeunganishwa
   
 3. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  kwani huyo miss dini yake inaruhusu kushiriki yale mashindano ya ulimbwende kwa kukaa uchi ila hayarusu pombe?
   
 4. Novatus

  Novatus JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2008
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 331
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu binti anatuyeyusha. Iweje ashiriki mashindano ya Urembo halafu aseme hawezi kuwa balozi wa Redds. Hivi alitegemea nini kushiriki haya mashindano??? Anastahili adhabu kali kwa kitendo hicho
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  alitaka gari lile jamani akaubiri injili
   
 6. Manda

  Manda JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 2,075
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  I think she was not seriuos...ni bora angebakia kanisani kwake awe muimba kwaya tuu!, ukila mbaazi tegemea.......(?), umechemka dada!
   
 7. LUSAJO L.M.

  LUSAJO L.M. JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 223
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mwendo wa pesa ni muhimu katika kufanya kila kitu...oooh ooh!
   
Loading...