MISINGI YA NDOA !! Zingatia!!!!!

MISINGI YA NDOA !! Zingatia!!!!!

Madame B upoooooooooo!! nazidi tu kuamini yeye ni wife material,anaupendo hadi shetani anamuogopa!!

hahaha! Mgomvi wewe!! Na uyazingatie hayo ! Siyo kesho na kesho kutwa unamsema mkeo mbele za watoto heshma ichukue mkondo wake ! Umeelewa mwekundu? Cc Himidini
 
Last edited by a moderator:
Madame B upoooooooooo!! nazidi tu kuamini yeye ni wife material,anaupendo hadi shetani anamuogopa!!

Nipo mdogo wangu.
Unajua nini ee... Najua nimeingia sehemu sahihi katika suala zima la mahusiano.
Himidini hana tatizo nami.
Nawe usiwe na wasi na Munkari.
 
Last edited by a moderator:
ila ndoa bila Mungu aisee inakuwa ngumu kweli. ni vyema kumshirikisha Mungu sana kwa mambo yote yaliyo na yasio katika uwezo wenu. maana msingi wa ndoa ni Mungu mwenyewe.
 
ila ndoa bila Mungu aisee inakuwa ngumu kweli. ni vyema kumshirikisha Mungu sana kwa mambo yote yaliyo na yasio katika uwezo wenu. maana msingi wa ndoa ni Mungu mwenyewe.

yap true true!! Mungu ni muweza wa yote! Bila kumsahau yeye!!
 
Msingi mkuu wa maisha ya ndoa ni UPENDO WA DHATI wa wanandoa wenyewe.kupendana kama walivyo.Ni jukumu la kila mwanandoa kuutunza upendo huo,kupalilia ukue vema,udumu na uzae matunda.Ili upendo wa wanandoa udumu,unahitaji mambo yafuatayo....HESHIMA KWA KILA MMOJA(hakuna aliyezaidi).Kila mwanandoa atambue na kuthamini uwepo wa mwenzake katka familia.Jali MATATIZO na FURAHA ya mwenzako.Usimfanye mwenzio kama chombo tu cha matumizi ndani ya nyumba.Mpe hadhi na heshima yake..,.pia UAMINIFU KWA KILA MMOJA-Kila mwanandoa ajitahidi kuwa mwaminifu kwa mwenzake ndani na nje,uaminifu na kuaminiana vina maana na uzito wa pekee ktk ndoa......KUSAIDIANA NA KUSHAURIANA(kubali ushauri wa mwenzio)Si vema kuona mwenzako hana maana kwako.Mungu amekupa huyo kama msaidizi wako,umshauri nawe ukubali akushauri.Hatakama unauona duni na mnyonge vip,si ulimpenda mwenyewe?iweje leo hutaki ushauri wake?kumbuka-Hata NG'OMBE mweusi hutoa maziwa meupe!...KUSHIRIKISHANA MIPANGO MBALIMBALI(Usiri ni sumu katk ndoa)Wanandoa mnapaswa kushirikishana mipango yenu ktk familia.Jambo laweza kuwa zuri kwa lenyewe lakini kama halikushirikishwa kwa mwenzi,laweza kuwa na harufu ya ubovu na hatimaye kuwa chanzo cha malumbano....KUVUMILIANA NA KUCHUKULIANA-Si kila jambo litakubalika kwa mwenzio,kuna mengine mnaweza kurekebishana mengine mtashindwa kabisa.Hayo yanayoshindkana kabsa basi uvumilivu wa kweli uchukue nafasi yake.NDOA zinazodumu ni za watu wavumilivu tu!.....KUJENGANA NA KUSAHIHISHANA KWA UPENDO.Yawezekana ktk maisha ya kila siku wanandoa mkakoseana na kukosea katka mambo mbalimbali.Iepukwe kila namna ya kushabikia/kubeza kosa la mwenzako badala yake mjenge hulka ya kuoneana huruma na kujengana ktka utu wema.kumbuka-aibu ya mwenzako ni yako pia!....UTUNZAJI SIRI ZA NDANI YA NDOA-Ni aibu kubwa sana kwa wewe mwanamke/mwanaume kuanika siri za mwenzio hadharani,kufanya hvyo ni kuhatarisha ndoa yenu wenyewe.mambo ya ndani yabaki ndani,kama itakuwa lazima sana yatoke nje,basi na yatoke kwa BUSARA KUU SANA ++

munkari uko ndoani au we kungwi? vigezo vyote ninavyo naomba nikuone kama bado uko single.
 
munkari uko ndoani au we kungwi? vigezo vyote ninavyo naomba nikuone kama bado uko single.
Munkari yupo ndoani,mumewe naye yumo humu JF anaitwa Mokoyo,mara ya mwisho alikuwa anafanya kazi Sudan lakini kwa sasa yupo hapa bongo kila siku anatembea na kikopo,watu wanasema ni tindikali ila mi sina uhakika na hilo.Baba mkubwa Kaizer alisema eti pia ana mguu wa kuku,kwa hiyo ukitaka aku Ufosaro endelea tu mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Tunashukuru mtoa mada sasa ni kukazana kuomba milango ya baraka iendelelee kufunguka ili tukifanikiwa tukapate kuyapractise na tunawaombea waliopo wapate kuyaangalia kwa kina. asante mtoa mada upate kujawa na furaha ya moyo.
 
hahaha! Loh nashukuru kwa jibu zuri murua!! Ushamaliza ntafute nikununulie kijoti na chama!!
 
Last edited by a moderator:
Tunashukuru mtoa mada sasa ni kukazana kuomba milango ya baraka iendelelee kufunguka ili tukifanikiwa tukapate kuyapractise na tunawaombea waliopo wapate kuyaangalia kwa kina. asante mtoa mada upate kujawa na furaha ya moyo.

asante Shuju barikiwa saaana!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom