MISINGI YA NDOA !! Zingatia!!!!!

MISINGI YA NDOA !! Zingatia!!!!!

Munkari

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2013
Posts
8,084
Reaction score
4,365
Msingi mkuu wa maisha ya ndoa ni UPENDO WA DHATI wa wanandoa wenyewe.kupendana kama walivyo.Ni jukumu la kila mwanandoa kuutunza upendo huo,kupalilia ukue vema,udumu na uzae matunda.Ili upendo wa wanandoa udumu,unahitaji mambo yafuatayo....HESHIMA KWA KILA MMOJA(hakuna aliyezaidi).Kila mwanandoa atambue na kuthamini uwepo wa mwenzake katka familia.Jali MATATIZO na FURAHA ya mwenzako.Usimfanye mwenzio kama chombo tu cha matumizi ndani ya nyumba.Mpe hadhi na heshima yake..,.pia UAMINIFU KWA KILA MMOJA-Kila mwanandoa ajitahidi kuwa mwaminifu kwa mwenzake ndani na nje,uaminifu na kuaminiana vina maana na uzito wa pekee ktk ndoa......KUSAIDIANA NA KUSHAURIANA(kubali ushauri wa mwenzio)Si vema kuona mwenzako hana maana kwako.Mungu amekupa huyo kama msaidizi wako,umshauri nawe ukubali akushauri.Hatakama unauona duni na mnyonge vip,si ulimpenda mwenyewe?iweje leo hutaki ushauri wake?kumbuka-Hata NG'OMBE mweusi hutoa maziwa meupe!...KUSHIRIKISHANA MIPANGO MBALIMBALI(Usiri ni sumu katk ndoa)Wanandoa mnapaswa kushirikishana mipango yenu ktk familia.Jambo laweza kuwa zuri kwa lenyewe lakini kama halikushirikishwa kwa mwenzi,laweza kuwa na harufu ya ubovu na hatimaye kuwa chanzo cha malumbano....KUVUMILIANA NA KUCHUKULIANA-Si kila jambo litakubalika kwa mwenzio,kuna mengine mnaweza kurekebishana mengine mtashindwa kabisa.Hayo yanayoshindkana kabsa basi uvumilivu wa kweli uchukue nafasi yake.NDOA zinazodumu ni za watu wavumilivu tu!.....KUJENGANA NA KUSAHIHISHANA KWA UPENDO.Yawezekana ktk maisha ya kila siku wanandoa mkakoseana na kukosea katka mambo mbalimbali.Iepukwe kila namna ya kushabikia/kubeza kosa la mwenzako badala yake mjenge hulka ya kuoneana huruma na kujengana ktka utu wema.kumbuka-aibu ya mwenzako ni yako pia!....UTUNZAJI SIRI ZA NDANI YA NDOA-Ni aibu kubwa sana kwa wewe mwanamke/mwanaume kuanika siri za mwenzio hadharani,kufanya hvyo ni kuhatarisha ndoa yenu wenyewe.mambo ya ndani yabaki ndani,kama itakuwa lazima sana yatoke nje,basi na yatoke kwa BUSARA KUU SANA ++
 
Hapo umenena kuweka udhaifu wa mwenzio hadharani ni hatari hata humu JF ni hadharani kuzisema humu hautatofautiana na wale wanaosema huko vijiweni
 
kweli kabisa Munkari
above all:upendo ndo kila kitu
ukiwa na upendo kwa mwenzio utastahimili vingi
 
Last edited by a moderator:
kweli kabisa Munkari
above all:upendo ndo kila kitu
ukiwa na upendo kwa mwenzio utastahimili vingi
mwallu nakusalimu hujambo?

Ndio maana Maandiko yanasema "nijaposema kwa Lugha za wanadamu na za malaika kama sinao Upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao .....si kitu mimi" (1 Kor.13:1-8)
 
Last edited by a moderator:
maneno kuntu,.......hapo ndo wanapofeli wanandoa wengi vipengele hivyo hapo!!
 
Habari haswa waisome na waizingatie wale wote ambao hawajaanza kulala bila vyupi...
 
hapo kwenye UVUMILIVU!!!! me sijaingia lakini huwa naamini uvumilivu huwa unaisha me nahisi UPENDO HAPO ndo kila kitu.
 
sijambo kabisa..halafu umeona ee
yani bila upendo ni burreeee kabisa
mwallu nakusalimu hujambo?

Ndio maana Maandiko yanasema "nijaposema kwa Lugha za wanadamu na za malaika kama sinao Upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao .....si kitu mimi" (1 Kor.13:1-8)
 
Habari njema sana hii na ni nzuri kwa wanaojiandaa kuingia katika ndoa mie naamini na bado naamini ndoa ni jinsi mtu atakavyotaka iwe,ukiwa mbishi na mbabe ama hauoneshi kujali ya mwenzio na mbinafsi mwisho ndoa itakuwa ngumu na nzito bora ya zege la tani10 ...akhsante mkuu kwa kutupa nini maana ya ndoa ya kweli na Mungu akubariki.
 
ninashukuru saana kwa mada yako imenibariki sana
hasa hasa upande wa ndoa ni kuvumiiliana, kuchukuliana, kuheshimiana na kuwa na upendo
umetukumbusha mambo ya muhimu sana
 
Back
Top Bottom