Mishahara ya wafanyakazi wa serikali iko wapi mwezi huu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mishahara ya wafanyakazi wa serikali iko wapi mwezi huu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Jul 30, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Leo ni tarehe 30 July 2009,na hakuna dalili yeyote kwamba wafanyakazi wa serikali watapata mishahara yao.Mitaani tunasikia wafanyakazi wa serikali kuu wakiilalamikia serikali yao katika kiwango cha kutisha sana.

  Tunacho hoji ni kwamba inakuwaje maagiza ya Rais yanakiukwa bila hata wafanyakazi husika kupewa taarifa yeyote?Itakumbukwa kwamba Rais alishaagiza ifikapo tarehe 23 ya kila mwezi wafanyakazi wawe wameshapata mishahara yao.Akaongeza kwamba kama itakuwa lazima kucheweshewa mishahara yao,basi isizidi tarehe 25 ya kila mwezi.

  Ikumbukwe kwamba mishahara ya wafanyakazi wa serikali ni midogo mno,na kwa sababu hiyo wengi wao hawana njia nyingine yeyote ya kujipatia kipato.Kwahiyo wakicheleweshewa mishahara athari ina kuwa kubwa sana kwa wao wenyewe na wale wote wanao wategemea.

  Tunaiomba serikali iwe makini zaidi katika swala hili ili kuwaepushia wafanyakazi usumbufu usio wa lazima.Tunaelewa fika kwamba kuna uzembe katika swala hili,kwa hiyo wale wote wanaochelewesha mishahara aidha kwa makusudi au kwa uzembe,wachukuliwe hatua kali za kinidhamu zinazostahili.

  Mungu wabariki wafanyakazi wa Tanzania na naomba uwape nguvu ya kuendelea mbele hata katika mazingira yao magumu.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 30, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Amen!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Na iwe kama ulivyoomba!
  Lakini ni wazi kwamba kuna uzembe mkubwa sana mahali!
  Kuna watu wanataka wajulikane kwamba wao ndo wao, na bila wao, hakuna linalowezekana!
  Anyway, siku zao zinahesabika!
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Siwaelewi wahasibu wa sector mbalimbali a serikali, hawa haswa ndio wenye shida kubwa! wanapenda kuonekana miungu watu, na ukiwaambia ukweli tu basi ni visa mtindo mmoja. unaweza kukaa miezi miwili huna mshahara, unaambiwa kuna tatizo hazina, sijui jia lako limekosewa wakati wa kulipeleka hazina.

  lakini hilo ni moja tu, maboss wa hawa wahasibu nao hawafanyi chochote kuhakikisha wanawawajibisha. Na wahasibu wanafahamu hilo.

  Hivi huu ndo utendaji utakaolipeleka taifa letu kule tutakapo?
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Jul 30, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Jamani ina maana hamjanote tu mbona karibia kila July huwa ni hivi? Si ndo mwisho sijui mwanzo wa mwaka wa fedha? huwa kuna mahesabu yao wanafanyaga (wajuzi watujuze).

  Kosa huwa hawatutaarifu ili watu tujipange vizuri
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Poleni sana
   
 7. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe unajiweka wapi, maana mfanyakazi akipata mshahara ndipo na mfanyabiashra anapata wateja, au wewe fisadi?
   
 8. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,263
  Likes Received: 4,237
  Trophy Points: 280
  Kila mwaka mwezi wa 7 wafanyakazi wa serikali mshahara huchelewa kutoka
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Kwanini?

  Bajeti ya Mshahara ya Wafanyakazi wa Serikali hupangwa hadi Juni? Au kuna jambo gani linalosababisha hii hali?

  Wanaofahamu tafadhali (MwanaJ1) tunaomba sababu ya hii "trend"
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Belo,

  Hiyo "Avanta" vipi? Tevez keshahamia Man City. Au na wewe umebadilisha TIMU?
   
 11. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuna marekebisho hufanywa kwenye mishahara ya wafanyakazi wa serikali kila mwezi wa saba. Kwa kuwa ndio mwaka mpya wa fedha wafanyakazi huongezewa ngazi ndogo ya mshahara mfano toka TGA D1 kwenda TGS D2 na ndio maana mishahara inachelewa kwa ajili ya marekebisho hayo
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hakika mimi nilisha ondoka huko Tanzania nipo ughaibuni ndio maana nawapa pole wenzangu.
   
 13. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,437
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu matatizo hayakimbiwi, yanafanyiwa kazi!!! kaka, dada, wadogo zako n.k. bado watapata tabu hii tunayopata sisi..
   
 14. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wafanyakazi wa serikali si wanadai wao hawatumii mishahara wanakula poshos tu? au waongo? au ni wachache tuu?
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jamani mishahara huchelewa mwezi huu ni kwa sababu ya transition toka mwaka mmoja wa fedha kwenda mwingine.Ingawa kuna uzembe nao huwa unachangia kama wa kuongeza siku bze mishahara si inajulikana.
  Unaweza kuta signatories wako bado Dodoma still wanajipongeza!!Hi ndio Tz bwana no hurry kabsaaa ukiwa na haraka nenda ulaya.
  Businessmen wanalalamika mzunguko wa fedha umepwaya!!!!!!!!
   
 16. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,638
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Hivi mshahara ukitolewa tarehe 23 hadi 23 mwezi ufuatao, NA ukitolewa tarehe 30 hadi 30 mwezi ufuatao, interval si inabaki ile ile ya mwezi mmoja? Wakati mwingine hizo ni kauli za kisiasa tu kuwapumbaza watu kwamba Serikali inawajali watumishi wake kwa kutoa mishahara mapema, wakati suala la msingi si kuwahi kutoa, bali kuongeza mishahara, kupunguza makato na kudhibiti mfumuko wa bei za bidhaa ili hela wanayoipata ifanye mambo makubwa yanayoonekana dhahiri.
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Limbani,

  Sijakimbia matatizo bali nimarudi kwenye asli yangu.
   
 18. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,638
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Mbona juzi tu ulikuwa unaripoti live matukio ya sherehe za Mwaka Kogwa huko Zanzibar ?
   
 19. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  wapo kweli wale wanaokula posho, tena posho inakuwa maradufu kwa mshahara. Hata mishahara yao kweli baadhi hawatumii. Ila kumbuka kuna wale wanaosubiri mshahara mwezi hadi mwezi ndio wapate kula yao na mahitaji mengine hao posho hawana. Hivyo ni wachache tu wapatao posho.
   
 20. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  .

  Labda ubainishe nilikuwa na ripoti wapi matukio hayo ya mwaka kogwa?
   
Loading...