Mai Mai, kuna issue mbili hapo.
1. Wageni kulipwa kuliko wenyeji-Hii ni kweli na ndivyo ilivyo duniani kote, hata hapa nyumbani, Watanzania wote wanaofanya kazi balozi mbalimbali, hulipwa chini kuliko wazungu hata kama mko ngazi moja, hii ni justified kutokana na huyu mgeni kuishi kwa gharama kubwa zaidi kuliko mwenyeji. Hata sisi Watanzania wenyewe, wale wanaofanya decent jobs nchi za watu kama experts, wanalipwa vizuri kuliko wenyeji.
Nenda kwenye balozi zetu, utakuta Watanzania wanaofanya kazi huko kama diplomat wanalipwa vizuri kuliko wenyeji, na kuza kazi ambazo tunatakiwa kuwaajiri wenyeji kwenye balozi zetu, lakini kutokana na dhiki zetu, tumewaajiri Watanzania kama locals, wao nao wanalipwa mishahara ya wenyeji ambayo ni midogo kuliko wenzao diplomats.
2. Watanzania tuna tatizo la bargaing power ya mishahara, kuna dada Mtanzania, alitafuta kazi mahali nas kuitwa kwenye interview, kumbe pia kuna mkenya aliitwa. Huyo dada ni freshh graduate wa UD na Mkenya ni diploma holder wa cho fulani cha uchochoroni tu kule Nairobi.
Kwa vile nilikuwa na inside information ya package ya hiyo kazi, nikamuuliza yule dada Mtanzania, what is your expectation ya salary, akajijibu, kwa vile ndio nimemaliza chuo na sijawahi kuajiriwa, I just need a job na niko tayari kufanya kwa any salary. Nikamuuliza tena, mshahara wa kiasi gani utakutosha mahitaji yako yote?, alijibu hata laki 5 (500,000), na kusema kwa vile yeye ni mtoto wa kike, hivyo anaishi na wazazi wake, hivyo zitamtosha kabisa. Nikampa inside information kuwa package ya hiyo kazi ni kati ya 1.2 mpaka 2.4. Hivyo nikamwambia wakukuuliza mshahara wewe waambie around 2.M alafu nga'ang'ania hapo usishuke. Hyo dada akashtuka na kusema si nitakosa kazi kwa kuonekana nina tamaa!, nikamhakikishia ndivyo wanavyolipa kwa posti anayoomba, akazidi kuogopa kupanda dau.
Siku ya interview ilipofika, nimekaa kwenye panel, yulele dada na digrii yake ya UD hakuonyesha confidence kabisa na nilichoka ilipofika kubargain mshahara, akasita sita na kusema hata 1.m itantosha!. Mkenya kaja na macofidence ya ajabu, kwenye mshahara akatakaUS $ 2,000!. Mwisho wa siku, wote wawili wakaajiriwa, yule dada akilipwa 1.4, akafurahi sana kwa vile ni more than her expectations, Mkenya analipwa 2.4!, na they are doing the same job!.
Sasa nilipomuuliza kwa nini alishuka, akasema aliogopa kutaka hela nyingi!, nikamwambia kwa taarifa yako, mwenzako analipwa 2.4!.
Hivi ndivyo Watanzania tulivyo when it comes to salary bargain!.