Mishahara Mwezi Agosti

Mishahara Mwezi Agosti

Mpatanishi

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2011
Posts
1,811
Reaction score
623
Katika hali isiyoeleweka mpaka sasa mishahara haijatoka. hususani kwa kada ya ualimu kwa manispaa zote tatu hapa Dar Es Salaam na kwa hili nadhani hata mikoani hali ni hii hii.

Hii serikali mbona haieleweki iweje mishahara isitoke na hakuna maelezo yoyote, wahusika wapo kimya.
 
Nashauri serikali itafute mwekezaji kwenye mishahara ya watumishi wake ili kujipunguzia majukumu.
Wakileta mwekezaji,mishahara kwa muda mwafaka maana sasa serikali yetu tukufu inasumbuka sana.
 
Mhe Mwigulu Nchemba A.k .a Jemba raia wako wanataka kufahamu wataishi vp?! Msharaha bado hawajapata hadi Leo?! Hivi kweli ufanisi utakuwepo??! Huu si ndio mwanzo wa rushwa?! Viongozi wetu kuweni serious
 
Huku kwetu tumepata tangu tarehe 28, mwezi huu.....Ila kuna baadhi ya watumishi hawajapata kutokana na matatizo mbalimbali
Poleni sana.
 
Katika hali isiyoeleweka mpaka sasa mishahara haijatoka. hususani kwa kada ya ualimu kwa manispaa zote tatu hapa Dar Es Salaam na kwa hili nadhani hata mikoani hali ni hii hii.

Hii serikali mbona haieleweki iweje mishahara isitoke na hakuna maelezo yoyote wahusika wapo kimya.
Wapo bize na bunge la posho
 
Huku kwetu tumepata tangu tarehe 28, mwezi huu.....Ila kuna baadhi ya watumishi hawajapata kutokana na matatizo mbalimbali
Poleni sana.

dah kaka upo mkoa gani wewe? Dar hakuna kitu
 
Acheni porojo zenu,mishahara imeshalipwa zamani sana.
 
kabisa kaka, sijawah kusikia wabunge wakilalamika kucheleweshewa malipo yao iweje sisi tu ndio wahanga wa hizh blah blah za serikali
Aulizwe Naibu waziri wa Hazina, Mwigulu Nchemba, kuwa pamoja na yeye kutahadharisha kuwa, kuendelea na bunge la katiba ni matumizi mabaya kabisa ya pesa za walipa kodi.

Sasa imekuwaje pamoja na kutamka hivyo, Hazina wanaendelea kuwapelekea posho wabunge la bunge la katiba na walimu, wanaachwa 'wafe' njaa, kutokana na kukosa mishahara yao?
 
Acheni porojo zenu,mishahara imeshalipwa zamani sana.

wewe utakuwa mjumbe wa bunge la katiba tu kwani naona huu uzi umekuudhi sana...mishahara hadi leo tarehe 31/08/2012 haijalipwa labda wew unayelipwa sh.laki 3 kwa siku ndo maana unasema ni porojo.Kwa kweli inasikitisha hakuna kiongozi yeyote ambaye ametolea ufafanuzi juu ya mishahara ya mwezi augosti.
 
Acheni porojo zenu,mishahara imeshalipwa zamani sana.

wewe ndo uache masihara kwenye hoja za msingi zinazogusa maisha ya watu. Mleta hoja limemgusa ndo maana kauliza.
Na ni kweli mishahara haijatoka kwani nami ni mhanga. Naona kuna shida mahali na nahisi wamefilisika na hawakopesheki tena na mabenki ya ndani pia nssf, ppf na pspf yameishiwa. Ipo siku tutakaa miezi 6 kama jamaa zetu wa kongo. Hebu mwenye taarifa za kina atujuze.
 
Wala vumbi mnatia huruma!

kuwa mstaarabu hasa unapochangia hoja zinazogusa maisha ya watu. Unamaanisha nini kusema wala vumbi. Bila wao hata hizo keypads usingezijua. Dharau zako zinaonyesha jinsi ambavyo hukuelimika japo ulowait wala vumbi kujitolea kwa uwezo wao wote kukuelimisha. Si makosa yako lakini. Utakuwa umevimbiwa hizo posho za bmk au wewe ni wa mtaa wa lumumba. Maamuma wewe!
 
Back
Top Bottom