Mishahara mipya serikalini 2013

Mishahara mipya serikalini 2013

Naomba utuwekee na wale wanaotumia scale za PUTs na PHTs.

Asante

Nahisi kwa upande wa PUTs kuna maumivu makali upande wa PAYE.

Serikali imefanya ujanja sana kwa kuwaandikia basic salary kubwa lakini ikawanyima marupurupu na wakati huohuo kuwawekea PAYE kwa kiwango kikubwa.

Tusubiri wenye detail tuone mazingaombwe.
 
Mbona TGTS ambayo ni scale ya walimu cjaiona?
 
Kumbe nimepata sababu kwanini rushwa imekita mizizi na waalimu wanagoma kufundisha kama kweli maisha haya unampa mtumishi wako kima cha chini 240,000/= hatari sana, exploitation+oppression.
 
Kwa nchi masikini kama Tanzania,viwango sio vibaya sana,tatizo kubwa ni inflation na kukosekana kwa huduma za msingi ambazo mwananchi wa kawaida anabidi azi-supliment.Mishahara inavyozidi kupanda ndio gharama za maisha zinapanda.ingekuwa poa mtu anayelipwa 240,000 angeweza kusave japo 10,000 kwa mwezi,bahati mbaya sio hivyo.wengi wana deficit month in month out.
 
Yapo mambo mengi yanayochangia kujenga madaraja ya wenyenacho na wasionacho katika jamii. Miongoni mwa mambo hayo ni mishahara.

Tuitake serikali itoe maelezo kwanini imependelea wanasheria?

Kwa sababu wanasheria wameweza kujenga hoja
 
Hivi kima cha chini cha Tsh 240,000/= kinatosha kugharamia chakula,chumba,maji,umeme,matibabu,simu na mavazi kwa mwezi?

Mtu anayeishi maisha ya kima cha chini inamtosha ila akitaka kuishi kama Wema Sepetu haitoshi...
 
Huku upande wa pili tukiona pesa inashuka thaman na ongezeko la kodi kwa kasi kubwa sana
 
Incredible! Je kuna mtu anayeweza kutupa takwimu sahihi za idadi kamili ya watumishi wa serikali kwa sasa? Serikali kuu imeajiri wangapi? Serikali za Mitaa wangapi?
 
Kwa kima cha chini cha mshahara wa mtumishi 240,000 ataacha kuiba kweli? Hivi wao wakipewa laki mbili tu si inaisha kwa dakika? Rushwa itaisha wapi? Bado ni kichekesho kingine hiki. Take it easy Serikali.
 
Mkuu,,
Ongeza kununua nani kwa mwezi 30,000,fungu ila kimi .70,000 saluni 20,000 etc...
 
Mtu anayeishi maisha ya kima cha chini inamtosha ila akitaka kuishi kama Wema Sepetu haitoshi...

Mkuu kama wewe umebahatika kuwa na kipato kikubwa, acha kabisa kutukana watu wakipato cha chini.Haya uliyosema ni matusi. Na kama uko kwenye ngazi ya uongozi basi hii ni hatari mkubwa.
 
Mkuu kama wewe umebahatika kuwa na kipato kikubwa, acha kabisa kutukana watu wakipato cha chini.Haya uliyosema ni matusi. Na kama uko kwenye ngazi ya uongozi basi hii ni hatari mkubwa.

Exactly ukiishi maisha ya kawaida utaweza kujimudu kimaisha
 
Exactly ukiishi maisha ya kawaida utaweza kujimudu kimaisha

Mkuu, ni maisha ya kawaida kwa familia kushindia mlo mmoja? Ni maisha ya kawaida kutokumudu gharama za matibabu kwa fammilia? Ni maisha ya kwaida kutwanga kwa miguu kwenda kazini na safari zingine kwa kushindwa kumudu gharama za dalai dala? Ni maisha ya kawaida kuto kuishi kwenye nyumba inayofaa kuishi binadamu kwa kutoweza kumudu gharama za pango? Ndio maana nasema acheni matusi kwa watu wa kipato cha chini. Mbunge au waziri anapo kuwa safarini kwa siku analipwa shs ngapi? Fananisha na kima cha vhini kwa mwezi.
 
Back
Top Bottom