Misemo ya wahenga na uhalisi wake

Misemo ya wahenga na uhalisi wake

Limbukeni

Senior Member
Joined
Feb 27, 2009
Posts
117
Reaction score
1
Utamaduni wetu umekuzwa kwa aina ya misemo mingi yenye malengo kama ifuatavyo.

Kutiana moyo.
Haba na haba hujaza kibaba,

maonyo
haraka haraka haina baraka , asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu

matumaini
mpanda ngazi hushuka

masharti
mtaka cha uvunguni sharti ainame

ubinafsi
mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu---- na mingine mingi

ukiachia ardhi urithi huu nisemo hauna gharama yeyote au uchoyo kuupata.. Je misemo ya aina hiyo ina uhusiano wowote na uhalisi wa maisha ? Kuifata au kutoifuta kuna uhusiano wowote wa mafanikio au maanguko katika maisha?
 
ukiachia ardhi urithi huu nisemo hauna gharama yeyote au uchoyo kuupata.. Je misemo ya aina hiyo ina uhusiano wowote na uhalisi wa maisha ? Kuifata au kutoifuta kuna uhusiano wowote wa mafanikio au maanguko katika maisha?

Kwa maoni yangu misemo hii bado ina uhusiano mkubwa tu na maisha ya sasa. Misemo hii inatokana na uzoefu katika maisha.Cha muhimu ni kutumia busara katika kupokea maarifa yatokanayo na misemo hiyo.
 
Misemo hii, ukiichukulia kama misemo inaweza kuwa haina uhalisi, ila ukijua wapi pa kuitumia uhalisi wake huibuka.

Kwa mfano unaweza kukuta misemo miwili inayopingana kama

Haraka haraka haina baraka
na
Ngoja ngoja huumiza matumbo

Sasa huwezi kusema misemo hii iko absolute, ila, sehemu ambapo unatakiwa kuasa dhidi ya papara na kukosa simile utatumia "Haraka haraka haina baraka" sehemu ambapo mambo yanaenda pole pole sana na unataka kuhimiza haraka utasema "Ngoja ngoja huumiza matumbo"

Uzuri wa misemo hii ni kwamba ime cover angles nyingi, ubaya wake ni kwamba haiko absolute na kama hujui kuitumia unaweza kuitumia vibaya, kwenye sehemu inayotaka simile unaweza kujifariji kwa kusema "Ngoja ngoja huumiza matumbo" kumbe ndiyo unajiingiza katika ajali.
 
actual misemo mingi inakua ni life experience,na maisha ni ya marudio tofauti iko kwenye vitu vidogo sana, hivyo ni muhimu ujue jinsi gani ya kuleta hali ya zamani katika maisha ya sasa, ni mizuri katika kujenga good life
 
Matumizi sahihi ya misemo kwenye mazingira yake ndiyo jambo muhimu.

Siyo misemo ya wahenga tu inayotaka matumizi mazuri ya mazingira, mfano;....baba amesafiri huku nyuma majambazi wakavamia nyumba yake, mtoto mmoja anajua baba yake anaweka wapi bunduki hivyo akaichukua na kufanikiwa kuwatimua majambazi yale! hapa bunduki ni nzuri sana na konyesha wapi unificha kwa watoto ni jambo jema pia. Lakini baba kasafiri mtoto huyo huyo kachukua bunduki akua jirani wanaegombea girl friend!!.... Hapa tena kitu kilekile kinageuka na kuwa kibaya sana!

Mwisho kabisa ni hivi,..KILAKITU DUNIANI KINA PANDE MBILI. Ubaya na uzuri!
 
LIMBUKENI, ameibua fikra muhimu sana kwa nyakati zetu.
Misemo mingi sasa haitiliwi sana maanani, kwa kile watu wa kizazi kipya wanachodai kwenda na wakati.

Nakuabaliana na wachangiaji waliotangulia kwamba misemo kama hiyo, ni sehemu ya uzoefu wa maisha,

Kadhalika, misemo kama hiyo., huwa ni njia rahisi na nyepesi sana ya kuwakilisha ujumbe kwa jamii.

Ya kale, ni dhahabu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom