Misemo ya kiswahili inayo viza maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misemo ya kiswahili inayo viza maendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MVUMBUZI, Jun 11, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hali ya umaskini tuliyo nayo imechangiwa kwa kiasi fulani na utamaduni wetu wa kiswahili haswa kutokana na kuwepo kwa misemo mingi inayochochea uzembe kuliko kujibidisha. Baadhi ya misemo ya Kiswahili zikiwepo methali zina maudhui hasi ambayo yamewafanya watu wengi kuridhika au ku maintain status quo kuliko kutafuta upenyo wa tatizo alilo nalo. Kwa mfano; Mithali zifuatazo:

  1."Kulenga siyo kufuma"
  2."Mipango siyo Matumizi"
  3."Kutangulia siyo kufika"
  4."Mpanda ngazi hushuka"
  5."Polepole ndio mwendo"
  6."Harakaharaka haina baraka"[/B]

  Misemo 1na 2 ina mkatisha tamaa mtu kupanga au kujiwekea malengo kwa sababu utekelezaji wake siyo lazima uwe kama ulivyopanga au sawasaw na shabaha yako. Kwa maaana nyingine kupanga na kutopanga haina tofauti.
  Hiii misemo kwa ufupi ina viza fikra za watu kuwa eti hutakiwi uwe na haraka wala kutangulia na kwamba eti kwenda taratibu basi ndiyo mwendo muafaka.

  Wenzetu wa magharibi wangezaliwa katika mazingira ya utamaduni kama huu wasingegundua magari wala ndege kwani polepole ndio mwendo na haraka haraka haina baraka. Pia wasingekuwa na utaratibu wa kuweka mipango na malengo ya baadaye kwani kulenga siyo kufuma na mipango siyo matumizi.

  Kwa mtazamo wangu misemo hii ya waswahili imewafanya wenye utamaduni huu kuridhika na kile anachopata bila kujishughulisha sana na ukimwuuliza kwa nini hutaki kujishughulisha anaanza kukukebehi na vimafumbo, mithali na nahau za kiswahili" Mtakuja, mtaondoka na mtatuacha hivihivi!!!!!!!!!!
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,367
  Likes Received: 22,230
  Trophy Points: 280
  umebananga
   
 3. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0

  kabananga nin?
  msaidie kumwelewesha il nxt tym ajichek fresh.....
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  buji huu msamiati mpya au?
   
Loading...