Misemo maridhawa ya kiswahili

Machepele

JF-Expert Member
Jun 28, 2019
295
438
Tuambie msemo/msemo ya kiswahili ambayo inafikirisha na inaacha maswali.
Naanza.

1. Siku moja babu yangu aliniambia "Mjukuu wangu machepele, Kile nikionacho mimi nikiwa nimekaa wewe hata ukisimama huwezi kukiona" msemo huu kwangu kwa wakati huo ulivuka upeo wa fikra zangu, lakini sasa naelewa alichomaanisha.

2. Mwanamke hana kifua

Endelea...
 
Huyu hapa Chinua Achebe kwenye kitabu chake cha
Things Fall Apart anasema

"Where are the young suckers that will grow when the old banana tree dies"

Huyu Chinua kwa nini anauliza?, tuchambue sentensi

"Iko wapi migomba chipukizi itakayoota baada ya migomba ya zamani kufa?" Nimejitahidi kuandika kiswahili chepesi ili tuelewe maana ya msemo huu maridhawa.

Kimsingi swali la Chinua, alikuwa anauliza wako wapi wataalam watakao saidia taifa pale wataalamu waliopo watakapo ondoka?, aidha kwa umauti, kustaafu, kufungwa, kubadili imani yako nakadharika.

Anauliza Chinua, wako wapi viongozi watakaofuata baada ya viongozi waliopo kuondoka katika nafasi zao, kwa vyovyote vile vifo, magonjwa, umri na hali nyingine zitakapo amua kuwaweka pembeni?

Anauza kuhusu madaktari, wandishi wa habari, wanasheria, watu wema, wanasiasa, wazazi, viongozi, nk..

Nyakati anaandika huyu Chinua Uchebe maneno haya ni imani yangu zilikuwa zama za akina Keneth Kahunda, Nkwame Nkuruma, Julius Nyerere, Jomo Kenyatta, Nelson Mandera, Thomas Sankara, Patrick Lumumba, nk...

Nauliza leo mimi machepele wa Tanzania.
"Iko wapi migomba chipukizi itakayoota baada ya migomba ya zamani kufa?"
 
Hivi ni Achebe au Uchebe?Corn-fused,you know?
 
Tuambie msemo/msemo ya kiswahili ambayo inafikirisha na inaacha maswali.
Naanza.

1. Siku moja babu yangu aliniambia "Mjukuu wangu machepele, Kile nikionacho mimi nikiwa nimekaa wewe hata ukisimama huwezi kukiona" msemo huu kwangu kwa wakati huo ulivuka upeo wa fikra zangu, lakini sasa naelewa alichomaanisha.

2. Mwanamke hana kifua

Endelea...
Hii siyo misemo ya kiswahili bali ya mitaani na inaweza kuwa inadhalilisha au haina maana! Misemo ya kiswahili ni ile inayojulikana na wengi, yenye busara, tumeipokea kutoka vizazi vilivyopita. Misemo kama ''mgaagaa na upwa hali wali mkavu''.
 
Tuambie msemo/msemo ya kiswahili ambayo inafikirisha na inaacha maswali.
Naanza.

1. Siku moja babu yangu aliniambia "Mjukuu wangu machepele, Kile nikionacho mimi nikiwa nimekaa wewe hata ukisimama huwezi kukiona" msemo huu kwangu kwa wakati huo ulivuka upeo wa fikra zangu, lakini sasa naelewa alichomaanisha.

2. Mwanamke hana kifua

Endelea...
Jua lililo Waka wakati Babu yako ana zaliwa, ndilo jua litakalo Waka wakati mjukuu wako wa mwisho ana kufa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom