Misamiati mipya ya Kiswahili sanifu

Kuperemba-kusimamia, fuatilia hotuba ya bajeti mkulo:serikali itaperemba mashirika yote yaliyobinafsishwa kujua ubora wake. Sasa kama ni kutongoza haitaleta maana..

Mkuu, Kuna baadhi ya maneno ya Kiswahili yana maana zaidi ya moja, mfano
kaa, paa,mbuzi, koroma,kina, kima..........Hivyo si ajabu hata neno peremba.
 
Kuna haja ya kujulkishana misamiati mipya ya lugha yetu adhimu. Kila siku lugja yetu inakua na misamiati inaongezeka kila siku.
Hapa kuna baadhi ya misamiati, pia naomba ndugu zangu muongezee baadhi ya maneno ya Kiswahili sanifu.
Tafrija mchapalo ni cocktail party.
Kanguvuke ni jenereta
Rununu ni simu ya mkononi
Weledi ni profesionalism
baobonya ni keyboard
Puku ni mouse.
Ngamizi ni kompyuta
.wavuti ni internet
tovuti ni website
Kichakata matini ni word processor
Runinga ni television.
Naomba tuongezee misamiati mingine


Dah!Asante sana mkuu kwa kutukumbusha umuhimu wa lugha yetu.
Ila nisidanganye,kwa staili hii nahisi sikijui kiswahili kama nilivyodhani,asante kwa changamoto.
 
Jamani Bujibuji hatusemi misamiati, neno sahihi na sanifu ni msamiati iwe katika wingi ama umoja.
 
kwa mtazamo wangu-wale wazee wanaotunga misamiati mipya-wanakosea sana-waache maneno yatumike kama yalivyo-mbona wachina wana simplified chinese,standard chinese na traditional chinese-na sisi pia tungeacha tuwe na simplified swahili ambayo itakuwa na mchanganyiko wa maneno ya kiingereza kama password,compyuta n.k, kuliko kulazimisha maneno mapya kama BAOBONYE n.k-bora iwe inajulikana kuwa Tanganyika wanazungumza simplified swahili-na zanzibar na mombasa wanazungumza traditional swahili-kuliko kutaka kubadili kila neno-hii inafanya sisi waswahili wenyewe kushindwa kuijua lugha yetu
 
Ndugu Katavi,
Salaam. Nimekupigia rununu yako bila majibu. Nilitaka nikufahamishe hitimisho la sakata ya kanguvuke ya Dowans kama ilivyojadiliwa bungeni.
Suala limejadili bila weledi na hii inanipa kihoro kuhusu hatima ya mgao wa umeme. Kwa mintaarafu ya yaliyojiri imebidi iundwe kamati ndogo ya kamati ya madini ili kuanzisha taftishi, na haiyumkiniki kuwa muktadha wa jambo hili utakuwa katika siku za usoni.

Nimeona katika runinga aina mpya ya ngamizi zenye baobonye ambazo puku zake hazitumii waya. Nimepewa dokezo kuwa kinakishi na nukushi vinapatikana kisutu madukani mkabala na jengo la mfuko wa jamii. Jaribu kutembelea wavuti ya JF ili kubaini uwezo wa kichaka matini yake kabla hujaagiza.

Usisahau kumwambia bujibuji ujumbe wake murua nimeupata. Ukiweza kumtia machoni Dena Amsi muulize kulikoni? ni muda sijasikia kutoka kwake. Vipi unategmea kuhudhuri kongamano aliloaanda Lizzy, mimi nitakuwa na warsha na nadhani AD, Hapanuchi nao watajumuika nami.

Tadhali usomapo ujumbe huu naomba usuli. Wajulie hali akina invisible, malaria sugu na Masanilo. Nasikia hamkani si shwari kwao walipata ban je ni kweli. Nasikia pia MMU wanaomba uanisho mtu anapofungiwa, je mchakato wa suala hilo umeshamfikia Melo.

Maslaam

Kaka Nguruvi.

hyseee! Nimekubali we mkali.
 
computer - tarakilishi
ict - teknohama (teknolojia ya habari na mawasiliano)
frequency - kasimawimbi
scratch card - kadihela
software - maunzi
screen - kiwambo
cpu - kku (kitengo kikuu cha uchakataji)
 
Nyie naona karibuni mtaanza kuandika hata matusi, eti ni misamiati mipya ya kiswahili. Shauri yenu!
 
ni BaoBonye si BaoBonya kwa Kizungu KeyBoard. ni sehemu mojawapo ya Tehama
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom