Misamiati mipya ya Kiswahili sanifu

Sasa hapo nd'o umeanza kazi! Asante sana kwa mchango wako! Kwangu mimi mwandishi wa habari, nahitaji sana kujua misamiati mipya ya Kiswali kila inapochipuka! Siju nichangie lau neneo moja?
  • Microwave ni wimbi mikro
  • Laptop ni kompyuta ya kupakata
  • Calculator ni kikokotoo
  • Air conditioner (AC) ni Kiyoyozi
Ntarejea baadaye na misamiati mingine.
 
chukua hii..kirefu cha www kwa kiswahili sanifu ni wavuti wa wasiliani.lugha hii adhimu sana
 
Kuperemba ni kubembeleza/kushawishi pia ni neno liliokuwa linatumiwa na kuleta maana ya kutongoza..sasa sanifu ya kuperembwa kuwa "monitor"naona si sahihi..tufafanulie zaidi sanifu hii.

Ratibu= coordinate
 
da itabidi nirudi cilos kusoma kiswahili..mfano: Rununu yako ya nokia ina salio.
 
kibechuo- ni kijiti cha kutolea uchafu kwenye meno(stik)
kipanya- ni mouse (ktk kompyuta)
 
Kuperemba ni kubembeleza/kushawishi pia ni neno liliokuwa linatumiwa na kuleta maana ya kutongoza..sasa sanifu ya kuperembwa kuwa "monitor"naona si sahihi..tufafanulie zaidi sanifu hii.Ratibu= coordinate
Kuperemba-kusimamia, fuatilia hotuba ya bajeti mkulo:serikali itaperemba mashirika yote yaliyobinafsishwa kujua ubora wake. Sasa kama ni kutongoza haitaleta maana..
 
Ndugu Katavi,
Salaam. Nimekupigia rununu yako bila majibu. Nilitaka nikufahamishe hitimisho la sakata ya kanguvuke ya Dowans kama ilivyojadiliwa bungeni.
Suala limejadili bila weledi na hii inanipa kihoro kuhusu hatima ya mgao wa umeme. Kwa mintaarafu ya yaliyojiri imebidi iundwe kamati ndogo ya kamati ya madini ili kuanzisha taftishi, na haiyumkiniki kuwa muktadha wa jambo hili utakuwa katika siku za usoni.

Nimeona katika runinga aina mpya ya ngamizi zenye baobonye ambazo puku zake hazitumii waya. Nimepewa dokezo kuwa kinakishi na nukushi vinapatikana kisutu madukani mkabala na jengo la mfuko wa jamii. Jaribu kutembelea wavuti ya JF ili kubaini uwezo wa kichaka matini yake kabla hujaagiza.

Usisahau kumwambia bujibuji ujumbe wake murua nimeupata. Ukiweza kumtia machoni Dena Amsi muulize kulikoni? ni muda sijasikia kutoka kwake. Vipi unategmea kuhudhuri kongamano aliloaanda Lizzy, mimi nitakuwa na warsha na nadhani AD, Hapanuchi nao watajumuika nami.

Tadhali usomapo ujumbe huu naomba usuli. Wajulie hali akina invisible, malaria sugu na Masanilo. Nasikia hamkani si shwari kwao walipata ban je ni kweli. Nasikia pia MMU wanaomba uanisho mtu anapofungiwa, je mchakato wa suala hilo umeshamfikia Melo.

Maslaam

Kaka Nguruvi.
 
Back
Top Bottom