Misamiati kwelikweli!

middo lulyheart

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
260
98
Habari wana JF!

Nimerudi kwa mara nyingine mwenzangu kuhitaji tafsiri hizi,
-HAGGLE
-SLUMP
-PAMPA
-HUMPER
-TEMPER
-ABIDE

Shukrani za dhati kwenu!
 
Haggle => Kubishana kwa ajili ya bei ya bidhaa
I know they will haggle over the price of tomatoes. => Najua watabishana kwa ajili ya bei ya nyanya.

Slump => Kushuka kwa ghafla
I am worried that the Microsoft stock will slump. => Nina wasiwasi kwamba hisa ya Microsoft itashuka bei.
If he falls asleep he will slump over in his chair. => Akilala atainama chini kitini kwake.

Pampa => Wanda wa bara la Marekani kusini. Neno hili latumika nadra sana. Labda unamaanisha "pamper"?
I travelled for three days to cross one pampa of Argentina. => Nilisafiri kwa siku tatu nivuke wanda mmoja wa Argentina.

Humper => Bible Humper ni mtu ajaribuye kukulazimisha kuwa Mkristo. Matumizi tofauti ya "humper" ni lugha mbaya ya mitaa.
That Bible humper tried to force me to be baptized. => Huyu mhubiri mwenye nguvu alijaribu kunilazimisha kubatizwa.

Temper => Tabia (nomino) au kupunguza (kitenzi)
(nomino) I lost my temper when he stole my bicycle. => Nilihamaki alipoiba baisikeli yangu.
He can't control his temper. => Hawezi kudhibiti tabia yake mbaya.
(kitenzi) You should temper your anger before speaking to your mother. => Uipunguze hasira yako kabla ya hujasemea mama yako.

Abide => Kuzingatia au kufuata
If you abide by the rules you will be benefitted. => Ukifuata masharti utanufaika.

Baadhi ya haya ni maneno magumu. Labda fafanuzi zangu za Kiswahili ni mbaya, lakini mifano ya Kiingereza ni mizuri.
 
Hongera ya hapo juu, beretta!

Juu ya ‘abide' yapo maana nyingine pia:

‘can't abide' = kutokupenda; kuchukia; kutokuvumilia

I can't abide tea without sugar. = Sipendi chai bila sukari.

‘abide' = kukaa; kuishi (ni maana ya zamani lakini bado watu wanaitumia)

He abides alone in the bush. = Anakaa peke yake msituni.
 
Back
Top Bottom