Misamaha anayoombwa Rais Magufuli na wale wanaokiri kuwa wamemkosea ina walakini

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,156
Nimemsikikiza kwa makini Mwanasiasa mkongwe hapa nchini, Abdrahman Kinana, kwa taarifa yake aliyotoa kwa Umma kwa kile alichokiita mwenyewe kuwa anaomba msamaha kwa Rais Magufuli kwa yale maneno yaliyonaswa kwenye video clip, ambayo anaamini yalimkera Mheshimiwa Rais

Nimemsikiliza pia Mheshimiwa huyo Abdrahman Kinana akilalamika kuwa kiukweli alipotamka maneno hayo, alikerekwa, alihuzunika na alikasirishwa sana.

Hakufafanua kuwa ni nini kilichomfanya Mheshimiwa Kinana, akerekwe, ahuzunike na akasirishwe sana na kama vitu hivyo vilivyomkasirisha wakati huo, vimekuwa "solved" kwa wakati huu

Hata hivyo anamalizia kwa kusema kuwa baada ya kufikiria kwa muda mrefu, anadhani ni muda muafaka kwake kumwomba msamaha Rais Magufuli, kwa kitendo alichokitenda ambacho anaamini kilimuudhi Mheshimiwa Rais na kwa kuwa yeye ni muungwana amelazimika kuchukua hatua hiyo ya kumwomba radhi Mheshimiwa Rais.

Hebu tutafakari kwa kina chanzo cha sakata hili zima la hao wazee wastaafu hadi kupelekea wawekwe kitimoto na kujadiliwa kwenye kikao cha juiu kabisa cha chama chao, kikao cha Kamati Kuu ya CCM

Mzozo wote huu chanzo chake ni kutokana na mtu mmoja anayeitwa Crispin Musiba kutoa tuhuma nzito zisizo na ushahidi na ambazo Wazee hao wastaafu waliona kuwa zimewavunjia heshima ndani ya jamii ya watanzania.

Hatua waliyochukua wazee hao ni kupeleka malalamiko yao kwenye uongozi wa chama chao, ambapo walidhani kuwa wangesikilizwa kwa kuitwa huyo mtu anayeitwa Musiba ili atoe ushahidi kwa yale anayowatuhumu

Bila shaka wote tulishuhudia kile kilichojitokeza baada ya hao wazee kuyafikisha kwenye chombo husika cha maamuzi ndani ya chama chao.

Cha kushangaza ni kuwa hao waliopelekewa malalamiko hayo, waliyaona ya moto sana na hivyo kupata "kigugumizi" kuyajadili na hivyo kuyatupilia mbali!

Swali tunalojiuliza ni nani haswa anayemkingia kifua "kivuruge" huyu Cyprian Musiba, hadi vyombo husika vya maamuzi vya chama, hata na vyombo vya sheria vya mahakama vipate "kigugumizi" kutoweza kumjadili kabisa??

Bila "ku-solve root cause" ya tatizo lenyewe ambaye ni huyu mtu amayeitwa Cyprian Musiba, hii misamaha inayodaiwa inaombwa na wahusika itakuwa kiini macho, na bado moshi utakuwa unaendelea kufukuta chini kwa chini na siku moto huo utakapokuja kulipuka, hakuna wa kuweza kuuzima!

Hebu tujiulize ni nani hasa huyu mtu anayemkingia kifua huyu mtu Cyprian Musiba hadi vyombo vya maamuzi vya chama na vyombo vya sheria vishikwe na "mchecheto" na kutoweza kumjadili kabisa??

Ninachotahadharisha ni kuwa kwa kuwa wastaafu hao wamegundua "weakness" yake Mheshimiwa mkubwa kabisa, basi nadhani wameshauriwa na watu wao wa karibu kuwa "bora liishe" kwa kuomba msamaha na huyo Mheshimiwa mkubwa kabisa atafurahi kwa kuamini ya kwamba yeye ndiye anayegopewa kuliko mtu yeyote hapa nchini!

Tahadhari kubwa ninayoitoa hapa ni kuwa misamaha ya aina hiyo haitoki ndani ya mioyo yao hao watu, Bali ni kukubali tu yaishe ili maisha yaendelee na wabaki kwenye "system"
 
Mkuu umeongea na umekata mpaka kwenye mfupa kwani ni kweli kuomba msamaha ni uungwana kwa waungwana lakini kuomba msamaha kwa kufunika kombe yaani bila Musiba kuchukuliwa hatua kwa utovu wa nidhamu hapo ukweli hakuna anayeomba msamaha wala anayeombwa msamaha
 
Mkuu umeongea na umekata mpaka kwenye mfupa kwani ni kweli kuomba msamaha ni uungwana kwa waungwana lakini kuomba msamaha kwa kufunika kombe yaani bila Musiba kuchukuliwa hatua kwa utovu wa nidhamu hapo ukweli hakuna anayeomba msamaha wala anayeombwa msamaha
👋👋
 
Abdrahman Kinana akilalamika kuwa kiukweli alipotamka maneno hayo, alikerekwa, alihuzunika na alikasirishwa sana.........

Hakufafanua kuwa ni nini kilichomfanya Mheshimiwa Kinana, akerekwe, ahuzunike na akasirishwe sana na kama vitu hivyo vilivyomkasirisha wakati huo, vimekuwa "solved" kwa wakati huu
ni wakati wa uchaguzi... Wakati wa kura ya kula ni lazima wawe wamoja kwanza hata ikibidi kwa kubadili majina ya rangi

Jr
 
Yani mpaka leo unauliza nani anamkingia kifua Musiba?

Musiba na magazeti yake wanalipwa pesa na hazina na TISS.
Yani doto ndio anailipa.
Kinana walikuwa hawajui.

Ila ni vizuri wnyooke kwa sababu huyu chatu walimfuga wao.
Na hata hawa walioko madarakani inabidi wajue kabisa kuwa wakiondoka madarakani na kuiacha hii katiba ya kikoloni lazima nao waje kugeukwa tu
 
Niliwahi kuambiwa na mwalimu wangu kuwa "Wasiwasi ndo akili", sikumuelewa. Mzee wangu akasema Kunguru anaishi maisha marefu "sababu ya woga wake", sikumuamini.

Baada ya tafakuri nikagundua yote mawili yanafanana, isipokuwa suala la Kunguru linahtaji marekebisho kwenye ufafanuzi. Kinachompa Kunguru maisha marefu si woga, Bali ni hulka yake ya kutilia shaka kila kitu hata kivuli chake.

Mzee Kinana si mwoga, lakini ana wasiwasi na hali iliyopo.

WASIWASI NDO AKILI.
 
Alikerwa na Musiba kumchonganisha yeye na bosi wake wa zamani... Kumbuka Musiba ndiye chanzo cha yote haya.. Tunashukuru now chama kimeshamdhibiti asiendelee kueneza sumu ya chuki ya kugombanisha wanachama, hasa wazee wetu ambao wamekitumikia chama kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
 
Abdrahman Kinana akilalamika kuwa kiukweli alipotamka maneno hayo, alikerekwa, alihuzunika na alikasirishwa sana.........

Hakufafanua kuwa ni nini kilichomfanya Mheshimiwa Kinana, akerekwe, ahuzunike na akasirishwe sana na kama vitu hivyo vilivyomkasirisha wakati huo, vimekuwa "solved" kwa wakati huu
ni wakati wa uchaguzi... Wakati wa kura ya kula ni lazima wawe wamoja kwanza hata ikibidi kwa kubadili majina ya rangi

Jr
Mshana Jr
Nimeemini kweli huu ni wakati wa uchaguzi, ndiyo sababu yote haya yanatokea.

Wakiamini kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Lakini wanachosahau hao watu ni kuwa "hawaja-solve root cause" ya sakata zima hili ambaye ni huyu kivuruge Cyprian Musiba
 
Na ule msamaha wa Msigwa kwenda kwa Kinana wenyewe haukuwa na wakakini?
 
Siku ikitokea na Mh. Bernard Membe naye akaomba msamaha kwa maandishi au kwa mdomo ili arudishwe chamani naombeni mnijulishe. Ule msemo wake wa 'bora ufe ukiwa umesimama kuliko uishi ukiwa umepiga magoti' nimeulewa sana.
 
Back
Top Bottom