Misafara ya viongozi wa Serikali ni manyanyaso kwa watumia barabara

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Wakuu niko njiani nasafiri na bus la Shabiby kuelekea Dodoma, tumesimamishwa hapa eneo la ubena kupisha msafara wa kiongozi wa serikali zaidi ya masaa mawili sasa tumesimamishwa.

Je, ni halali watu kusimama hivi barabarani muda mrefu bila huruma kisa mtu mmoja anapita kuelekea Dar? kwa nini viongozi wa serikali wanakuwa hivi wakuu. Kimsingi nimechukia sana.
 
Yaani wakati dunia ikifanya mambo mengi kuokoa muda, sisi huku tunafanya juhudi kubwa ya kupoteza muda kumpisha Mtu Mmoja ambae Hata Madhara Hana . Fikiria vitu vingapi tumepoteza.
 
Huwa inaboa sana hiyo misafara, mtu anaenda safari ndefu kama ya Kigoma bado akifika njiani akikuta msafara anaongezewa saa mbili za kusimama njiani kupisha msafara wa mtu anayeenda hapa na hapo tu sio fair.
 
It is absurdity, kufunga barabara kwa muda mrefu kama huo, wakati hata kiongozi mwenyewe hajaamka. Mi nadhani isizidi nusu SAA na ifungwe tu pale musafara wake unapokaribia. Siyo MTU yuko morogoro nyie mmeshafunga barabara mzima kuanzia Mlandizi Mpaka Morogoro
 
Sitasahau Kuna mwaka tulikamatwa kwa kosa la kuingilia msafara wa mtoto wa rais (Ridhiwan Kikwete).

Kipindi hicho hata ubunge hana.
 
Wakuu niko njiani nasafiri na bus la Shabiby kuelekea Dodoma, tumesimamishwa hapa eneo la ubena kupisha msafara wa kiongozi wa serikali zaidi ya masaa mawili sasa tumesimamishwa.

Je, ni halali watu kusimama hivi barabarani muda mrefu bila huruma kisa mtu mmoja anapita kuelekea Dar? kwa nini viongozi wa serikali wanakuwa hivi wakuu. Kimsingi nimechukia sana.
Kuna watu wanapenda kujipa umuhimu ambao hawana.
 
It is absurdity, kufunga barabara kwa muda mrefu kama huo, wakati hata kiongozi mwenyewe hajaamka. Mi nadhani isizidi nusu SAA na ifungwe tu pale musafara wake unapokaribia. Siyo MTU yuko morogoro nyie mmeshafunga barabara mzima kuanzia Mlandizi Mpaka Morogoro
Kinachosikitisha wanakuzuia wewe ambae inawezekana unaenda kutafuta kodi inayolipia mafuta ya hayo ma VX yao!
 
Subirini bunge la bajeti lijalo watapitisha hela ya kununulia helikopta waache kututesa na foleni🤸🐒🤣
 
Wakuu niko njiani nasafiri na bus la Shabiby kuelekea Dodoma, tumesimamishwa hapa eneo la ubena kupisha msafara wa kiongozi wa serikali zaidi ya masaa mawili sasa tumesimamishwa.

Je, ni halali watu kusimama hivi barabarani muda mrefu bila huruma kisa mtu mmoja anapita kuelekea Dar? kwa nini viongozi wa serikali wanakuwa hivi wakuu. Kimsingi nimechukia sana.
Suala hili pia liwemo kwenye marekebisho ya katiba!
 
Kinachosikitisha wanakuzuia wewe ambae inawezekana unaenda kutafuta kodi inayolipia mafuta ya hayo ma VX yao!
Kama Ulikuwepo Mkuu, Naenda Dodoma Kuangalia mavuno Ya Alizeti na Kuanza Kukamua Mafuta Kwa ajili Ya Kufanya Biashara. Wamenikasilisha Sana Hawa Washenzi
 
Angalia motorcade ya waziri mkuu wa uingereza: magari maatatu tu ukichanganya na lile la polisi.
Mbona alipokuja BUSH na Obama si barabara tu bali hata simu zilizimwa kwa kipindi kirefu tu na hamkulalamika?? Ama kwa sababu huyu ni mweusi mwenzetu?
 
Wakuu niko njiani nasafiri na bus la Shabiby kuelekea Dodoma, tumesimamishwa hapa eneo la ubena kupisha msafara wa kiongozi wa serikali zaidi ya masaa mawili sasa tumesimamishwa.

Je, ni halali watu kusimama hivi barabarani muda mrefu bila huruma kisa mtu mmoja anapita kuelekea Dar? kwa nini viongozi wa serikali wanakuwa hivi wakuu. Kimsingi nimechukia sana.

Hahaha hahahaa😂😂
 
Mbona alipokuja BUSH na Obama si barabara tu bali hata simu zilizimwa kwa kipindi kirefu tu na hamkulalamika?? Ama kwa sababu huyu ni mweusi mwenzetu?
Hivi wewe unajua kuwa ikifungwa Nyerere road unapata option njia nyingine? Tena inajulikana kabisa siku fulani anakuja watafunga njia. Sasa unaenda Morogoro njia imefungwa uko katikati kuna njia mbadala utachepuka?
 
Back
Top Bottom