Mbunge ahoji kuhusu misafara ya viongozi

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,794
21,372
Mbunge wa Viti Maalum, Kunti Majala ameshauri mamlaka zinazosimamia misafara ya viongozi, kuwasiliana ili kupunguza muda wa watu kusimama njiani wakati wakiwasubiri wapite.

Mbunge huyo ameyasema leo Aprili 12,2023 wakati akichangia mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

Mbunge huyo amesema viongozi wao wanawaheshimu, wanawapenda na wanajua changamoto zao kwa majukumu yao wanayoyafanya lakini watu husema muda ni mali.

“Kusimamisha wananchi zaidi ya saa tatu barabarani, kiongozi hajatoka anatokako, tuna wagonjwa, kuna watu ambao wanatakiwa kwenda kutekeleza majukumu yao mbalimbali.

“Niwaombe viongozi wanaosaidia hususani wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Polisi, biashara ya kusimamisha magari, mabasi na wananchi wengine kwa ajili ya viongozi wetu wanapopita wawe wanawasiliana kwa kadri muda unavyosogea wawaache Watanzania (wapiti),”amesema.

Amesema leo Waziri Mkuu alikuwa anatoka nyumbani kwake kuanzia saa 2.17 magari yalisimamishwa ambapo foleni imefika hadi Nzuguni na kuhoji hilo linapandisha uchumi.

Amehoji kama angeamua kutumia magari kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, wananchi watasimama kwa muda gani.

“Niombe sana hivi vitu vingine tuwe tunaenda na wakati. Kwa safari (viongozi), ndefu watumie ndege waache kutumia magari,”amesema.

Akitoa taarifa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema suala la kusimamia usafiri wa viongozi liko katika mamlaka zinazohusika.

“Nadhani ingekuwa ni bora kwa mbunge kutoa ushauri kwa mamlaka badala ya kuhusisha na utendaji kazi wa viongozi wetu ambao umewekwa kwa utaratibu unaozingatia heshima ya viongozi wetu hapa nchini,”amesema.

Amesema ni utaratibu huo uko dunia nzima na kwamba utaratibu huo umekuwa ukitumika kutoa heshima kwa viongozi.

Hata hivyo, akiendelea kuchangia Kunti amesema wananchi ndio wanaona adha na hivyo wakiamua kuuchukua ushauri huo ni sawa na pia ni sawa.

Chanzo: Mwananchi
 
Attachments

  • E045BA7A-91DE-4E43-97AC-73BAA921938D.jpeg
    E045BA7A-91DE-4E43-97AC-73BAA921938D.jpeg
    18.5 KB · Views: 4
Tz kupoteza muda ni jambo la kawaida unakuta mnasimamishwa barabarani hata huyo kiongozi hajaamka,hajaoga,hajanywa chai,hajaaga wenyeji wake,umbali aliopo hadi mliposimamishwa ni zaidi ya kilomita 350+
Huyo Jenista analinda ugali wake hawezi akawa na majibu yanayoeleweka.
 
JENESTER Mhagama huyu mmama sijawahi kabsa kumukubali yaani huwa anamajibu yakukatisha tamaa tu hata kama jambo liko wazi kama hili la misafara ya viongozi imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi
 
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum, Kunti Majala ameshauri mamlaka zinazosimamia misafara ya viongozi, kuwasiliana ili kupunguza muda wa watu kusimama njiani wakati wakiwasubiri wapite.

Mbunge huyo ameyasema leo Aprili 12,2023 wakati akichangia mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

Mbunge huyo amesema viongozi wao wanawaheshimu, wanawapenda na wanajua changamoto zao kwa majukumu yao wanayoyafanya lakini watu husema muda ni mali.

“Kusimamisha wananchi zaidi ya saa tatu barabarani, kiongozi hajatoka anatokako, tuna wagonjwa, kuna watu ambao wanatakiwa kwenda kutekeleza majukumu yao mbalimbali.

“Niwaombe viongozi wanaosaidia hususani wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Polisi, biashara ya kusimamisha magari, mabasi na wananchi wengine kwa ajili ya viongozi wetu wanapopita wawe wanawasiliana kwa kadri muda unavyosogea wawaache Watanzania (wapiti),”amesema.

Amesema leo Waziri Mkuu alikuwa anatoka nyumbani kwake kuanzia saa 2.17 magari yalisimamishwa ambapo foleni imefika hadi Nzuguni na kuhoji hilo linapandisha uchumi.

Amehoji kama angeamua kutumia magari kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, wananchi watasimama kwa muda gani.

“Niombe sana hivi vitu vingine tuwe tunaenda na wakati. Kwa safari (viongozi), ndefu watumie ndege waache kutumia magari,”amesema.

Akitoa taarifa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema suala la kusimamia usafiri wa viongozi liko katika mamlaka zinazohusika.

“Nadhani ingekuwa ni bora kwa mbunge kutoa ushauri kwa mamlaka badala ya kuhusisha na utendaji kazi wa viongozi wetu ambao umewekwa kwa utaratibu unaozingatia heshima ya viongozi wetu hapa nchini, ”amesema.

Amesema ni utaratibu huo uko dunia nzima na kwamba utaratibu huo umekuwa ukitumika kutoa heshima kwa viongozi.

Hata hivyo, akiendelea kuchangia Kunti amesema wananchi ndio wanaona adha na hivyo wakiamua kuuchukua ushauri huo ni sawa na pia ni sawa.

MWANANCHI
 
Hili nalo waliangalie ndege zipo wanashindwa kupanda wakati wao ndyo wamiliki hawalipii Chochote.Wanawapoteza muda mwingi watu barabarani .Muda ambao wangeingiza pesa Kwa Taifa.
 
Sio tu wanaboa yaani ni kero tupu , mtu yupo bafuni anaoga huku watu washasimamishwa na mikwara kibao ya mitutu ya bunduki , sasa unawaza mbona tafrani wazee
 
Back
Top Bottom