Misaada inayoitaji kupewa kipa umbele | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misaada inayoitaji kupewa kipa umbele

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by taneesha, Apr 13, 2012.

 1. t

  taneesha New Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani ndugu zangu mi nina kero moja na nimeona niitolee hapa.
  hivi mbona serikali yetu haiipi kipa umbele mambo muhimu juzi nimeangalia news TBC1 kuna mwanamke toka Arusha anahitaji 900,000 mwanae akafanyiwe operation ya kutobolewa sehemu ya haja kubwa . mtoto mchanga jamani hivi vitu kama hiyo hawa wabunge wa mikoa wenyewe tu si wanakuwa na uwezo wakumsaidia hizo fedha,?
  leo tena katika gazeti la Mwananchi mwanamke mwingine tena anashida na hela mwanae akafanyiwe surgery ya kuwekewa utumbo wa plastic hana hela hizo.
  jamani hawa watoto ndio wanaweza kuja kuwa marais wetu. kweli ningekuwa na uwezo huo ningewasaidia mimi binafsi.

  huku unasikia serikali imetoa mchango wa mamilioni kwenye vitu visivyo na misingi, wabunge wanachangisha hela za kusaidia familia ya Lulu wakati wao wana miguu na mikono ya kufanya kazi.
  mtoto mchanga analia anashindwa kujisaidi anatokwa damu tumboni kweli jamani tumefikia kubaya.


  Naomba serikali itowe michango yake kusaidia masikini zaidi kodi tunazolipa nchi hii sio kidogo.
   
Loading...