Mirathi wake wawili

KGM

Senior Member
May 21, 2007
190
20
Naomba ufafanuzi wa mirathi ya wake ewawili.
Nina kaka yangu aliyefariki miaka miwili iliyopita akiwa na wake wawili. Mke wa kwanza alifunga naye ndoa kanisani na amezaa naye watoto wanne na Mke wa pili amezaa alimtolea mahali ya kimila na amezaa naye watoto watatu.

Wakati anafariki Mke wake wa kwanza alikuwa amemkimbia kama Mwaka mmoja hiyo walikuwa hawaishi naye.

Alipofariki familia ilikaa na kuamua kaka mkubwa asimamie mirathi na Mali za marehemu waligawanyiwa wake za marehemu sawa sawa baada ya mama mzazi wa marehemu kupewa Shamba moja na ng'ombe mmoja kutoka kwenye Mali ya marehemu. Pia Shamba moja lilibakishwa ili liuzwe kugharamia madeni ya marehemu

Baada ya mgawanyo huo Mke mkubwa wa marehemu alikataa na akaenda mahakama ya mwanzo akisema hakushirikishwa na pia hamtambui bi mdogo wa marehemu. Mahakama ilikubali ombi la bi mkubwa kutoshirikishwa ikaagiza familia ikae upya.

Bi mkubwa alikata rufaa mahakama ya wilaya na hatimae mahakama imemkubalia kuwa kuwa hatukumshirikisha hivyo tukae naye yeye tu kwan yeye tu ndo anatambulika kisheria na hiyo bi mdogo tunamjua sisi hiyo hawezi kurithi yeye na watoto wake watatu. Hukumu hii imenishangaza na kuniumiza kwa kweli kwan nilidhani mwanamke ambaye ameishi na marehemu, akamtolea mahali, akazaa naye watoto watatu na actually yeye ndo amemuuguza marehemu kwan bi mkubwa alishamkimbia kwamba hawezi kumrithi mumewe mbele ya jicho la mahakama. Naomba wajuzi wa sheria mnisaidie kufahamu swala hili kwa kweli
 
Kwenye vitu kama hivi ndo unagundua Uislamu ni dini ya ukweli, ilishaliona kitambo na kuweka sheria kali!

Anyhow polen sana kwa msiba na majanga ya mke mkubwa
 
  • Huyo bi mdogo ndo chanzo cha mke mkubwa kutimka;
  • Wana familia mlitakiwa msuluhishe hilo wakati kaka yenu akiwa hai;
  • Hata wakati wa mazishi mlitakiwa mke mkubwa awepo.
  • Nyie teteeni haki ya hao watoto wa bi mdogo, huyo bi mdogo kimekula kwake.
 
Sheria unasema juu ya swala hili. Ni kweli kwamba Mke mdogo hatambuliki kisheria kwa MTU aliyefunga ndoa kanisani????
UOTE="Mamndenyi, post: 16101976, member: 41512"]
  • Huyo bi mdogo ndo chanzo cha mke mkubwa kutimka;
  • Wana familia mlitakiwa msuluhishe hilo wakati kaka yenu akiwa hai;
  • Hata wakati wa mazishi mlitakiwa mke mkubwa awepo.
  • Nyie teteeni haki ya hao watoto wa bi mdogo, huyo bi mdogo kimekula kwake.
[/QUOTl l E]
Kiukweli Mke mkubwa ndio chanzo cha Hata kaka mwenyewe kufariki. Lakin Mimi nacho uliza ni nini Sh
 
Kwenye vitu kama hivi ndo unagundua Uislamu ni dini ya ukweli, ilishaliona kitambo na kuweka sheria kali!

Anyhow polen sana kwa msiba na majanga ya mke mkubwa
Ni kweli kwamba bi mdogo hatambuliki kisheria ukishafunga ndoa kanisani???
 
Mkuu mie sio mwana sheria lakini kuna swali labda linaweza kusaidia kufahamu uamuzi huo wa mahakama

Mahakama imentambua bi mkubwa pekee kwa sababu gani ? ndoa ilisajiliwa serikalini na ana hati ya ndoa ambayo mke mdogo hana ?
 
Ni kweli kwamba bi mdogo hatambuliki kisheria ukishafunga ndoa kanisani???
Ukiangalia cheti cha ndoa kinasehemu unatakiwa utick kama ni ndoa ya mke mmoja au wake wengi, yeye alitick ya mke mmoja(naamini alifanya hivo)! Na cheti cha ndoa ni mkataba halali unaotambulika na serikali kwa hiyo ndoa ya pili haitambuliki unless ya kwanza imevunjika au iko kwenye process ya kuvunjika!
Labda hakimu awaonee huruma kwa mtakavyoelezea hali ya ndoa ilivokuwa (kama ilikuwa mbaya sana mnaweza pata ahueni)
 
So ndo kusema hawa watoto wa bi mdogo hawatakiwi kupata chochote??
 
Pole ndugu, kama hadi ndugu yako anafariki hakuwa ametalikiana na huyo mke mkubwa jambo ambalo talaka ni dokomenti ya kisheria, Hakika huyo bi mkubwa ataendelea kushinda kesi mahakamani hata kama mtakata rufaa.!!!. La maana hapo piganieni fungu la mirathi ya watoto wa Bi mdogo kwani kisheria wanahaki ya mali ya baba yao maana hawana baba mwingine, sheria zinawatambua watoto hao hata kama mama yao asingeishi kabisa na baba yao.
 
katika Hali kama hii ikitokea mke wa kwanza nihalali wa ndoa kafariki mke wa pili ni halali wa ndoa yupo hai Ila mke mkubwa kafariki Na mine wao kafariki kabaki mke mdogo ti Na Mali alizikuta kama nyumba ya biashara vipi kuhusu hizo Mali endapo mke mdogo yupo Na watoto wake Na watoto wa mke mke mkubwa wapo VIP upande wa Mali za marehem?
 
Naomba ufafanuzi wa mirathi ya wake ewawili.
Nina kaka yangu aliyefariki miaka miwili iliyopita akiwa na wake wawili. Mke wa kwanza alifunga naye ndoa kanisani na amezaa naye watoto wanne na Mke wa pili amezaa alimtolea mahali ya kimila na amezaa naye watoto watatu.

Wakati anafariki Mke wake wa kwanza alikuwa amemkimbia kama Mwaka mmoja hiyo walikuwa hawaishi naye.

Alipofariki familia ilikaa na kuamua kaka mkubwa asimamie mirathi na Mali za marehemu waligawanyiwa wake za marehemu sawa sawa baada ya mama mzazi wa marehemu kupewa Shamba moja na ng'ombe mmoja kutoka kwenye Mali ya marehemu. Pia Shamba moja lilibakishwa ili liuzwe kugharamia madeni ya marehemu

Baada ya mgawanyo huo Mke mkubwa wa marehemu alikataa na akaenda mahakama ya mwanzo akisema hakushirikishwa na pia hamtambui bi mdogo wa marehemu. Mahakama ilikubali ombi la bi mkubwa kutoshirikishwa ikaagiza familia ikae upya.

Bi mkubwa alikata rufaa mahakama ya wilaya na hatimae mahakama imemkubalia kuwa kuwa hatukumshirikisha hivyo tukae naye yeye tu kwan yeye tu ndo anatambulika kisheria na hiyo bi mdogo tunamjua sisi hiyo hawezi kurithi yeye na watoto wake watatu. Hukumu hii imenishangaza na kuniumiza kwa kweli kwan nilidhani mwanamke ambaye ameishi na marehemu, akamtolea mahali, akazaa naye watoto watatu na actually yeye ndo amemuuguza marehemu kwan bi mkubwa alishamkimbia kwamba hawezi kumrithi mumewe mbele ya jicho la mahakama. Naomba wajuzi wa sheria mnisaidie kufahamu swala hili kwa kweli
Kama hakukuwa na wosia wa marehemu kuhusu mgawanyo wa mali uamuzi wa mahakama ya Wilaya ni sahihi. Hapo Kuna ndoa ya kikristo ambayo kisheria inatambulika ni ya mke mmoja na haikuwa imebatilishwa.
 
Nimeanza kupata mwanga,. Sasa nini wanachoweza kupata
 
Back
Top Bottom