Naomba ufafanuzi wa mirathi ya wake ewawili.
Nina kaka yangu aliyefariki miaka miwili iliyopita akiwa na wake wawili. Mke wa kwanza alifunga naye ndoa kanisani na amezaa naye watoto wanne na Mke wa pili amezaa alimtolea mahali ya kimila na amezaa naye watoto watatu.
Wakati anafariki Mke wake wa kwanza alikuwa amemkimbia kama Mwaka mmoja hiyo walikuwa hawaishi naye.
Alipofariki familia ilikaa na kuamua kaka mkubwa asimamie mirathi na Mali za marehemu waligawanyiwa wake za marehemu sawa sawa baada ya mama mzazi wa marehemu kupewa Shamba moja na ng'ombe mmoja kutoka kwenye Mali ya marehemu. Pia Shamba moja lilibakishwa ili liuzwe kugharamia madeni ya marehemu
Baada ya mgawanyo huo Mke mkubwa wa marehemu alikataa na akaenda mahakama ya mwanzo akisema hakushirikishwa na pia hamtambui bi mdogo wa marehemu. Mahakama ilikubali ombi la bi mkubwa kutoshirikishwa ikaagiza familia ikae upya.
Bi mkubwa alikata rufaa mahakama ya wilaya na hatimae mahakama imemkubalia kuwa kuwa hatukumshirikisha hivyo tukae naye yeye tu kwan yeye tu ndo anatambulika kisheria na hiyo bi mdogo tunamjua sisi hiyo hawezi kurithi yeye na watoto wake watatu. Hukumu hii imenishangaza na kuniumiza kwa kweli kwan nilidhani mwanamke ambaye ameishi na marehemu, akamtolea mahali, akazaa naye watoto watatu na actually yeye ndo amemuuguza marehemu kwan bi mkubwa alishamkimbia kwamba hawezi kumrithi mumewe mbele ya jicho la mahakama. Naomba wajuzi wa sheria mnisaidie kufahamu swala hili kwa kweli