Mipango na mbinu za kibiashara kwa mjasiriamali Mdogo, Kati na hata Mkubwa

Mr Lukwaro

JF-Expert Member
Jun 3, 2023
357
621
Dunia leo hii inawataja mabilionea wafanyabiashara wakubwa kama vile Bilgates, Carlos Slim, Abraham Markovich, Trump, Mc Donald, Jeff Bezos na wengine wengi waliofanikiwa kifedha na kupata umaarufu mkubwa kupitia biashara.

Imekuwa ni changamoto Kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo kutambua. Je, ni mbinu gani wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakizitumia katika kupata mafanikio yao?

Watu wamekuwa wakijitahidi kusoma vitabu Na makala mbalimbali za wafanyabiashara wakubwa kama vile “I CAN, I MUST, I WILL” Kilichoandikwa na Dr.MENGI. Na Vitabu vingine vingi ili kuzipata mbinu bora za kibiashara. Kuna wakati wengine hufikiria Imani za kishirikina ili ziwasaidie kupata mvuto na umaarufu katika biashara zao lakini kwa bahati mbaya huwa hazifanyi kazi.

Yote kwa yote zipo mbinu na kanuni bora za biashara ambazo zikitumiwa vyema na wajasiriamali zinaweza kuwasaidia na ikakuondolea Imani haba juu ya uwezekano wa mafanikio ya kibiashara. Nazo ni Kama:-

1. Kutoa huduma na kuzalisha bidhaa bora zenye viwango vya kimataifa.
2. Ubunifu. (Creativity)
3. Njia za kutafuta soko (NETWORKING)
4. Nidhamu ya Pesa (MONEY DISCIPLINE)
5. Hakikisha mzunguko wa Pesa katika biashara yako (Invest in Business for cash flow)
6. Petient na Imani katika Mungu.

1.KUTOA HUDUMA NA KUZALISHA BIDHAA BORA ZENYE VIWANGO VYA KIMATAIFA.
Biashara inahitaji juhudi na ufanisi mzuri katika kuzalisha bidhaa ambazo zinaweza kushindana sokoni.Biashara nyingi za wajasiriamali huwa na mitaji mikubwa na zinashindwa kudumu kwasababu ya bidhaa kuwa zenye viwango duni (Low quality and poor quantity).

Hivyo haijalishi kiasi cha mtaji cha mjasiriamali ila UBORA wa huduma (services) na bidhaa (products) zake kwa wateja wake.

2. UBUNIFU (CREATIVITY)
Hii ni mbinu muhimu sana kwa mfanyabiashara na mjasiriamali mdogo, wa kati na hata mkubwa ili kuweza kuliteka soko. Je mbunifu ni mtu wa namna gani?

Mwenye kuipa na kuiongeza bidhaa yake Thamani kwa kuzingatia unafuu. (Eg. Packaging ).

Mwenye kuja na wazo la kutatua changamoto iliyoko ndani ya soko la bidhaa yake (Eg. Accessibility) na kupunguza matumizi ya fedha.

Mwenye kuonyesha upekee Fulani katika utowaji huduma kwa wateja wake.Yaweza kuwa namna ya kuwafikia wateja ,kuwa karibu na wateja au namna mpya inayowasaidia wateja katika kuifikia huduma au bidhaa yako

3. NJIA ZA KUTAFUTA SOKO (NETWORKING).
Biashara hupaswa kuwa na njia nzuri za kupanua soko na kuongeza wateja ili biashara iweze kukuwa. Wafanyabiashara na wajasiriamali wengi wa sasa hutumia njia za matangazo kama vile Mabango, Vyombo vya habari, pamoja na mitandao ya kijamii kama vile Whatsup,Instagram na n.k .Sambamba na Network nzuri ni vyema mfanya biashara kuzingatia vitu kama vile,
a. Maono ya biashara (Good vision).
b. Uhakika wa busara na hekima baina yako na wateja ili wateja wawavute na wateja wengine.
c. Jina zuri la kuitambulisha biashara yako. (Good name to brand your business).
d. Mahusiano chanya yako wewe mfanyabiashara na wafanyabiashara wengine.


4. NIDHAMU YA PESA (MONEY DISCIPLINE)
Hii ni sehemu muhimu kwani ikikosekana umakini biashara ya mjasiriamali haiwezi kuongezeka .Pia ili kulinda mtaji wa biashara mara nyingi huwa ni pesa. Kanuni muhimu za fedha kwa mjasiriamali ni kama vile;-
  • Epuka kukopa fedha hasa mikopo ya riba.
  • Epuka kutumia pesa ambayo bado haujaipata.
  • Tenga akiba.
  • Omba ushauri kwa waliofanikiwa na sio kuomba fedha.
  • Epuka kukopa fedha bila mipango (Ovyo) tafuta vikundi sahihi vinavyotoa na ushauri

MBINU ZA KUPATA WATEJA WENGI NA KUVUKA MATARAJIO KATIKA BIASHARA YA MJASIRIAMALI.
Uliza mrejesho baada ya kutoa uduma au kuuza bidhaa. Tumia mbinu ya kuvutia kibiashara.
a. Mjue mteja wako kisha nenda kule aliko.
b. Kutana na jamii ili kuongeza wateja wapya.
c. Hakikisha kila mteja anapokutafuta huwa unapatikana. (Mawasiliano mazuri).

MBINU ZA KUJALI WATEJA KATIKA KIWANGO BORA HASA CHA KIMATAIFA.
Hakikisha huduma bora na bidhaa nzuri zinazokidhi mahitaji ya wateja wako.(Mnyororo bora wa biashara).

Kufikia matarajio ya wateja wako, Kama vile kufanyia kazi maoni yao, kuwashangaza kwa ubunifu, kugawa zawadi mbalimbali kwa wateja.

Kutoa huduma kwa wakati yaani kuzingatia mudaa. Na hasa kutatua matatizo ya wateja wako haraka.

Kufanya vitu vya ziada kama vila kubadilisha vifungashio, ongeza ladha mara kwa mara.

Kuwa mwenye furaha na mchangamfu wakati unatoa huduma.

Jifunze kwa wafanyabiashara wenzako pamoja na kwa wateja.

Wafikie wateja wako wapya au wale wasikuzote mara kwa mara kwa kuitangaza biashara.

Kuwa na mbinu bora za kumhudumia mteja wako aliyekasirika.

5. PETIENT NA IMANI KATIKA MUNGU.
Mfanyabiashara/Mjasiriamali anaetamani kufanikiwa ni muhimu awe na Uvumilivu na mwenye Imani katika Mungu. Wajasiriamali wengi hushundwa kufanikiwa kwasababu ya kukosa uaminifu, uvumilivu na Imani katika Mungu pale wanapopitia changamoto katika biashara zao. Imani thabiti katika Mungu na uvumilivu ni muhimu Sana katika biashara yoyote. Hii huambatana na kutoa misaada na Sadaka halali kwa Imani ya mfanyabiashara husika.

Biashara yoyote mpya ili ifikiwe lazima kuwe na:
Ubunifu.
Eneo zuri la biashara.
Mtaji sio lazima iwe ni pesa au mtaji mkubwa.
Ujasiri.
Kuliteka soko.
Nidhamu ya pesa.
Mungu kwanza.
Lugha nzuri kwa wateja.
Malengo na mkakati.
Utekelezaji kwa makini.

JINSI YA KUANZISHA BIASHARA NA MTAJI MDOGO
Wajasiriamali wengi wamekuwa wakilalamika kuhusu mitaji midogo. Ukweli ni kwamba kuwa na mtaji mdogo sio sababu ya kukuzuia kuanzisha biashara yako kisha polepole ikaanza kukuwa, Baada ya kuwa na wazo la biashara unaweza ku:-
a. Tafuta eneo zuri la biashara
b. Fanya biashara ya mambo unayoyaelewa ili usipoteza mea kutafuta mambo mapya.
c. Kama wazo lako la biashara ni kubwa na mtaji wako ni mdogo, Shirikiana na Mwingine.
d. Waweza kuomba mkopo hasa mikopo katika vikundi sahihi au Ndugu na Marafiki.
e. Tafuta elimu Zaidi juu ya masuala ya kibiashara ili kuongeza mawazo.
f. Tangaza biashara yako katika mitandao ya kijamii na mabango madogo ili kupunguza gharama.

BIASHARA KAMA VILE
Kuuza mayai, Kuuza maindi, Kuuza mitumba, Kuuza vyakula, Kuuza matunda, Kuuza maji na Nguo za wanawake

HITIMISHO:
Licha ya changamoto za ushindani sokoni na teknologia katika uzalishaji kwa wajasiriamali, changamoto kubwa ni:- Sapoti ndogo kutoka kwa Serikali hivyo hupelekea Kudumiza sekta ya Biashara na wajasiriamali.
 
Asanteni sana Jamii Forums platform, nimepata sehemu ya kuyafanya mawazo yangu yaifikie jamii
 
Kuna Siri kubwa kwenye utajiri mkubwa asikiaye na afahamu...usione mbele kweupe ukadhani ni rangi nyeupe nyuma mbele na katikati ......nilianza na 5000 Leo Nina bilionibilioni myfuti....
 
Back
Top Bottom