Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Naomba niwaambie jambo moja. Miongoni mwa mambo ambayo humkera mwanamke ni kukutana na mwanaume mwongo na anayejikweza. Mwanamke na hata mwanaume hupenda kitu au mtu asilia na sio mtu feki.
Ukweli ni kwamba kwa kutojiamini kutokana na kuambiwa kwamba wao ni bora kuliko wanawake, na kufundishwa kwamba ili waonekane wa maana ni lazima waoneshe mafanikio na ndipo watakapokubaliwa na wanawake, wanaume wengi wamekuwa wakijikweza na kusema uongo ili kuwapata wanawake.
Ni kweli huwapata wanawake hao, lakini cha kushangaza huwapata wanawake hao sio kwa sababu ya uongo na kujikweza kwao, bali ni kwa sababu wanakuwa wamevutiwa nao. Na kwa sababu ya ujinga mwanaume atadhani amempata mwanamke kwa sababu ya uongo na kujikweza kwake!
Kwani hamjawahi kuona wanawake kwa maelfu wanakimbia ndoa za wenye fedha na walio Maarufu? Cécilia Ciganer-Albéniz, Mke wa Rais wa Ufaransa Nicolas Salkozy ni mfano wa jambo hili.Kama ingekuwa anachoangalia mwanamke ni mali na umaarufu, naamini kusingekuwa na talaka nyingi.
Kwa asilimia nyingi, mwanaume ndiye anayejikanyaga kwa mwanamke, ndiye anayejikweza ili mwanamke ampandishe thamani.