Mimi sina Dini, Nitapata Mke Mwenye itokadi kama yangu?

Usijar utapata. Mwanamke siku zote huwa chini ya mwanaume. Kama umeweza kuamini hakuna uwepo wa mungu, basi kwa facts ambazo zilikufanye wewe usiamini, unaweza mfungua macho na mwenzako.

Mm ni mmoja kati ya wasioamini uwepo wa mungu. Nina mke jembe ambaye nilimpa fact mpaka sasa yupo kwenye mstari wangu
Napata moyo sana kukutana na michango kama hii. Mwamko wa watu unatia faraja sana.
 
Tupo mkuu hata mimi naona jamaa hana cha kupoteza akafunge nae ndoa popote tu iwe kanisani,msikitini Mimi sina presha na hizi dini nkikutana na Salma ntaitwa Omary nkikutana na Sarah ntaitwa Christopher basi mradi sikwamishi lolote kwa jili ya dini
Ndiyo hivyo, complications hizi za watu utapasua kichwa tu.
 
Wakuu nimekuwa nikiishi bila kuamini chochote kwa miaka 8 sasa. Usiniulize kwa nini, we jua nipo hivyo, siamini uwepo wa mungu na hata shetani.

Nimedate na wanawake 7 mpaka sasa, na sasa nina miaka 25.
Kwa sasa Nina mahusiano na binti mmoja yeye ni mkatoliki mwenye imani sana na huwa hapendi ucheze na Mungu.

Nimemweleza nataka kumwoa na ningependa iwe kabla ya mwaka huu akasema mpaka awasiliane na wazazi.

Nilifanya mipango kama tamaduni zetu za kitanzania za kumtuma mshenga.
Ikafika kwenye suala la ndoa, hapo ndio mtiti ulipo anzia.

Mwazoni binti alijua mimi ni mkatoliki na huwa namdanganya mara nyingi nimekwenda kanisani. Huwa ananielewa sana kutokana na ustaarabu na ukarimu nilionao.

Ila mwezi wa 11 ndipo nilipoweleza ukweli kuwa siwezi funga ndoa ya kanisani kwakuwa mimi sina dini na siamini uwepo wa mungu.

Binti hakuamini maneno yangu mpaka ikafikia kuamini natumia mbinu hiyo kumkataa.
Nilimweleza km yupo tayari twende tukafunge ndoa ya serikali.

Binti alikataa na kusema imani yake haimruhusu kuishi na mtu ambae haamini chochote na hata wazazi wake wasinge afiki kitu km hicho licha ya kumsisitiza lazima aolewe na mkatoliki tu.

Imebidi tuvunje mahusiano yetu na sasa nimeamua kutuliza kichwa kwanza.

Napenda kuuliza hii kitu, kuna wasichama ambao hawaamini uwepo wa mungu au ambao hawana dini kabisa?

Je nitaweza pata binti ambae anaendana na msimamo wangu?

Ushauri tafazali, ila usijikite kuuliza kwa nini sina dini.
Bora uamini yupo utakapoenda umkose kuliko usiamini halafu umkute. Kwa issue ya laaziz labda uwanja Wa fisi
 
Usijar utapata. Mwanamke siku zote huwa chini ya mwanaume. Kama umeweza kuamini hakuna uwepo wa mungu, basi kwa facts ambazo zilikufanye wewe usiamini, unaweza mfungua macho na mwenzako.

Mm ni mmoja kati ya wasioamini uwepo wa mungu. Nina mke jembe ambaye nilimpa fact mpaka sasa yupo kwenye mstari wangu
Natamani nifahamu hizo facts ulizompa akaelewa na mie nielewe inakuwaje hapo kuna mwanaume kipindi cha nyuma kidogo aliniambia nataka nkuoe ila usiende kanisani wala msikitini nilishtuka na kushangaa sana nkamwambia hapana me sijalelewa hivo najua Mungu yupo na ananafasi katika maisha yangu basi nkakutana na mwingine wa imani yangu.

Ila hakunipa facts kabisa nkaelewa anasema ukubali tu.
 
Huamini uwepo wa Mungu!!? Bora hata ungesema huna dini, go to hell mfuasi wa ibilisi wewe.
 
Natamani nifahamu hizo facts ulizompa akaelewa na mie nielewe inakuwaje hapo kuna mwanaume kipindi cha nyuma kidogo aliniambia nataka nkuoe ila usiende kanisani wala msikitini nilishtuka na kushangaa sana nkamwambia hapana me sijalelewa hivo najua Mungu yupo na ananafasi katika maisha yangu basi nkakutana na mwingine wa imani yangu.

Ila hakunipa facts kabisa nkaelewa anasema ukubali tu.
Ni somo refu kidogo na linahitaji uelewa. Ni vitu ambavyo ukishavijua, hakika utajiona mzembe sana maana ni mtego mdogo tu
 
Usijar utapata. Mwanamke siku zote huwa chini ya mwanaume. Kama umeweza kuamini hakuna uwepo wa mungu, basi kwa facts ambazo zilikufanye wewe usiamini, unaweza mfungua macho na mwenzako.

Mm ni mmoja kati ya wasioamini uwepo wa mungu. Nina mke jembe ambaye nilimpa fact mpaka sasa yupo kwenye mstari wangu
Unajisifu et ulimpa fact mwanamke! huwa wanasema wanawake hawana dini unajua kwanini?

Wanawake kubadili imani kwa sababu ya mapenzi mbona kitu rahisi sana wala hata sio kitu cha kuja kusema et umempa fact.
 
Natamani nifahamu hizo facts ulizompa akaelewa na mie nielewe inakuwaje hapo kuna mwanaume kipindi cha nyuma kidogo aliniambia nataka nkuoe ila usiende kanisani wala msikitini nilishtuka na kushangaa sana nkamwambia hapana me sijalelewa hivo najua Mungu yupo na ananafasi katika maisha yangu basi nkakutana na mwingine wa imani yangu.

Ila hakunipa facts kabisa nkaelewa anasema ukubali tu.
Hakuna facts zozote,kinachofanyika ni sawa na kumshawishi mtu aliyefanyiwa uovu kwenda kufanya revenge tu.

Yani mtu ambaye tayari ana tatizo kwenye imani yake ndiyo anapewa hizo porojo zenye kuitwa facts,lakini hivi hivi tu sioni ni vp zinaweza kuwa facts.
 
na hutampata wa kudumu kutokana na misimamo yako mikari maana huna hofu ya Mungu yaani utaoa na kuacha kila siku maana hakuna mwanamke atakaekuvumilia
 
mke au mme utoka kwa mungu, wewe utambui uwepo wake mke utampata wapi?

kwa shetani nako uwezi pata mke maana amoja ma kiburi cha shetani ila nae anatambua uwepo wa mungu, ndo maana shetani tunamkemea kupitia nguvu za mungu, na ujue hakuna mtu wa shetani watu wote ni wa mungu, hata wewe ni wa mungu

pamoja na kujitutumua kote hapa si ajabu ukipataga shida unasema "mungu wangu"

mungu akiamua leo kesho unabatizwa marehemu
 
Back
Top Bottom