Mimi sina Dini, Nitapata Mke Mwenye itokadi kama yangu?

hiden

JF-Expert Member
Sep 28, 2015
381
1,000
Wakuu nimekuwa nikiishi bila kuamini chochote kwa miaka 8 sasa. Usiniulize kwa nini, we jua nipo hivyo, siamini uwepo wa mungu na hata shetani.

Nimedate na wanawake 7 mpaka sasa, na sasa nina miaka 25.
Kwa sasa Nina mahusiano na binti mmoja yeye ni mkatoliki mwenye imani sana na huwa hapendi ucheze na Mungu.

Nimemweleza nataka kumwoa na ningependa iwe kabla ya mwaka huu akasema mpaka awasiliane na wazazi.

Nilifanya mipango kama tamaduni zetu za kitanzania za kumtuma mshenga.
Ikafika kwenye suala la ndoa, hapo ndio mtiti ulipo anzia.

Mwazoni binti alijua mimi ni mkatoliki na huwa namdanganya mara nyingi nimekwenda kanisani. Huwa ananielewa sana kutokana na ustaarabu na ukarimu nilionao.

Ila mwezi wa 11 ndipo nilipoweleza ukweli kuwa siwezi funga ndoa ya kanisani kwakuwa mimi sina dini na siamini uwepo wa mungu.

Binti hakuamini maneno yangu mpaka ikafikia kuamini natumia mbinu hiyo kumkataa.
Nilimweleza km yupo tayari twende tukafunge ndoa ya serikali.

Binti alikataa na kusema imani yake haimruhusu kuishi na mtu ambae haamini chochote na hata wazazi wake wasinge afiki kitu km hicho licha ya kumsisitiza lazima aolewe na mkatoliki tu.

Imebidi tuvunje mahusiano yetu na sasa nimeamua kutuliza kichwa kwanza.

Napenda kuuliza hii kitu, kuna wasichama ambao hawaamini uwepo wa mungu au ambao hawana dini kabisa?

Je nitaweza pata binti ambae anaendana na msimamo wangu?

Ushauri tafazali, ila usijikite kuuliza kwa nini sina dini.
 

Kibo255

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
4,408
2,000
[HASHTAG]#freemaxencemelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TunamtakaBenAkiwaHai[/HASHTAG]
[HASHTAG]#JusticeForLema[/HASHTAG]
[HASHTAG]#usirudiekosa2020[/HASHTAG]
 

Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
9,032
2,000
Ukitaka kufunga ndoa kanisa katoliki watataka barua toka parokia unakosali. Hapo ni bibie aamue kuasi vinginevyo katafute mwenzio Wa jadi.
 

ZNM

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
1,083
2,000
Uwe na dini ama usiwe nayo, huzuii ama huongezi wingi wa siku za uhai wako, tafuta utakayejirisha kukufaa maishani kisha tia mimba na ulee zaidi ya watu wa dini!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom