Mimi Piga ua, Magufuli namuunga mkono na nitaendelea kumuunga mkono: niulize kwanini?

Hisha Sorel

Senior Member
Dec 27, 2017
192
140
Nimesoma criticism nyingi kuhusu Mh. Magufuli lakini mpaka sasa sijaona hata moja inayo-niconvince.

Critisism hizi zinaonekana wazi zinapotoka: Bussiness na foreign ruling class wakitumia nguvu yao ya press kuyumbisha effort za nchi kujiondoa toka kwenye mtego wa umasikini.

Kwani ni lengo lao kuona nchi inaendeshwa kama "bussiness as usual": tupe madini, ardhi, na control sisi tutakupa mikopo ili tukudai na mwishowe tuku-control.

Struggle ya kuondoa nchi katika mtego huo ndo chanzo cha malalamiko ya aina yoyote kupewa sauti:

Leo, wameanza kulalamika kuhusu Rais Magufuli kuwekeza Chato ambayo ipo Tanzania na wanaoishi ni waTanzania na pia auhitaji visa kuamia.
Miaka yote ambapo Dar es salaam, ambao sio mji mkuu, imekuwa ikipata priority kwenye investment hakuna aliekuwa akilalamika; ila leo imekuwa tatizo kwa Chato.

Uvivu wa critics inabidi uwe exposed kwani unaharibu credibility ya argument zao

Mh. Magufuli ni Force muhimu katika hii nchi: we need change and he is the change!
 
Sawa lakini ngano 32000 mafuta 82000
Na asilimia 14.7 ya Wamarekani hawana kazi, waliobakia wa deal na gig economy

Maisha ni magumu kila pande: kikubwa na kujaribu kutatua matatizo kwa sera zenye manufaa ya mda mrefu.

Serikali ya Mh. Magufuli imelenga ku-invest kwenye viwanda, na usafilishaji (bara bara): hopefully itazaa matunda
 
Miaka yote ambapo Dar es salaam, ambao sio mji mkuu, imekuwa ikipata priority kwenye investment hakuna aliekuwa akilalamika; ila leo imekuwa tatizo kwa Chato.
Mkuu kama unataka kumtetea Magu wewe mtetee tu... ila haya ya Chato yaache tu maana hayana mfanoa wake, labda utusaidie; yeye ni wa 5, je wa 4 waliotangulia walifanya nini kwao?

Kuhusu Dar... kaa ukijua kuna Capital city na Commercial Capital.
 
Miaka yote ambapo Dar es salaam, ambao sio mji mkuu, imekuwa ikipata priority kwenye investment hakuna aliekuwa akilalamika; ila leo imekuwa tatizo kwa Chato.
Dar ni business hub ya Tanzania, ndiyo maana inatambulika kama mji wa kibiashara wa Tanzania, na hii ni kutokana na location yake. Huwezi linganisha na mikoa mingine na pia kwa muda mrefu ofisi zote za serikali na mashirika makubwa plus barozi za nchi mbalimbali ziko hapa.
 
nani aliyechagua Dar iwe bussiness Hub, mi sikumbuki kupigia kura hiyo decision!!!

mwisho wa siku mji ukua kulingana na investment: wakoloni walichagua Dar waka-invest na wanachi wakafuate investment.

Kwanini tusifante ivyo kwa miji mingine: tena mji wenye wazawa
 
Mkuu kama unataka kumtetea Magu wewe mtetee tu... ila haya ya Chato yaache tu maana hayana mfanoa wake, labda utusaidie; yeye ni wa 5, je wa 4 waliotangulia walifanya nini kwao?

Kuhusu Dar... kaa ukijua kuna Capital city na Commercial Capital.
hiyo commecial capital inachaguliwaje? kama sio investment ya wakoloni ilisukuma watu kuchukulia kama capital.

2. Kwani Mh. Magufuli anamiliki Chato? Kwani Chato hakuna waTanzania?
 
nani aliyechagua Dar iwe bussiness Hub, mi sikumbuki kupigia kura hiyo decision!!
Location yake imeifanya dar iwe hivyo haihitaji kupiga kura hata. Ni sawa sehemu yenye mgodi automatically kutatokea mji mkubwa na maendeleo ya haraka.

Sipingani haya kufanyika sehemu nyingine, ile usilinganishe na dar. Halafu unajua kwanini watu wanahoji, ni sawa wewe uwe kiranja wa chakula halafu nyama nyingi zielekee kwako lazima watu wataunganisha cheo chako na unachokipata.

Haya yangekuwa yanafanyika chato wakati aliyeko madarakani siyo mtu wa huko usingesikia kelele hizo. Mwaka 2015 nilipita chato, nikashangaa kunataa za barabarani japo nimekaa hapo almost three hours, na kama yalipita magari hayazidi 3 na kumbuka wakati huo mheshimiwa alikuwa waziri wa barabara. Punda tu ndiyo walikuwa wengi, sijajua sasa maendeleo yamefika wapi.
 
Dar ni mji wenye wakazi takribani milioni 7,wakazi ambao ukiwapeleka nchi jirani ya Zanzibar hata kupishana hawateweza Sababu ya mbanano, wenye akili timamu priorities zikipelekwa huko wala hatuwezi kuhoji, lkn chizi mmoja anakuja kutetea priorities zipelekwe kijiji cha chato ambacho wakazi wake hawafiki hata laki moja!!
 
Location yake imeifanya dar iwe hivyo haihitaji kupiga kura hata. Ni sawa sehemu yenye mgodi automatically kutatokea mji mkubwa na maendeleo ya haraka....
sijakuelewa kwaninin Dar ni tofauti: kwani Dar palianza kama Chato vile, sehemu fulani ambapo wakoloni walipapenda kisa ukaribu na bahari.

Kuhusu yeye kutokea chato, tatizo lipo wapi?
Wanaoishi Chato ni waTazania pia, wanalipa kodi, na wanataka maendeleo.

Maendeleo kama barabara na taa sio kama chakula kwani kila mtu anaweza kutumia; hata wewe uaempinga magufuli umeweza kutumia.

maendeleo sio lazima yafuate demand: unaweza ku-invest ukitegema sehemu kukua baada ya maendeleo kufika. Barabara inaweza kujengwa ikitegemea kuvutia wafanyabiashara kuhamia sehem flani.

sema kweli sijui kwanini 2021 tunalalamika kwamba mtu kajenga barabara, air port, na hospitali.

SouthAfrika walipigwa nyumba binafsi ya Zuma, Eti huku tunamwinda Mh. Rais kwa kujenga mali ya Umma.

dah!
 
Dar ni mji wenye wakazi takribani milioni 7,wakazi ambao ukiwapeleka nchi jirani ya Zanzibar hata kupishana hawateweza Sababu ya mbanano, wenye akili timamu priorities zikipelekwa huko wala hatuwezi kuhoji, lkn chizi mmoja anakuja kutetea priorities zipelekwe kijiji cha chato ambacho wakazi wake hawafiki hata laki moja!!
watu hao million 7 walitokea wapi kama hawakufuata maendelea yaliotokana na uwekezaji kwenye jiji la Dar

hivi unafikili wakoloni wasingejenga Dar watu wangeamia Dar?

Investment inamaanisha kuweka ukitegemea matunda mbeleni.

Sijui kwanini Chato aipaswi kupata investment
 
sijakuelewa kwaninin Dar ni tofauti: kwani Dar palianza kama Chato vile, sehemu fulani ambapo wakoloni walipapenda kisa ukaribu na bahari.

Kuhusu yeye kutokea chato, tatizo lipo wapi?
Wanaoishi Chato ni waTazania pia, wanalipa kodi, na wanataka maendeleo.
Dar geographical location yake ndiyo inaifanya iwe kama ilivyo hata mkoloni aliichagua kwasababu ya geographical location na imeendelea kuwa hivyo.
Sasa mkuu ukitaka kujicompare una jicompare na mwenye afya au mgonjwa? Mimi nitajicompare na mwenye afya, siwezi sema eti mimi naumwa ila flani anaumwa zaidi. Kwahiyo siyo haki kufanya comparison na wizi aliofanya Zuma na ndiyo maana hata hakumalizakipindi chake.
 
Location ilikuwa priority ya mkoloni (Extraction ya resources kupitia port)

Sisi hatuna lengo la kusafilisha mali kwenda ulaya: ila tuna nia ya kukuza ndani ya Tanzania amabapo wazawa wanaishi.

Chato pamoja na sehemu nyingine kuna "strategic interest", So kwa kujenga miundombine tunavutia watu ndani ya nchi na kusambaza maendeleo.

Point yangu ya Mr. Zuma ilikuwa na nia ya kuonyesha ubora wa magufuli, kiasi kwamba kwa mara ya kwanza Tanzania tunabishana wapi tujenge miundombinu na sio kukwidana kisa pesa za richmond.

Kila kiongozi na strategy yake ya infastracture, sio kila nchi ita-invest kwenye port cities, na sio kila nchi inalenga kunufaisha bussiness class tu: kuna baadhi ya viongozi wana cultural, security, au other interest.

swali la wapi investment iende ni complex lakini sio simple kama watu wanavyotaka: "more people= more investment" "bussiness as usual". rubbish
 
watu hao million 7 walitokea wapi kama hawakufuata maendelea yaliotokana na uwekezaji kwenye jiji la Dar

hivi unafikili wakoloni wasingejenga Dar watu wangeamia Dar?

Investment inamaanisha kuweka ukitegemea matunda mbeleni.

Sijui kwanini Chato aipaswi kupata investment
Hakuna aliyesema chato haipaswi kupata investment, bajeti ingekuwa inaruhusu ilipaswa kila mtaa hapa tz upate investment zaidi hata ya chato, lkn tatizo linakuja kasungura ni kadogo inatakiwa kila mkoa walau upate kamnofu angalau kapunje kamoja ka mshikaki, pia kumbuka investment zipo planned kitaifa ambazo kuna short/medium na long term, ni uendawazimu kujenga national airport chato ili kije kitumike mwaka 2100 wakati kuna wakazi million 7 daresalam hawana uhakika wa maji.
 
Back
Top Bottom