Chikawe Jr
Member
- Jun 6, 2017
- 23
- 85
Na: Juma George
Sio kazi rahisi kuhimili mashambulizi ya wapinzani iwe nje au ndani pale unapoonyesha waziwazi kukipenda Chama Cha Mapinduzi au Kumuunga mkono Rais Magufuli. Unahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana kuyapokea matusi na kejeli usiku na mchana tena wakati mwingine yakitokea upande ambao hutegemei (Ndugu zako katika Imani).
Toka kuingia kwa Rais Magufuli na kuunda Serikali ya Awamu ya tano, watanzania tumepitia changamoto nyingi lakini zaidi sana tulioamua kumuunga mkono jitihada zake kama Rais tumepitia hayo Mara mbili. Rais alipoanza safari yake tulikuwa wengi tulioshangilia na kupiga mayowe ya furaha tukiashiria kukubaliana na yanayotokea, na ni ukweli usiopingika wapo ambao walienda mbali zaidi kwa kupigwa na butwaa kwa kile kilichokuwa kinaendelea.
Tulikuwa pamoja na kujisifu hakika tumepata Mtu sahihi kwa taifa letu na sasa kilio cha watanzania kwa miaka mingi kinakwenda kunyamaa kwa kuwa amepatikana mkombozi. Furaha hii ilidumu kwa muda ingawa siku hadi siku mambo yaliendelea kuwa tofauti kwani baadhi yetu walianza kuchoka baada ya maslahi yao kuanza kuguswa.
Hatukufahamiana kabla isipokuwa tuliunganishwa na jambo moja tu Magufuli 4 Change. Lakini kadri muda ulivyotutupa mkono na mabadiliko kuanza kumgusa mmoja baada ya mwingine tulianza kupungua, na mbaya zaidi wale waliopungua ndio wamekuwa wakitoa mashambulizi makubwa kwa Rais na Kila Mtanzania aliyeonyesha nia ya kumuunga mkono hawakumuacha salama.
Wapo walioguswa kwa kunyimwa uteuzi kwa kuwa ndio yalikuwa maslahi yao na baada kukosa wakageuka mwiba kwa Rais huyu Mzalendo, na wengine waligeuka baada ya Mabosi zao waliokuwa wanawafadhili katika hali zao kuguswa na Rais Magufuli.
Moyo wa mwanadamu ni kichaka, hatukujua kwanini tulikuwa nao, lakini tunajua kwanini hatupo nao tena katika harakati hizi za kuijenga Tanzania mpya. Baada ya kuishindwa hii safari sasa wamegeuka na hawana tofauti na WAPINZANI naam, WAPINZANI ndio marafiki zao siku hizi, husema kama wasemavyo wapinzani na hutenda vivyo hivyo.
Ingawa bado hawajajivika vazi rasmi lakini Chui hata umfungie ndani vipi hawezi kuwa paka, matendo yao na maneno yao yanadhiirisha kile kiujazacho moyo. Wamekuwa sio wenzetu tena, na sasa nawaona wamepata mashabiki na wafuasi wa matendo na maneno yao, HIVI NI NANI ALIYEWAROGA?.
Hivi unaanzaje kumpinga Rais Magufuli eti kisa KAZUIA AKAUNTI za MAFISADI? Au KUZUIA wizi katika MIGODI YETU uliowezeshwa na baadhi ya watanzania wenzetu? au Kuzuia Utakatishaji wa fedha uliokuwa umetapakaa nchi nzima? au KUTUMBUA watumishi wabadhilifu wa rasilimali za UMMA?. Katika hili nina ujasiri kusema watakuwa wanufaika wa haya maovu na sasa hali imekuwa ngumu wameamua kugeuka.
Wamegeuka na kuamua kushambulia kila anaemuunga Mkono Rais Huyu Mzalendo. Silaha kubwa wanazotumia ni maneno ya kejeli 'ETI UNASIFIA UNATAKA UTEUZI' mbona mwanzo tulikuwa tunasifia wote je na 'SISI TUKISEMA MNASHAMBULIA KWA KUWA MMEKOSA UTEUZI' mtasemaje?. Hamta tukatisha tamaa, nguvu ya umoja itawashinda, Jemedali Rais Magufuli yuko IMARA kama chuma hatingishwi.
Niwaombe watanzania wazalendo ambao siku zote wameonyesha kumuunga mkono Rais Magufuli kutokatishwa tamaa na vijembe hivi. Rais anawahitaji sana Watanzania wenye Uzalendo wamuunge mkono. Spika wa Bunge Job Ndugai na Naibu wako Dr. Tulia Akson endeleeni kuwa imara sisi Watanzania Masikini tunawategemea. Kumbukeni hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu, hiyo nayo ni Huduma na inamalipo kwa wakati wake.
Tumewapa dhamana mtufikishe mahali salama acheni wale wanaohukumiwa na historia wavune walichopanda, maana imeandikwa Apandacho mtu ndicho atakachovuna.
Umoja wa kitaifa ndio ushindi wetu tusikubali mtu kutugawa kwa namna yoyote ile. NAMPONGEZA RAIS NA KAMATI iliyosimamia mchakato wa maridhiano hakika Historia hii itakumbukwa vizazi hata vizazi.
TANZANIA IMARA INAJENGWA NA WAZALENDO WA KWELI
Aluta Continua
Mapambano yanaendelea.
Chikawe Jr.