Mimi nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba Magufuli atarudi na uenyekiti Dodoma

Hivi NCHI hii MSUKUMA ni kosa kuwa Rais? Pia nani kawambieni Magufuli ni MSUKUMA?
Hizo porojo ndizo zimeifanya nchi kukaa zaidi ya miaka 15 bila rais! Haya kwa vile ni nchi ya kidemkrasia na hapo ni wengi wape, Wahaya na Wachaga walishajikalia pembeni sasa unganisheni na Wasukuma. Mpaka huu ujinga utakapotutoka vichwani naamini wenzetu watakuwa wameshaanzisha makazi ya kudumu kwenye sayari ya Mars.
 
Hivi Uchaguzi uliopita haujawafundisha kama Ccm siyo Chama cha mchezo mchezo? Hamjajifunza tu? Hahaha mna vichwa vigumu aisee! Dr Magufuli ni Mwenyekiti mpya wa chama. Hakuna wa kuzuia.
 
Magufuli anaenda kinyume na Jf sasa ujumbe kaupata haweki msukuma hata mmojA
 
Ninachojua tayari JPM ndiye Mwenyekiti Mpya wa CCM. Tena atapitishwa kwa kura nyingi tu. Kama kuna watu wanatoa hela ili asipitishwe wasubiri maumivu ya hasara nyingine baada ya ile ya kumpitisha mgombea urais kuumiza wengi.
 
Nasema nitakuwa wa mwisho. Makundi ya watu waliopita mikoani na maburungutu ni mengi mno na yote ukiangalia yana watu mashuhuli nyuma yake, na hoja zao zinafanana kwamba chama hicho kitageuzwa chama chama cha kisukuma na kikanda .


Sasa hata kama kuandika tu vizuri jina la Raisi wa nchi hauwezi kwa nini iwe ajabu kutokujua utaratibu wa CCM?
 
Ningependa kumshauri JK kwamba akijiandaa kukabidhi uenyekiti ahakikishe misingi ya uongozi,hekima na nidhamu ya KATIBA zinaheshimika.Tena hili alisimamie kwa nguvu zote
 
Nnachompendea JPM ni kuwa yy wala haonekani kuushobokea huo uenyekiti wa chama... Ni kama anawachora tu watu wanavyohangaika... Na akiupata tu anatumbua mtu faster.. Awamu hii lazima watu waishi ka mashetani
Kama ambavyo hakushobokea uraisi.... alipoupata tu... Alianza kutembea kwa mguu hadi hazina
 
Itakuwa historia mpya
Kama kura zitapigwa kura historia mpya itapatikana. Kuwa atapatikana Mwenyekiti mpya kwa lazima lakini kura hazikutosha.
Maana hata NDIYO ikiwa 30% bado watampa tuu nakusema ni 95% lakini wapo watakaoujua ukweli. Hiyo itakuwa historia mpya.
 
Katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 23/7/2016, Kuna kura mbili.. NDIYO na HAPANA. Kwa utaratibu wa CCM kura ya Ndiyo huwa inamaanisha "Ndiye sahihi", wakati kura ya Hapana huwa inamaanisha "Hahapa mwingine zaidi yake". Kwa hivyo Magufuli lazima apewe Uenyekiti
 
Nasema nitakuwa wa mwisho. Makundi ya watu waliopita mikoani na maburungutu ni mengi mno .

Kuna mtu aliyetembeza maburungutu kama lowa......Mwisho wa siku alikatiliwa mbali na CCM na maburungutu yake sembuse hao wasiojulikana hata majina!!!

Cha msingi usitoroke kwenye hili jukwaa.Waambie hata kama wana maburungutu hawakatizi
 
Back
Top Bottom