Siipendi chadema Bali wana chadema. Hivi mwenyekiti Wa ccm oh sorry mwenyekiti Wa chadema huwa anakujaga humu jamvini? Maana zile topics za kuwa na data base ya wanachadema wote sijui ilifikia wapi. It was a good idea na ile ya kuaza kutengeneza mashina huku mitaani. Mimi nitajitahidi kutengeneza hata mashina manne na kila shina naweka laptop kwaajili ya kupata habari motomoto kutoka jamii forum. Nafkiri jamii forum ni shule tosha kwa mashina kuhusiana na elimu ya uraia
love chadema too. sioni ccm ikifika 2015 salama (QUOTE)
Hii ni hadithi ya FISI aliyemfuata binadamu kwa umbali mrefu akidhani mkono wa binadamu utadondoka. Lakini haukudondoka na mate ya FISI yakazidi kutiririka kama chemchem na akaamua kutafuta mifupa.
Mkuu hii elimu inabidi ianzie kwa CCM, kwani wao wangeweka maslai ya Taifa mbele tusingekuwa hapa tulipo! Angalia sasa kutanguliza maslahi ya chama kwa kuwakumbatia mafisadi badala ya Taifa ndo kunawachimbia kaburi na 'soon and very soon' wataelekea kwenye nyumba ya milele!
Siichukii...lakini naipenda Tanzania zaidi.
Nawapenda Wa-TZ wenye uchungu wa ukweli na nchi hii. Hivyo nampenda saaaana Dr Slaa kwa vile yupo kwenye kundi hili.
Dr Slaa hata angekuwa CCM ningempenda, kama nilivyokuwa nampenda Mpendazoe wakati bado yuko kule.
Ng'wanangwa uko sawa kabisa. Tuache ushabiki wa kinafiki hapa. Katika nchi ambayo katiba ilisha expire kama Tz, huwezi kusema eti unaweka mbele maslahi ya taifa mbele wakati uko nje ya chama cha siasa. Lazima kwanza utafute chama makini, ambayo imeonyesha dhamira ya dhati katika kutetea na kuyeendeleza maisha na maslahi ya wananchi wake. Hapa Ng'wanangwa ameeleza ukweli bila unafiki kuwa chama makini ni CHADEMA kutokana na sera zake za kuwaletea watz maendeleo. Inawezekana Ng'wanangwa kanywa mpaka maji ya bendera, lkn ujumbe wake ni wa msingi kwa wapenda maendeleo.
Nampenda zaidi slaan kwa sababu ya uzalendo wake ana uchungu na nchi waanzania wanaoishi maisha ya duni wakati mafisadi wanafurahia maisha na kodi za wanyonge slaa hata kama angekuwa chichiem ningempenda tu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.