Mimi ni Nani?

Bin Chuma75

JF-Expert Member
Dec 15, 2012
994
1,067
Huwa najiuliza hili swali mara nyingi, mimi ni nini? Maana najikagu naona mguu wangu, naona mkono wangu, naona kichwa changu, naona kiwiliwili changu, hapo vyote naona ni vyangu, sasa mimi ni kipi?

Wanasayansi wanataka kuweka kichwa cha binadamu mwingine kwenye mwili mwingine, najiuliza nikitolewa kichwa kikawekwa kingine bado nitakuwa mimi?

Mshana Jr. Mzizi mkavu na wengine mniambie.
 
MTV MBONGO@ wanasayansi wapo hatua za mwisho kukamilisha hilo zoezi
 
Huwa najiuliza hili swali mara nyingi, mimi ni nini? Maana najikagu naona mguu wangu, naona mkono wangu, naona kichwa changu, naona kiwiliwili changu, hapo vyote naona ni vyangu, sasa mimi ni kipi?

Wanasayansi wanataka kuweka kichwa cha binadamu mwingine kwenye mwili mwingine, najiuliza nikitolewa kichwa kikawekwa kingine bado nitakuwa mimi?

Mshana Jr. Mzizi mkavu na wengine mniambie.
WEWE ni mjumuiko wa roho, nafsi na mwili. ukiondoa roho inabaki maiti, roho ni hiyo pumzi ya Mungu iupao mwili uhai, roho haionekani bali mwili ndio unaoonekana.Roho huongea japokuwa unaweza ukawa upo kimya lakini unaisikia inaongea na hapa ni tofauti na kuwaza WEWE mwenyewe...sijui kama huwa inakutokea..unaweza kusikia jambo halafu ukawaza kichwani na kufanya maamuzi lakini roho akawa hakubaliani nayo na unahisi kama kuna mtu ndani anakukataza. Hivyo mkuu WEWE sio kitu kimoja bali ni: roho +nafsi+mwili= WEWE

Asante
 
Uko vizuri, kibiblia wameiweka hivi
Udongo(mwili) + pumzi(roho)=nafsi hai
 
Back
Top Bottom