Mimi ni mtu mzito zaidi

IrDA

JF-Expert Member
Aug 26, 2010
743
350
Siku moja wapenzi wa timu za Yanga na Simba walikuwa wakibishana ambapo kila mtu alisema lake kwa mtazamo wake.


Mzee mmoja yeye alionekana kuwa na hasira zaidi akaanza kuongea kwa sauti kubwa akitoa kashfa kuhusu viongozi wa nchi huku akisisitiza kuwa uongozi uliopo madarakani ni uozo mtupu hakuna hata zuri moja walilolifanya tangu washike hatamu.


Wakati akiropoka hayo jamaa mmoja alimuuliza yule mzee ni kwa nini anatoa kashfa kwa viongozi?


Mzee alimtazama yule jamaa kuanzia chini hadi juu, akamuuliza, “Wewe ni kama nani unayeniuliza hivyo?”


Washambenga wakiwa wameshajaa, yule jamaa alitaka sifa akatoa kitambulisho chake aliwaonesha watu wote waliokuwepo.


Kitambulisho hicho kilionesha kuwa jamaa ni afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la polisi, kisha akaongea kwa sauti ya juu mimi ni mtu mzito, naweza nikamtia ndani huyu mzee na asionekane tena.


Katika hali ya kushangaza mzee naye akasema “Mimi ni mzito zaidi yako na ndiye niliyewaweka viongozi madarakani kitambulisho hiki hapa..,


Kabla hajakitoa watu wote walitulia na kumuangalia kwa makini..., alipokitoa na kukionesha juu..., watu wote walivunjika mbavu kwa kicheko..., kilikuwa ni kitambulisho cha mpiga kura.
 
Kwa nchi zenye kufuata demokrasia halisi mtu wa pili ni mzito zaidi
lakini kwa nchi hii, yeye ni mdharauliwa (kinyume cha mheshimiwa)
 
Back
Top Bottom