Kongosho
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 35,987
- 24,234
haya huwa ni mameno ya kijana mmoja hapa mtaani kwetu.
Kisa chake kiko hivi.
Kijana huyu alizaliwa baada ya mama yake kupewa ujauzito na mme wa dada yake (shemeji) aliyekuwa anamlea mama yake.
Yule kijana akalelewa na mjomba wake na kusomeshwa hapo.
Kijana huyu hakuwahi kutaka mahusiano na baba yake kabisa. Hata amwite vipi alikuwa haendi, hata akiulizwa baba yake nani atajibu simjui ama hayupo ama jibu lolote lakini hakuwahi kumtaja yule baba.
Kijana huyu ana kazi, lakini ni mlevi mlevi mno, tena kazi nzuri ambayo tangua anaanza kazi mwaka '95 angekuwa mbali sana kimaisha.
Akiambiwa, ujue huo ulevi unajiabisha? Jibu lake huwa 'mie mwenyewe ni aibu tu tangu kuzaliwa kwangu, mtu gani sina hata baba?'
huyu baba yake aliugua muda mrefu akawa anamwita hapo waongee hakuwahi kwenda, ila kwenye msiba alienda na alishiriki kama mtu mwingine yeyote.
Sasa nachojiuliza, ni kwamba kijana huyu alishindwa kubeba aibu ya mama yake ya kuzaa na shemeji aliyemlea?
Na kitu kama hiki huwa kipo kweli cha mtoto kushindwa kusamehe mzazi?
Na kama kipo anaweza saidiwaje? Rehab?
He is such a wonderful soul basi tu sijui kachanganyikiwa na nini?